5.6 Matendo ya
Utukufu:
Kisha kufa na Kristu tafakari ya rozari yatufufua pamoja na
Kristu; kuuonja utukufu wake anapofufuka na anapopapaa mbinguni, kuonja furaha
pamoja na Mama Bikira Maria aidha wote waliosikia habari kwamba Yesu amefufuka
na kumwona mzima tena. Uwe pamoja na Mama siku ya Pentekoste na umshudie Mama
akipalizwa mbinguni na kuwekwa Malkia wa
mbingu na dunia. Twangojea ukamilifu wa Kanisa na ulimwengu mzima, wakati sisi
wenyewe tunaitangazia dunia nzima
Injili.
5.7.Sala ya rozari ni mdundo wa maisha ya mtu. Kumtafakari
Kristu kupitia Mama Maria. Kusali rozari ni kumkabidhi Bwana Yesu pamoja naye
Mama Maria mizigo yetu yote.
Ahadi za Mama kwa
wanaosali rozari:
(alizowakabidhi
Mtakatifu Dominiko na Mwenye heri Alan)
1.Yeyote anayenitumikia kwa kusali rozari tutampa neema
kadhaa nyingi na kubwa, tena basi za pekee.
2. Naahidi kwamba wote wanaosali rozari nitawalinda sana na
kuwapa neema nyingi kabisa.
3.Rozari itakuwa kwao nguo ya kuwakinga wasiingie motoni,
itakomesha mwenendo mbaya hatua kwa hatua, itawaponya mwelekeo wa kutenda
dhambi, watashinda uasi wa kukana kweli
mbalimbali za Imani na maadili ya kimungu.
4.Rozari itaimarisha fadhila na maadili mbalimbali ya kimungu,
itadumisha na kustawisha matendo mema, itawawezesha wenye kuisali
watubu na kupata msamaha mwingi wa Mwenyezi Mungu.
5.Mtu yeyote anayejitoa na kujiweka kabisa mikononi mwangu
kwa kuisali Rozari, kamwe sitamwacha afe katika hali ya dhambi ya mauti na wala
hataonja moto wa milele.
6.Ninaahidi pia kwamba ajali mbaya wala mikosi haitamshinda
mtu yeyote anayesali Rozari kwa ibada, huku akiyakumbuka na kuyatafakari
matendo makuu ya kazi ya ukombozi ambayo rozari hukumbusha, kuhimiza na
kumwezesha mtu ayatende katika maisha yake.
7.Yeyote anayefanya bidii ya kuisali rozari vema, na mara
kwa, hakika atapokea sakramenti za Kanisa kabla ya kuyaacha makao haya ya muda.
8.Watu wanaosali rozari kadiri nilivyoagiza(yaani rozari
nzima, kwa ibada kila siku) Mungu ataangaza nyoyo zao kwa nuru yake na kuwajaza
neema zake wakati wangali wanaishi hapa duniani na saa yaa kufa kwa Mungu
atawapokea mbinguni na kuwashirikisha tuzo na mastahili ya Watakatifu.
9.Nitawaondoa Toharani wale wote wanaojitahidi na kukazana
kusali rozari kwa ibada.
10.Wana wa rozari waingiapo mbinguni tutawatunza kwa utukufu
wa kiwango cha juu sana.
11.Kwa njia ya rozari niombeeni chochote name nitawapeni.
12.Katika shida zote, nitawasaidia kwa namna ya pekee wale
wote wanaotangaza na kueneza rozari.
13.Mwanangu Yesu
amenikubalia kwamba, wale wote wanaotetea rozari iweze kusaliwa na kutumiwa,
tutawapatia Malaika na Watakatifu wote wa mbinguni ili wawaombee katika maisha
yao yote na katika saa yao ya kufa.
14.Wote wanaosali rozari ninawahesabu ni watoto wangu na
ndungu za Mwanangu wa pekee, Yesu Kristu.
15.Kusali rozari kila
siku kadiri nilivyoagiza ni ishara ya kuitwa na Mungu Mwenyezi kuingia
Mbinguni.
Namna ya kusali
rozari.
Kumbuka .
