Mt. Athanasius(Atanasi)Askofu na Mwalimu wa Kanisa
(295-373)
Alizaliwa mjini Alexandria(Misri) 295. Mungu alimteua awe Mtetezi Mkuu wa Umungu wa Bwana Yesu dhidi ya Arius aliyefundisha kwamba Yesu ni Mtu tu. mwaka 325 Atanasi alifuatana na Askofu wake Alexanda kwenye mtaguso wa Nisea(Uturuki) kwa nia hiyo ya kupinga uzushi wa Arius.
Baada ya hapo akawa Askofu wa Alexandria, na akaandika vizuri sana kuonyesha na kutetea mafundisho ya kweli.
Baada ya Mtaguso wa Nisea Atanasi bila kuchoka aliendelea kupambambana na wafuasi wa Arius.Hao walimshtaki Atanasi uwongo mwingi kwa Mfalme Konstantino ambaye alimpeleka mara nyingi uhamishoni jangwani pamoja na wakristu waliozinagatia kwamba Yesu ni Mungu-Mtu. Kwa mieze waumini akinena "Tulieni.Leo viongozi wa Kanisa na Mfalme wanamiliki makanisa, na sisi tunamiliki imani katoliki. Baada ya muda sisi tutamiliki vyote viwili: Makanisa na imani katoliki. Na ili kufika mbinguni, zingatia awali ya yote imani katoliki"
WIMBO WA ROHO MTAKATIFU
1.Uje Roho Mtakatifu, Tuangaze toka mbingu Roho zetu kwa mwangao.
2.Uje baba wa maskini, Uje mtoa wa vipaji , Uje mwanga wa mioyo.
3.Ee Mfariji mwema sana, Ee rafiki mwa-(a)-nana,Ewe raha mustrarehe.
4.Kwenye kazi u pumziko, Kwenye joto burudisho, U mfutaji wa majozi.
5.Ewe mwanga wenye heri, Uwajaze waumini, Neema yako mioyoni.
6.Bila nguvu yako wewe, Mwanadamu hana kitu, Kwake yote yana kosa.
7.Osha machafuko yetu, Panyeshe-e-pakavu petu., Na kuponya majeraha.
8.Ulegeze ukaidi, Pasha moto ubaridi, Nyosha upotevu wote.
9.Wape waamini wako, Wenye tumaini kwako, Paji z
ako zote saba.
10.Wape tuzo ya fadhila, Wape mwisho bila, Wape heri ya milele.
11.Amina aleluya, Amina aleluya, Amina aleluya.
(Wakati wa Kwaresima)Amina,amina, (x3)
WIMBO WA EKARISTI TAKATIFU(Ufuatao au mwingine)
1.Ninakuabudu Mungu wangu,unayejificha Altareni,
Ninakutolea moyo wangu, usiofahamu siri yako.
2.Mafahamu yangu yadanganya, yanapokuona na kugusa,
Namsadiki Yesu,hadanganyi, Yeye Mungu Mwana na ukweli.
3.Waficha Umungu Msalabani, na Ubinadamu Altareni.
Nami naungana zote mbili, kama mwivi yule mwenye toba.
4.Tomas aligusa majeraha, nami nasadiki bila shaka,
Ewe Yesu nipe pendo lako, tumaini kwako na imani.
5.Umeteswa nini Bwana mwema, kwa kunipa mkate wa uzima?
Yesu, unifiche ndani yako, ili nionje pendo lako.
6. Yesu Pelicane nitazame, na kwa damu yako nitakase,
Tone moja ndilo linatosha, na dunia yote yaokoka.
7.Ndani ya mafumbo Yesu yumo, atafumbuliwa kwangu lini?
Nikuone, Yesu, uso wako, nishiriki nawe heri yako.
KUJIANDAA KIROHO:
K. Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.
W.Amina.
K. Tukisema kwamba hakuna Mungu.
au kwamba hatumuitaji Mungu,
au kwamba hatuna dhambi,
tutakuwa waongo,
na wala ukweli hautakuwa kinyawani mwetu.
Basi tutafiti kwa kitambo udhaifu wetu na makosa tuliyotenda leo na katika maisha yetu, kisha tumwombe Mungu msamaha......
(Ukimya wa tafakari ya moyo)
K.Sala ya kutubu: Yesu Mwana wa Daudi.
Ee Yesu, Mwana wa Daudi unihurumie
Ee Baba,Mwumba wa vitu vyote,
wewe ndiwe asili ya vyote,
Mwangaza wa milele na chanzo cha kila mwangaza.
Wewe ndiwe umchaguaye mtu katika hali yake ya unyonge,
toka mavumbini, na kumwinua kutoka uharibifu.
Ndivyo ulivyonichagua mimi kwa njia ya Mwanao mpenzi,
ukaniingiza katika uhuru na staha ya watoto wa nyumbani mwako.
Unijalie niwe mtoto mtakatifu nisije nikawa mbele yako pasipo kustaili jina niitwalo,
bali nitimize barabara wito wangu wa maisha yasiyokuwa na lawama.
Laiti niyatimize hayo kwa moyo safi na akili nyofu.
Watu walimletea Yesu mtu mmoja aliyepooza mwili,
amelazwa juu kitandani.
Yesu alipoona imani yao,
akawaambia huyo mtu aliyepooza,
"Jipe moyo, mwanangu! Umesamehewa dhambi zako."
Wafarisayo walisema, "Kwa nini mnakula na kunywa
pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?"
Yesu akawajibu, "Wenye afya hawamhitaji daktari,
Sikuja kuwaita watu wema,
bali wenye dhambi ili wapate kutubu."
"Bwana, sistaili uingie nyumbani mwanga.
Lakini toa neno, na mtumishi wangu atapona.
Yesu akamwambia, "Na iwe kama ulivyoamini."
Yesu, Mwana wa Daudi, unihurumie,
mwanao mnyonge na mkosefu sana,
kama ulivyowafanyia hao wenzangu. Amina
B.Sala ya Mama Bikira Maria.
1.Mfalme wa Wafalme, Bwana na Muumba wa vitu vyote,*
Mbele yako ninasujudu kiumbe wako niliye vumbi na jivu.
2.Nipo hapa kwa nguvu ya neema na upendendelea wako,*
Maana hata sikujua kabisa jinsi ya kukufikia.
3.Hata sasa najiona nasukumwa na wingi wa neema zako,*
nikushukuru.
4.Lakini nitakulipa na nini miye*
ambaye nimepokea kwako kila kitu hata huku kuwepo kwangu kwenyewe?
5.Nitakulipaje mimi mkosefu*
ninayelemewa na wingi wa huruma na baraka za Umungu wako?
6.Nikupe zawadi gani, ewe Mungu*
Miye kiumbe wako nisiyestahili lolote?
7.Nimepata kwako roho yangu, uwepo wangu/
na kila kitu kutoka mikononi mwako*
na naendelea kupokea hata nguvu zangu zote.
8.Naitolea nafsi yangu kwako mara elfu nzima,*
Niwe kwako sadaka ya kukutukuza.
9.Lakini deni langu kubwa/
silo tu, la kupewa nawe kila kitu,*
bali na la kunipa kila kitu kwa upendo mkubwa.
10.Awali ya yote katika viumbe vyote umeniumba Immakulata*
bila doa wala waa la dhambi.
11. Kisha ukaniteua kuwa Mama mzazi wa Mwanao/
nimchukue tumboni mwangu, nimnyonyeshe maziwa yangu*
Miye binti Adamu, mnyonge na vumbi.
12.Natambua jinsi umenipenda mno*
Sina cha kukulipa ila nami nikupende tu/
kuliko kila kitu hata nafsi yangu.
13.Na sasa roho yangu inafurahi na kuchangamka/
Kwa sababu nina kitu mikononi mwangu cha thamani kubwa kuliko zote*
cha kuweza kukutolea kama sadaka tukufu:
14.Ndiye Mwanzo mpenzi*
wa kumzaa wewe mwenyewe tangu milele/
aliye sawa nawe katika utukufu na ukamilifu.
15.Amezaliwa nawe ulipojitambua kaatika Umungu wako,*
Ndiye mfano wako halisi:
16.Ndiye utimilifu wa furaha yako,*
na Mwanao mpendwa wa pekee.
17.Baba wa milele, huyu ndiye sadaka yenyewe/
ninayokutolea ewe Mungu Mwenyezi.*
Naamini itakupendeza, nawe utairidhia na kuipokea.
18. Mimi nilimpokea akiwa Mungu,*
Leo nakutolea akiwa Mungu na Mtu.