Mafungu yote 20 ya Rozari ya Fatima, nay ale 7 ya Rozari ya
Mateso Saba ya Mama Bikira Maria, yanaposaliwa mfululizo ile sehemu ya wali,
yaani kuanzia Kanuni ya imani hadi Salamu Maria 3 za kuomba imani, matumaini na
mapendo, husaliwa mara moja tu. Mafungu hayo lakini yakisaliwa kwa nafasi
mbalimbali, yaaani mafungu ya Furaha pekee, mafungu ya nuru pekee, na
kadhalika, hapo kila safari rozari huanzia na Kanuni ya Imani. Au na ile Baba
yetu ya kwanza kabisa.
Matendo ya Furaha = Matendo ya Uchungu.
+Matendo ya Nuru
- Matendo ya Utukufu.
Sala ziundazo rozari
1.Ishara ya msalaba:
(mwanzo na mwisho)
Kwa jina la Baba na La Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
2. Kanuni ya Imani:
Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi, Mwumba Mbingu na Dunia. Na kwa Yesu Kristu, Mwanae
wa pekee Bwana wetu, aliyetungwa kwa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria,
akateswa kwa mamlaka ya Ponsio Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashuka
kuzimu, siku ya tatu akafufuka katika wafu,akapaa mbinguni, amekaa kuume kwa
Mungu Baba Mwenyezi, toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu. Nasadiki kwa
Roho Mtakatifu, Kanisa katoliki, Ushirika wa Watakatifu, maendeleo ya dhambi,
ufufuko wa miili, uzima wa milele.
Amina.
3.Baba Yetu.
Baba Yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako
ufike. Utakalo lifanyike, duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila
siku.Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie
katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina.
4.Salamu Maria;
Salamu Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe. Umebarikiwa
kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu,
Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
5.Atukuzwe Baba:
6.Waridi:(sala tatu
pamoja:Sala ya Fatima ya kuombea wakosefu, sala ya Tobara kuombea marehemu,
Tuwasifu milele Yesu, Maria na Yosefu.
Ee Yesu utusamehedhambi zetu. Utukinge na moto wa milele.
Uongoze roho zote Mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.
Damu ya Kristu, iziokoe roho zinazoteswa Toharani, uzitie
nuru ya uzima wa milele.Amina.
Mama na Mwana,
mtujalie kuishi mnayosema, na kupata mnayoahidi.
Maandilizi ya Kiroho.
1.Kwa neema yako
Mungu Mwenyezi(Sala ya Papa Yohane Paulo II)
K.Kwa jina la
Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.
W.Amina.
K.Kwa neema yako
Mungu Mwenyezi , imani na tafakari, tunaanza(naanza) sala hii ya rozari; safari
yetu(yangu) ya kiroho pamoja na Bwana Yesu, Mama Maria na Malaika, ya kuja
kwako Baba wa milele.
Tunapotafakari (ninapotafakari) matendo haya mateule ya kazi
ukombozi, yaliyochaguliwa miongoni mwa matendo mengi mengine, tunaomba(ninaomba) Mwenyezi Mungu
ujaze mioyo yetu kwa furaha ya Krismas; Bwana Yesu nuru ya dunia, angaza
ulimwengu mzima, Kanisa lako, Tohara na Limbo, na familia zote, nawe Mama yetu
Bikira Maria utuombee wanao wote wanyonge na wakosefu neema ya kushiriki
kikamilifu pamoja nawe raha na mateso ya Kristu na yako mwenyewe, hatimaye
utukufu wa ufufuko, milele na milele.
W.Amina.
2.Tunakuabudu Mungu
mmoja.
K.Baba wa
mbinguni, Bwana Yesu Kristu, Mungu Roho Mtakatifu mfariji.
W.Tunakuabudu
Mungu mmoja katika Umoja wa Utatu Mtakatifu na kukiri pamoja na Malaika.
Mtakatifu, Mtakatifu,Mtakatifu, Bwana Mungu wa Majeshi Mungu
uliyekuwepo, uliyepo na unayekuja.