19.Hakuna sadaka nyingine bora zaidi kuliko hii/
ambayo mimi wala kiumbe mwingine yeyote aweza akakupa.*
Wala wewe mwenyewe waweza ukadai.
20.Ni sadaka ya thamani kuu*
ambayo naamini itanilipia deni langu lote.
21.Namtolea kwako kwa niaba yake Yesu,
22.Mimi ndimi mama ya Mwanao wa pekee*
Nimempa mwili na kumfanya ndungu ya wanadamu.
23.Maadam ametaka awe Mkombozi na Mwalimu wao,
Yanipasa niwe mshenga wao*
Niwalete mbele yake na kuwaombea msaada wake.
24.Kwa hiyo Baba ya mwanangu wa pekee/
Na Mungu mwenye
huruma,*
Namtolea kwako kwa moyo wangu wote.
25.Kwa njia yake na kwa ajili yake,*
Nakusihi uwasamehe wakosefu wote.
26.Uwamiminie tena neema zako za tangu zama*
Na uwafungulie chemchemi za upatanisho nao.
27.Huyu ni samba wa
Yuda amegeuka kondoo/
Anayeondoa dhambi za dunia.*
Ndiye hazina ya Umungu wako.”Amina.
3.Sala
Tunakuabudu Mungu
Mmoja.
Baba wa mbinguni, Bwana wetu Yesu Kristu,
Mungu Roho Mtakatifu Mfariji,
Tunakuabudu Mungu Mmoja katika Umoja wa Utatu Mtakatifu,
Na kukiri pamoja na Malaika:
Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, Bwana Mungu wa Majeshi.
Mungu uliyekuwapo, uliyepo na unayekuja.
Nawe Bikira Maria, Mama ya Mungu,
Malkia wa Mbingu na dunia na wa viumbe vyote,
Pokea pia salamu yetu wanao.
Malaika na Watakatifu wote wa mbinguni, karibuni.
Twaomba, iwapendeze nyote,
Kwa namna ya pekee kusali pamoja nasi,
Wana wenu tuliokusanyika hapa leo.
Tunaomba pia, Mama yetu Bikira Maria
Ikupendeze pamoja na Wakazi wote wa Mbinguni
Kuwaudumia na watoto wale wote ambao wanatamani kuwa hapa lakini
wameshindwa kufika.
Kwa pamoja tusaidieni tuweze katika nafasi hii,
Na maisha yote, kumsifu Mwenyezi Mungu jinsi anavyostahili,
Anayeishi na kutawala
milele. Amina.
4.Wimbo:Kuwakaribisha
Malaika.
Kiitikio.Malaika
wangu malaika wangu, unilinde mimi niongoze,
Usije ukanitupilia
mbali, mimi wako siku zote X2
1.Ni mapenzi yake Mungu, wewe kuwa wangu mimi,
Niongoze niandae ya neema.
2.Malaika wangu mimi, unilinde siku zote,
Niongoze njia nzuri ya neema.
3.Moto ndio vazi lenu, mwamwabudu Bwana Mungu,
Na milele mnaimba jina lake.
4.Malaika Bwana Yesu,
Mwamliwaza matesoni,
Na ushindi wa Mfufuka mwatangaza.
5.Mungu Baba, Mungu Mwana, Mungu Roho Mtakatifu,
Malaika nasi watu twamwabudu.
5.Sala.
Kujikabidhi kwa Mama
Bikira Maria.
Ee Mungu Mwenyezi, usitutupe wanao wanyonge na wakosefu.
Asante Mungu Mwenyezi, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
Uliyependa kumteua Mama Bikira Maria awe Mama wa Mungu,
Mama wa Mkombozi na Malaikia wa viumbe vyombe.
Asante Bwana Yesu, uliyewapenda wanadamu hadi upeo,
Wala hukusita kumfanya Mama yako wa pekee
Awe mama wa wanadamu wote.
Ukiwa msalabani ulisema:
Mama, tazama
Mwanao; halafu
Mwana, tazama
Mama yako.
Kwa kauli hii moja ulimkabidhi Mama Bikira Maria wanadamu
Wote awapende na kuwatunza kama alivyokufanyia wewe mweyewe.
Asante Mama kwa kukubali ombi la Mwanao,
Mkombozi wetu Yesu
Kristu, la kuwa Mama yetu.
Kwa ahadi nyingi na upendo unatuita daima:
Njooni
kwangu nyote, ndimi Mama yenu .
Mtu
anikimbiliaye na kusali rozari yangu kwa imani na toba, kamwe sitamwacha.
Nitamjalia
Baraka zote anazotamani katika maisha
yake yote.
Na saa ya
mwisho nitampokea katika Nyumba ya Baba.
Ili tupate kushiriki kazi, na kufaidi matunda ya ukombozi.
Mama pia umeagiza kwa upendo mkubwa kuwa:
Wanangu,
ili mpate kupoza hasira ya Mungu juu ya
dhambi za binadamu na kudumisha amani na
Upendo
duniani:
Tubuni dhambi, mrudieni Mwanangu Yesu Kristu, saline
rozari yangu kwa imani kila siku, na wa
Aombeeni wakosefu zaidi na zaidi.
Kwa nafasi hii, Mama Bikira
Maria, sisi wanao wa Sala za
Maombi, huku tukizingatia ahadi zako na maagizo yako tukiwa tumepiga magoti
mbele yako, Mama yetu Bikira Maria, mosi, tunakuomba msamaha kwa makosa yetu
yote tuliyokwisha mkosea Mungu na wewe
Mama yetu tangu utoto wetu hadi hii leo.
Pili, tunakushukuru Mama kwa neema na Baraka zote
ulizokwisha mjalia kila mmoja wetu katika maisha yake, kiroho na kimwili.
Pia tunakushukuru Mama kwa kukubali mwaliko wa Mwenyezi
Mungu kwamba usimamie na uongoze Sala hizi maalum za Maombi.
Asante pia mama, maana kwa
upendo na unyenyekevu unashuka kila siku na kukaa kati yetu na
kutuhudumia katika maswala yote, kimwili
na kiroho, aidha na kwa miujiza mbalimbali unayotuonyesha wewe mwenyewe binafsi
au kupitia watumishi wako mbalimbali.
Pamoja na hayo yote, Mama kwa nafasi hii hii tunaomba kukabidhi rasmi
mikononi mwako nafsi zetu na shida mbalimbali(taja shida zako……..)
Kila tulicho nacho, na kila tulitendalo liwe chini ya
uongozi na usimamizi wako.
Tunaomba pia, Mama
Mtakatifu wa Watakatifu, imarisha
kazi yako, izidi kudumu, ili wanao duniani kote, tuzidi kufaidi matunda yake.
Tunaomba hayo yote kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristu,
anayeishi na kutawala na Baba na Roho Mtakatifu, Mungu daima na milele.Amina.
Sehemu ya Kwanza
Kuabudu Sakramenti Takatifu
(Hata kama sakramenti Takatifu
haipo, sehemu hii husaliwa)
1.Wimbo wa Ekaristi Takatifu:(Ufuatao
au mwingine)
1.Pie
pelicane Jesu Domine,
Me immundum
munda tuo sanguine,
Cujus una
stilla salvum facere,
Totum mundum
quit ab omni scelere.
2.Jesu quem
velatum nunc aspacio,
Oro fiat
illud quod tam sitio,
Ut te
reveleta cernens facie,
Visu sim
beatus tuae gloriae Amen.
2.Sala mbele ya Sakramenti Kuu
Au Natambaa mwokozi wangu.
Bwana asema,
“Amelaaniwa
mtu Yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake na moyoni
mwke amemwacha Mungu.
Mwanangu
sikiliza maneno yangu, tega sikio lako, isikilize kauli zangu.
Zisiondoke
machoni pako, uzihifadhi ndani ya moyo wako,maana ni uhai kwa wale wazipatao na
afya ya mwili wao wote
Mungu
wangu,Mungu wangu, niliyasikia maagizo yako nikayapokea kwa muda. Katika ubichi wa ujana wangu lakini
nikaanza kuyapuuzia, nikaona hayanihusu. Mweyewe nikajituliza na kusema; Roho
ni imara, bali mwili wangu ni dhaifu!
Nikajidanganya
nafsi yangu na kujifariji. Mungu haoni wala hajali nitendayo!
Na hakiona,
yu mwingi wa huruma!
Macho juu,
kifua mbele, nimeambatana na shetani na kumganda mwanadamu. Sikio la kufa
halisikii dawa jamani. Roho yangu leo ni tenga la maovu na hatia za dhambi.