Nawe Bikira Maria, Mama wa Mungu, Malkia wa Mbingu na dunia
na wa viumbe vyote, pokea pia salamu yetu wanao. Malaika na Watakatifu wote wa
Mbinguni, karibuni. Twaomba, iwapendeze nyote, kwa namna ya pekee kusali pamoja
nasi, wana wenu tuliokusanyika hapa leo.
Tunakuomba pia, Mama yetu Bikira Maria ikupendeze
pamoja na wakazi wa mbinguni kuwahudumia
watoto wale ambao wanatamani kuwa hapa lakini wameshindwa kufika. Kwa pamoja
tusaidieni tuweze katika nafasi Mwenyezi Mungu jinsi anavyostahili, anayeishi
na kutawala milele. Amina.
3.Kumkaribisha Roho
Mtakatifu.
K.Karibu Mungu Roho Mtakatifu Mfariji, utuangaze na ututie
nguvu mpya tuweze kuadhimisha vema ibada hii ya rozari takatifu.
Wimbo/Sala:
Kiitikio:Uje Roho
Mfariji, shusha kwetu vipaji, Roho Mungu
njoo.
K.1.Tushushie hekima, tukupende daima, Roho Mungu njoo.
2.Tunaomba akili, tufahamu imani, Roho……….
3.Tusaidie kwa ushauri, tuchague vizuri, Roho………..
4.Nguvu iwe tayari, tushindane hodari , Roho………..
5.Utujaze elimu, mafundisho yaelee, Roho……..
6.Tuwashie ibada, na uchaji wa Mungu, Roho……..
4.Kuomba toba.
K.Ndungu zangu sote hapa tu wakosefu. Tukisema kwamba hatuna
dhambi twazidanganya nafsi zetu wala ukweli haumo ndani yetu. Papo hapo Mungu
ni mwingi wa huruma, hana hasira. Hivyo, tukiri sasa makosa yetu, tumwombe
msamaha kwa ajili ya dhambi zetu wenyewe, dhambi za ulimwengu wote na hasa wale
wasiomkiri Mungu, wasiokumbuka kabisa kutubu aidha walio mahututi, pia kwa
ajili ya roho walioko Toharani na watoto wachanga waliokufa bila kubatizwa.
K.Nakuungamia
Mungu Mwenyezi,
W.Nanyi ndungu.
Kwani nimekosa mno ,kwa mawazo, kwa maneno,
kwa vitendo na kwa kutotimiza wajibu . Nimekosa mimi, nimekosa mimi,
nimekosa sana. Ndiyo maana nakuomba Maria mwenye heri, Bikira daima, Malaika na
Watakatifu wote, nanyi ndungu zangu. Niombee kwa Bwana Mungu wetu.
Amina.
K.Mungu Mwenyezi
atuhurumie, atusamehe dhambi zetu, atufikishe Kwenye uzima wa milele.W.Amina.
5. Kujikabidhi kwa
Mama Bikira Maria.(rejea kwenye ukarasa wa mwanzo katika blogi)
MATENDO YA ROZARI
TAKATIFU NA LITANIA YA MOYO IMMAKULATA.
Rozari ya
Fatima:Matendo ya Furaha:
Nia:Tunapokumbuka
miaka 12 ya utoto wa Bwana Yesu tuombe Mungu atujalie amani na imani kwake kwa
ajili ya Tanzania na ulimwengu.
Wimbo:Ahadi imetimia.
1.Ahadi imetimia,
furaha ya Noeli,
Ndiyo ya Nazareti yafuta ya Edeni,
-Nuru imeingia ulimwenguni, amani kwa watu wenye mapenzi
mema.
2.Mtamaniwa wa Israeli, Mwokozi wa dunia, wanamfia wachanga,
wazee wamsujudia.
-Anapokimbilia kule Misri, aiambia Afrika: Amani kwako.
3. Siku tatu hekaluni, amefunza Viongozi, majilio yake
mawili, uchambuzi wa ajabu.
- Leo Nuru ni kondoo wa kuchinjwa, kesho wa wote Hakimu mtukufu.
Matendo ya Furaha.
1.Malaika anampasha habari Maria kwamba atakuwa Mama wa
Mungu
-Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu.