Nao mwili
wangu ni kaya bovu la maradhi.
Shetani
ananisimanga, kanizungushia utandu wake:” Nilikushawishi , katu
sikukulazimisha, dhambi umetenda mwenyewe. Jibu mashtaka mwenyewe!” Namtafuta
mja, simwoni. Lo kanikimbia kitambo!
Mungu mwingi
wa huruma, huhurumia!
Mwanadamu
aweza akahurumia!
Bali
maumbile kamwe hayana msamaha!
Ee nafsi
yangu, zi wapi nguvu za ujanani?
Natambaa,
Mwokozi wangu. Maji shingoni, nakiri. Nimekutenda dhambi wewe peke yako, na kufanya maovu mengi mbele
yako, ee Mungu wangu . Uniponye, ee Bwana nami nitaponyeka. Uniokoe, nami
nitaokoka, Kwa maana wewe ndiwe Mweza peke.
Naona aibu,
Mwanakondoo wa Mungu. Macho chini nakusihi.Unioshe kabisa na uovu wangu katika Damu yako azizi
na maji ya ubavu wako. Unitakase dhambi zangu pamoja na hatia zangu nami
sitarudia tena.
Yesu Mwana
wa Daudi, unihurumie.(Rejea Yer.17:5:14:Mith.4:20-22:Zb.51:3-4)
3.Wimbo:Bwana Yesu Yuko wapi?
1.Bwana Yesu
yuko wapi, mpenzi wangu rafiki?
Njia gani
amekwenda? Nitamwonaje mimi?
Roho yangu
yajutishwa, na dhambi na huzuni,
Yesu mpenzi
wangu mwema, namtafuta kwa bidii.
2.Napaliza
sauti yangu, nalia wapi Yesu?
Ndani mwangu
sina raha, mpaka nimwone Yesu.
Ningekuwa na
mabawa , ningeruka upesi,.
Milimani
mabondeni, kumtafuta Bwanangu.
3.Aondoa
shida zangu, mahararibifu yote,
Nikiona
ta’bu mimi, anituliza yeye.
Nitafanya
bidii sana, kumtafuta popote.
Sitachoka
kutembea, mchana hata usiku.
4. Bwana
Yesu nitokee, roho yangu inakuita.
Niondoe na
maovu, Yesu Mwokozi waNGU.
Utulize hamu
yangu, kaa kwangu daima.
Nikupende
sana wewe, niwe wako milele.
4.Wakati wa mfungo:Sala ya kuomba
Toba
Moyo Mtakatifu wa Yesu.
1.Ee Yesu Bwana wetu, Mungu wetu,
Ndiwe
Mkombozi mtukufu wa watu wote, uliyetupenda mno, hata ukataka kujifumba katika
umbo la mkate ndani ya hostia. Mbele yako sasa tumekusanyika sisi, watu wakosefu
tunaotambua matusi yote yanayotukanisha Umungu wako. Kwahiyo twakuomba:
Mwokozi
mwenye huruma Yesu utuhurumie.
2.Tumekuangukia
sote pamoja tukikuomba toba wazi. Kadiri
tuwezavyo, tunataka kukusaulisha matusi yote yaliyoitukanisha Nafsi yako
takatifu. Matusi hayo twajua ni mengi mno. Yamekuwa mengi wakati wa maisha yako
duniani, mengi katika siku za mateso yako na uchungu, mengi bado siku hizi watu
wanapoitukana Ekaristi Takatifu, siri hii kuu ya upendo wako uliowapenda
wanadamu. Kwahiyo twakuomba.
Mwokozi
mwenye huruma Yesu utuhurumie.
3.Tumekokosea
shukrani Mfalme wetu mwenye moyo mwema kabisa, usiache kutupenda, na mwenye
ukarimu usio na mwisho kwetu japo sisi tunaendelea kukutukana badala ya
kukushukuru.
Mwokozi
mwenye huruma Yesu utuhumie.
4.Kweli
inalitupasa kuwa na machozi ya damu, kuzililia dhambi zetu zilizozidi mno!
Toba, Bwana, kwa ugumu wa mioyo yetu, kwani tumekuacha mara nyingi mno,Toba,
kwa kusahau mema yako na mapendo yako makuu. Toba, Bwana kwa dhambi zetu
nyingi, nyingi za kila siku na kuzidi za kuchukiza kabisa. Toba kwa matusi ya
jinsi zote, ya mawazo, maneno na matendo, Toba kwa ukosefu wa heshima katika nyumba ya Mungu. Toba hasa ya kumunyo nyingi za kufuru
Mwokozi mwenye huruma Yesu utuhurumie.
5.Sogeeni Mitume wa Mungu, sogeeni enyi watu waadilifu, sogeen, nanyi mabikira, mliowekwa kumtumikia Mwanakondoo asiye na
6. Ee Bwana, ukiyakubalia machozi yetu na majuto,tuondolee
makosa yetu sisi maskani, tufae bado kuungana nawe.
Mwokozi
mwenye huruma Yesu utuhurumie.
7. Kwamba u sadaka yetu, twaomba ruhusa kuitwaa sadaka hiyo,
tumtolee Baba yako heshima yakufaa.Tunataka kukutolea mioyo yetu, iwe yake Moyo
wake, na hasa tunaomba tufae kukupenda na kukuabudumilele. Amina.
ROZARI YA
FATIMA:Matendo ya furaha
Sehemu ya pili.
Liombee Kanisa.
Kwa ajili ya Kanisa Piganaji-Duniani.
Wimbo:
1.Yosefu,
tunakutolea sifa na heshima.
Wana wako
elekea, uwe wetumjima.
Kiitikio:Ewe
mlinzi mwminifu,
Tunaomba kwako.
Mlinde Baba Mtakatifu
Na Kanisa lako.
2.Yesu
amekuteua, kuwa mlishi wake.
Heri
gani umejua, kuitwa Baba yake.(K)
3.Ukamtunza
na Maria Mama wa Mwenyezi,
Kwako
tunakimbilia, Baba na mwombezi.(K)
4.Roho
tunapozimia, Yosefu, karibia
Saa ile
saidia, Kwako tufikie.(K)
1.Somo:Efe.1:22,4:7,16
K.Kanisa ni mwili wa Kristu na ukamilifu wake yeye
anayekamilisha vitu vyote kila mahali.Mwili huu hauna kiongo kimoja tu, bali
una viongo vingi. Sisi sote, tukiwa Wayahudi au watu wa mataifa mengine, watumwa
au watu huru, sote tuliobatizwa kwa Roho mmoja katika Mwili huo mmoja, na
kunyweshwa roho huyo mmoja ndio viungo
vyake.
Mungu amekipa
kila kiungo neema ya kushikamana na viungo nyenzake pamoja na Kristu ambaye ndiye kichwa. Pia
amekipa kila kiungo kazi ya kufanya.
Chini ya
uongozi wake viungo vyote hushikamana pamoja. Na kila kiungo kikitekeleza kazi
yake ipasavyo. Mwili wote, yaani Kanisa,
hukua na kujijenga katika upendo.
Neno la Mungu.
2.Sala
1.Kanisa ni
mji wa Mungu aliye hai,
nasi ni watu wake(aleluya)
Kiitikio. Bwana, naupenda uzuri
wa nyumba yako,(aleluya).
2.Basi, sisi
tulio watoto wa Mungu tumjue Mungu, tuwe watu waliokomaa katika Mwanae Kristu
Yesu, Bwana wetu(aleluya).
3.Nyumba ya
Mungu ni mahali patakatifu, humo Bwana atatumikiwa kwa kuwa ameijenga hiyo
nyumba(aleluya)
4.Asifiwe
Mungu! Ukombozi, utukufu na nguvu ni
mali yake Mungu wetu. Hukumu yake ni haki na ya kweli,(aleluya).
5.Bwana,
naupenda uzuri wa nyumba yako, Mahali ambapo utukufu wako unakaa(aleluya).
K. Bwana, sikiliza sala zangu
W. Na mlio wangu ukufikie.
K. Tuombe. Ee Bwana yesu, tunafahamu fika
Jinsi
Mtakatifu Athanas Askofu alivyokulinda
Wewe na
mafundisho ya kanisa lako Takatifu mpaka akatengwa na kanisa. Twakuomba
utujalie nasi kiasi kile kile alichokuwa
nacho yeye cha nguvu, ujasiri na utulivu wa kukusadiki wewe Mungu-Mtu na
kumpenda sana Mama Bikira Maria.