Waridi:Baada ya kila
fungu(fumbo) la rozari husaliwa
-Tuwasifu milele Yesu, Maria na Yosefu.
-Ee Yesu, utusamehe dhambi zetu, utukinge na moto wa milele.
Ongoza roho zote mbinguni, hasa za wale wanaoitaji zaidi huruma yako.
-Damu ya Kristu, iziokoe roho zinazoteswa toharani, izijalie
nuru ya uzima wa milele. Amina
-Mama na Mwana, mtujalie kuishi mnayosema na kupokea
mnayoahidi.
Amina.
2. Maria anakwenda kumtembelea Elizabeth.
-Tumwombe Mungu atujalie
mapendo ya jirani
Waridi:Tuwasifu……….
3.Yesu anazaliwa Betlehemu.
-Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara
Waridi:
4.Yesu anatolewa
hekaluni.
-Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo
Waridi:
5.Maria anamkuta Yesu hekaluni
-Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
Waridi:Tuwasifu……
WKW.Husaliwa kila
baada ya matendo matano, na mwisho wa Rozari ya Mateso 7:
Rozari ya
Fatima:Matendo ya Nuru.
Nia:Tunapokumbuka
miaka mitatu ya mwisho ya ujana wa Bwana Yesu tuliombee Kanisa, tohara na
Limbo, pia roho sugu wamrudie Mungu.
Wimbo:Walipoona nuru
(i)Walipoona nuru ya Baba,/
Wakaisikia na sautin yake,…
Petro alikiri:/ Ni vema sisi kuwapo hapa!
(ii)Sasa tekeni, asema Yesu, /mpekeeni mkuu wa meza
Wakashangaa: / Siyo maji, ni divai njema!
(iii)Yesu mtoni Yordani, / Roho ashuka, Baba anena;
“Msikieni yeye” /Mwanzo mkuu wa ubatizo.
(iv)Kuleni, huu mwili wangu, / Kunyweni, Hii damu yangu,
Alisema Yesu. /Kaeni katika pendo langu.
(v)Na walio gizani tubuni, / Ufalme wa Mungu u karibu, Yesu
atangaza, /ndimi Nuru ya ulimwengu.
Matendo ya Nuru.
1.Yesu anabatizwa
mtoni Yordani.(Mt. 3:15)
Yesu alimwambia Yohane Mbatizaji:
Ukubali hivi sasa, unibatize, tupate kutimiza haki yote.
-Tuombe neema ya kumtii Mungu kuliko chochote.
Au: Mbingu
zikafunguka; Baba anena:
Huyu ni mwanangu mpendwa wangu.
Na Roho Mtakatifu ashuka mfano wa njiwa.
-Tuombe nuru tuukiri Utatu Mtakatifu na kushiriki vema kazi
ya ukombozi.
Waridi: Tuwasifu……..
2.Yesu anageuza maji
kuwa divai katika harusi ya Kana.
(Mt. Yoh. 2.3, 5)
Mama Bikira Maria
alimwambia Yesu: Hawana divai.
Kisha akawaambia watumishi: Lolote atakalowaambia fanyeni.
-Tuombe neema ya
kumheshimu , kumsikiliza na kumtii Mama wa
Mungu siku zote.
Waridi….
3.Yesu
anahubiri(Mt.4:12,17)
Yesu alikwenda mpaka
Galilaya, akaanza kuhububiri na kusema;
Tubuni, kwa maana ufalme wa
Mbingu umekaribia.
-Tuombe neema ya kuweka miyoni mwetu kila neno litokalo kwa
Mungu na kulitenda.
Au: Tuombe tumpokee
kwa imani Kristu, Nuru ya dunia na Mkombozi wetu.
Waridi…
4.Yesu anageuka sura.(Mt.
17:5)
Mungu alinena kutoka mbinguni Huyu ni mwanangu, mpendwa
wangu, Ninayependezwa naye, msikieni yeye.
-Tuombe neema ya kumsikiliza Yesu na kutenda asemayo,
atujalie nuru ya kumwona uso kwa uso milele yote.