Wakati
wapinzani wake walipomtenga asifanye
kazi zake za kipadre na kumnyima kabisa masilahi yake yote, Mtakatifu Athanasi
alidumu hodari, imara na mkweli, aliendelea kupinga mafundisho batili na uongo
waliohubiri maadui zake, na waumini wakaendelea kumpenda.
Bwana Yesu,
twakusihi umfanye Mtakatifu Athanasi mmoja wa Watendakazi katika Safina, na kwa
masitaili yake twakuomba ulirejeshee Kanisa amani na imani, upendo, ujasiri, na
moto ule mkali aliokuwa nao yeye wa kuendelea kupepea bendera yako Bwana Yesu
na ile ya Mama yetu bila ya woga, kusitasita wala kujihurumia.
Salamu Maria
X3
Atukuzwe
Baba X1
.
ROZARI YA FATIMA:Matendo yaNuru.
Kwa ajili ya Kanisa la wateswa
Toharani na Limbo.
1.Wimbo:Languentibus au mwingine
1.Languentibus
in Purgatorio/Qui Purgantur ardore nimio
Et
torquentur gravi supplicio/Subveniat tua compassion:O Maria.
2.Fon es
patens qui culpas abluis/Omnes juvas et nullum respuis/
Manum tuam
extende mortuis//Qui sub poenis languent continuis O Maria.
3.Ad te pie
suspirant mortui/ Cupientes de poenis erui/
Et adesse
tuo conspectui/Aeternique gaudiis perfrui; O Maria
4.Gementibus
Mater accelera/Pietatis ostende viscera/
Illos, Jesus
per sua vulnera/Ut sanare dignetur impetra:O Maria.
5. Fac
Lacrimae quas bona respicis/Quas fundimus
Ad pedes
judicis/ Mox extinguant vim flammae vindicis/
Ut jungantur
choris angelicis: O Maria.
6.Et cum
fiet stricta discussion/ In tremendo Dei judicio/
Judicanti
supplica Filio/Ut cum Sanctis sit nobis portio:O Maria
2.Somo:(Ufunuo 20:11,12:Mt.25:34,41)
K.”Kisha nikaona kiti cha enzi kikubwa cheupe na yule
aketiye juu yake.
Kisha
nikaona watu wakubwa na wadogo wamesimama mbele ya kiti cha enzi, na vitabu
vikafunguliwa.
Halafu
nikaona kitabu kingine, yaani kitabu cha uhai, kikafunguliwa pia. Wafu
wakahukumiwa kadiri ya matendo yao, kama ilivyoandikwa ndani ya vitabu hivyo.
Kila moja kwa kadiri ya matendo yake.
Aliye
mtakatifu kabisa hulakiwa mbinguni, kushiriki uzima wa milele.”Njoo, wewe
uliyebarikiwa na Baba yangu, pokea ufalme uliotayarishiwa tangu kuumba
ulimwengu.”
Mlaanifu
hutupwa katika ziwa la moto wa milele. “Ondoka mbele yangu, ewe mlaaniwa! Nenda
katika moto wa milele uliyotayarishiwa Ibilis na malaika wake.”
Lakini Mungu
ana huruma bado na watakatifu majeruhi. Baadhi yao ni watu wazima waliokufa
wakiwa katika neema ya utakaso lakini roho zao hazijawa nyeupe kabisa. Hao
huenda toharani wakasafishwe kwa moto. Wengine
ni watoto waliokufa bila ya kubatizwa, wanayo bado dhambi ya asili. Hao
hupelekwa Limbo.
Kuhusu hao
watakatifu majeruhi Bwana Yesu anaagiza:”Waombeeni marehemu toharani ambao wako
hoehai, na watoto wachanga waliokufa bila ubatizo, ili Mungu mwenye huruma
awape msamaha.
Neno la Mungu.
W.Tumshukuru Mungu.
3.Sala:(Rejea Is.6:7,Zb.51:1,7: Malaki 3:3,4)
1.Mungu ni
mtakatifu kabisa, na mbingu imetanda utukufu wa Mungu, haipokei roho yoyote
isiyotakasika ikakamilika.