Waridi…
5.Yesu anaweka
Ekaristi Takatifu(Mt. 16,26-28, Lk.22:17-20).
Katika karamu ya mwisho Yesu aliwaambia Mitume wake, Huu ndio mwili wangu, uleni. Hii ndiyo damu
yangu, inyweni. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi.
-
Tuombe neema: Kamwe tusiikufuru Ekaristi
Takatifu, nuru ya pendo la Yesu,sadaka timilifu.
-
Waridi…..WKW.
Rozari ya
Fatima:Matendo ya Uchungu.
Nia:Tunapokumbuka
wiki ya mwisho ya maisha yake Bwana Yesu tuwaombee wagonjwa,wafungwa, wasafiri
na wenye shida mbalimbali za maisha.
Wimbo:Kikombe cha
moto.
(i)Kwa ajili yetu, umekwenda ile njia, ya ghadhabu yake
Mungu.
(ii)Kwenye ile bustani, iliyofumbata msiba, ‘imetoka jasho
la damu.
(iii)Ukakumbwa upweke, mijeredi ukapigwa, taji la
miiba’kavikwa.
(iv)Kikombe cha moto kile, msalaba ukabebeshwa, mtini
ukaangikwa.
(v)Mtu wa masikitiko, huzuni hiyo ya kwako,’tutie nuru na
toba.
Matendo ya Uchungu.
1.Yesu anatoka jasho la damu.
- Tumwombe Mungu atujalie sikitiko timilifu.
Waridi:Tuwasifu……
2.Yesu anapigwa mijeredi.
-Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.
Waridi.
3.Yesu anatiwa miiba kichwani.
-Tumwombe Mungu kushinda kiburi
Waridi.
4.Yesu anachukuwa msalaba.
-Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taaba.
Waridi….
5.Yesu anakufa msalabani.
-Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.
Waridi…WKW
Rozari ya Fatima:
Matendo ya Utukufu.
Nia:Tunapoifurahia Pasaka ya Bwana Yesu na kipindi kizima baada
ya ufufuko wake tuombee familia, wajane na yatima, wanafunzi na wakimbizi.
Wimbo:Uhai
umepatikana.
(i)Bendera za kifalme, kokote zapepea , Uhai ‘mepatikana.
(ii)Utatu Mtakatifu, sifa tunakuimbia Kristu mzima kafufuka.
(iii)Kristu mbinguni kapaa, kulia umekalia mshindi wa mauti.
(iv)Hongera Mama
Maria, Mbinguni umepalizwa roho pamoja na mwili.
(v)Mbinguni Mungu yu Baba, Mwana ndiye Mfalme, Mama na
Malkia ni wewe.
Matendo ya Utukufu.
1.Yesu anafufuka.
-Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.
Waridi:Tuwasifu…..
2.Yesu anapaa mbinguni.
-Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu
Waridi.
3.Roho Mtakatifu anawashukia Mitume.
-Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.
Waridi.
4.Bikira Maria anapalizwa mbinguni.
-Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.
5.Bikira Maria anawekwa
Malkia mbinguni.
-Tumwombe Mungu atujalie kufa vema.
Waridi….WKW.
Rozari ya Mateso saba
ya Mama Bikira Maria.
Wimbo:Mama pale
msalabani.
(i)Mama pale msalabani,
macho yatoka machozi, akimwona Mwanae.
(ii)Kweli vile akilia, uchungu kama upanga ukampenya moyowe.
(iii)Mwenye moyo mgumu nani, asimhurumie basi Mama mlilia
Mwana?
(iv)Ewe Mama mtakatifu, usulibiwe na Yesu, moyo wangu wa
dhambi.
(v)Nae Mwokozi niteswe, madonda nigawiwe, pamoja na
Mkombozi.
(vi)Nisimame msalabani, niwe name wako mwenzi, wa uchungu na
msiba.
Mateso 7.
(Kila teso hutanguliwa na sala fupi ifuatayo)
Majonzi na mateso ya
Mama Maria wa Yesu hayana mfano.
1.Mzee Simeoni aliagua
kwamba Bikira Maria atachomwa upanga moyoni.
-Tuombe neema ya kuvumilia mateso. Mama wa mateso, utuombee
Waridi:Tumsifu……
2.Mama Maria na Yosefu walikimbilia Misri usiku ili kumficha
Yesu asiuawe na Herodi.
-Tuombe neema ili mioyo yetu iwe kimbilio lake Yesu.
Mama wa mateso, utuombee.
Waridi.
3.Mama Maria aliona uchungu sana Mtoto Yesu alipopotea kwa
muda wa siku tatu,
-Tuombe neema ya kudumu na Yesu mioyoni mwetu.
Mama wa mateso, utuombee.
Waridi.
4.Bikira Maria alikutana na Yesu katika njia ya msalaba.
-Tuombe neema ya kudumu na Yesu siku zote .
Mama wa mateso,
utuombee
Au:Tuombe neema
nasi tubebe hodari misalaba yetu siku zote
Mama wa mateso,
utuombee.
Waridi
5.Bikira Maria alimwona Mwanae akitundikwa msalabani;
Akasimama chini ya huo msalaba kwa muda wa masaa sita.
-Tuombe neema ya kufa mikononi mwa Yesu na Mama Maria.
Mama wa mateso ,utuombee.
Waridi.
6.Mama Maria alimpokea Mwanae na kumpakata miguuni pake
kisha shushwa msalabani.
Alishiriki kikamilifu mateso ya Mwanae kwa ajili ya dhambi
za wanadamu.
-Tuombe neema ya kutotenda dhambi.
Mama wa mateso, utuombee.
Au Tuombe neema
ya kumpokea Yesu wa Ekaristi Takatifu kwa ibada na uchaji sikuzote.
Mama wa mateso, utuombee.
Waridi.
7.Mama Maria alirudi kwa majonzi nyumbani kisha kumzika
Mwanae Yesu.
-Tuombe neema ya kitulizo kwa Mama Maria katika mateso yetu.
Mama wa mateso, utuombee.
Waridi….WKW
Litania ya Moyo
Immakulala wa Maria.
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristu utuhurumie
Kristu utuhurumie
Bwana utuhurumie
Baba wa mbinguni, Mungu
utuhurumie
Mwana, Mkombozi wa dunia, Mungu utuhurumie
Roho Mtakatifu, Mungu
utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja utuhurumie
Moyo Immakulata wa Maria ulioshiriki kikamilifu kazi ya
ukombozi ya Mwanae utuombee.
Moyo unaochomwa kila siku kwa kuona roho nyingi
zinateketea utuombee.
Moyo Immakulata uliojaa upendo kwa binadamu utuombee.
Moyo Immakulata unaohuzunika kwa dhambi za binadamu utuombee
Moyo Immakulata unaotamani kutulizwa na binadamu kwa njia ya
rozari Takatifu utuombee
Moyo Immakulata unaotamani kuvuta roho zote ziingie katika
Ufalme wa mbingu.
Moyo Immakulata unaosikiliza kilio cha watoto wake dhaifu na
wanyonge. Utuombee.
Moyo Immakulata ambao uko tayari kumfariji kila
anayemkimbilia utuombee.
Moyo Immakulata unaoalika siku hadi siku.
“Njoni mkamiminiwe neema zitokazo katika Moyo huu” utuombee
Moyo Immakulata unaoomba daima,
“Fanyeni malipizi mahali mahali pa wakosefu wote” utuombee.
Moyo Immakulata unaokumbusha daima ,
“Waombeeni marehemu
Toharani bwanaoteseka na ambao hakuna anayewakumbuka” utuombee.
Moyo Immakulata unaoagiza kwa upendo;
“Waombeeni pia watoto wachanga wanaokufa bila ubatizo utuombee.
Moyo Immakula unaohimiza daima:” Uombeeni ulimwengu amani ya
kweli pamoja na imani thabiti kwa Mwenyezi Mungu” utuombee.
Moyo Immakulata unaohiza daima:”Liombeeni Kanisa na hasa
viongozi wake na Watendakazi wote Mama Maria”
utuombee
Sehemu ya pili.
Moyo safi wa Maria, baada ya moyo wake Mungu mwenyewe utuombee.
Moyo safi wa Maria,
Ee chombo cha Roho Mfariji utuombee.
Moyo safi wa Maria, goroto la Utatu Mtakatifu utuombee.
Moyo safi wa Maria, makao ya Neno la Mungu utuombee.
Moyo safi wa Maria , mkingiwa dhambi tangu kuumbwa. Utuombee.
Moyo safi wa Maria, unaofurika neema
utuombee.
Moyo safi wa Maria,
mbarikiwa kati ya mioyo yote. Utuombee.
Moyo safi wa Maria, kiti cha enzi cha utukufu utuombee.
Moyo safi wa Maria, bahari ya unyenyekevu utuombee.
Moyo safi wa Maria, sadaka ya mapendo utuombee.
Moyo safi wa Maria, uliosulubishwa wakati umesimama chini ya msalaba. Utuombee.
Moyo safi wa Maria, mtuliza wenye huzuni. Utuombee.
Moyo safi wa Maria, makimbilio ya wakosefu utuombee.
Moyo safi wa Maria, matumaini yao wanaozimia. Utuombee.
Moyo safi wa Maria, makao ya huruma utuombee.
Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za dunia utusamehe
ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za dunia utusikilize
ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za dunia utuhurumie.
K.Moyo
Immakulata, mpole na mpole na mnyenyekevu,
W. Utufanye mioyo
yetu ifanane na Moyo wa Yesu.
Tuombe, Mungu
mwingi wa huruma, ili kuwajalia wakosefu wokovu na wanyonge makimbilio,
umeufanya Moyo Immakulata wa Mama Maria ufanane sana na Moyo wa Yesu kwa wema
na huruma zao.
Twaomba, utujalie nasi tunaoheshimu Moyo huu Immakulata
mtamu na uliojaa upendo, tustahili kuishi katika kuifuhasa Mioyo miwili
iliyoungana, ya Mama na Mwanae. Kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina.
Sala za Mwisho
Kamwe
hatukuachi.(Papa Yohane Paulo II)
Kamwe hatukuachi, Ewe rozari takatifu ya Mama Maria, Cheni
itufungayo na Mungu, mkufu wa upendo utuungao na Malaika, mnara imara utukingao
na maoteo ya shetani, bandari salama katika bonde kubwa la machozi. Usimpe
shetani nyara za bure, zuia na uzime vita vyote duniani.
Ndiwe faraja yetu saa ya kufa, Ee Malkia wa rozari wa
Pompei, Mama mpendelevu, kimbilio la wateswa, usifiwe popote, leo na daima,
hapa dunia na huko mbinguni.
Amina.
Salamu Malkia.
Salamu Malkia, Mama mwenye huruma, uzima tulizo na matumaini
yetu salaam. Tunakusihi ugenini hapa sisi wana wa Eva.
Tunakulilia, tukilalamika na kuhuzunika bondone huku kwenye
machozi. Haya basi, Mwombezi wetu, utuangalie kwa macho yako yenye huruma. Na mwisho wa ugeni
huu utuonyeshe Yesu, Mzao mbarikiwa wa tumbo lako.
Ee mpole, ee mwema ee mpendevu, Bikira Maria. Amina.
KumbukKumbuka, Ee Bikira Maria mpole sana, haijasikilika
bado hata mara moja, kwamba ulimwacha mtu aliyekimbilia ulinzi wako, aliyeomba
msaada wako na maombezi yako. Kwa matumaini hayo nakukimbilia wewe, ee Mama,
Bikira wa Mabikira. Ninakuja kwako, ninasimama mbele yako nikilalamika mimi
mkosefu, ee Mama wa Neno la Mungu, usikatae maneno yangu, bali upende kuyasikia
na kuyasikiliza. Amina.
Tunakimbilia.
Tunakimbilia ulinzi wako, ee Mzazi Mtakatifu wa Mungu
usitunyime tukiomba katika shida zetu. Utuokoe siku zote kila tuingiapo
hatarini. Ee Bikira mtukufu mwenye Baraka. Amina.
Kwa jina la Baba
na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.