Kiitikio. Yesu, Mwana wa Daudi utuhurumie
2.Huzinyoshea
mkono wake roho za wampendao, ili kuyeyusha uchafu wao
wote na kuondoa takataka zao zote.(K)
3. Yeye
atakuja kuhukumu kama mtu asafishaye fedha. Atawasafisha wazawa wamfuatao kama
afuavyo dhahabu au fedha, mpaka wamekuwa dhabihu zinazokubalika.(K)
4.Utuhurumie,
ee Mungu kadiri ya fadhili zako. Ufutilie mbali makosa yangu kadiri ya wingi wa
huruma yako. Unioshe kabisa hatia yako,
unisafishe dhambi yangu, unisafishe kwa
isopo, nitakate, unioshe niwe mweupe kabisa.(K)
5.Tazama,
kaa hili limekugusa mdomo, umeondolewa
hatia yako, umesamehewa dhambi yako.(K)
6.Nimrudishie Bwana nini kwa haya yote aliyonitendea? Sina
la kukupa Mungu wangu, licha ya kusema,Bwana Mungu amenitendea makuu, Jina lake
litukuzwe.(K)
7. Ee Bwana
unisafishe kwa mrashi nami nitakuwa safi. Unioshe nami nitakuwa mweupe kuliko
theluji.(K)
K.Bwana, sikiliza sala yangu.
W.Na mlio wangu ukufikie.
Tuombe:Mungu Baba yetu, ambaye kwa kifo na
ufufuko wa Mwanao, sisi tumekombolewa,
ndiwe utukufu wa waumini wako na uzima wa watakatifu wote, uwarehemu wagonjwa
wetu wawe na afya njema, na wale unaowaita kwako uwapatie furaha ya milele. Kwa
njia ya Kristu Bwana wetu. Amina
4.Wimbo:Ushindi wa Moyo Immakulata wa
Maria.
Kiitikio:Ee Mungu Mwenyezi twakuomba uupe
ushindi Moyo Immakulatawa Maria wala mipango yake shetani mwovu na watu waovu
usifanikishe.
1.-Baba,
twawakabidhi sasa binadamu wote kwa Mama Maria, na kuomba:Moyo Immakulata wa
Maria utawale.Kiitikio
-Baba,
twalikabidhi tena taifa letu kwa Mama Maria na kuomba:Moyo Immmakulata wa Maria
utawale. Kiitikio
2.-Baba,
twaikabidhi tena dunia yote kwa Mama Maria na kuomba: Moyo Immakulata wa Maria
utawale.Kiitikio.
-Baba,
twalikabidhi tena Kanisa lote kwa Mama Maria na kuomba:Moyo Immakulata wa Maria
utawale.Kiitikio.
3.-Baba,
twaikabidhi tena hii Safina kwa Mama Maria na kuomba:Moyo Immakulata wa Maria
utawale.Kiitikio.
-Baba
twawakabidhi marehemu wetu wote kwa Mama Maria na kuomba:Moyo Immakulata wa
Maria utawale.Kiitikio.
ROZARI YA FATIMA:Matendo ya uchungu.
Sehemu ya
tatu
Iombeeni nchi
yenu
(Ibada ya kuiombea Tanzania na
Ibada kwa Mashaidi wa Uganda)
1.Wimbo wa Taifa.
i.Mungu
ibariki Afrika,
Wabariki
viongozi wake,
Hekima,
umoja na amani,
Hizi ni ngao
zetu, Afrika na watu wake
Ibariki Afrika, ibariki
Afrika.
Tubariki watoto wa Afrika
ii. Mungu
ibariki Tanzania,
Dumisha
uhuru na Umoja,
Wake kwa
waume na watoto,
Mungu
ibariki, Tanzania nawatu wake
Ibariki Tanzania, ibariki
Tanzania
Tubariki watoto wa Tanzania.
2.Salamu za Matawi
1.Kwa jina
la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Amina
2.Bwana asipoulinda mji.
Ee Baba wa
Mbinguni.*
Usitutupe
wanao wanyonge na wakosefu.
Ee Bwana wa
majeshi, twalikumbuka fika,*agizo lako la kwenye Zaburi.
“Bwana
asipoijenga nyumba.*waijengao wafanya kazi bure.
Bwana asipoulinda
mji.*
Yeye
aulindaye akesha bure.
Bwana
asipoulinda mji.*
Yeye
aulindaye akesha bure”
Wafalme wa
dunia wanajitayarisha/ nao wakuu wa watu jeuri wanashauriana pamoja kumwasi
Mungu na kuutokomeza mzabibu wako.
“Tuiondolee
Tanzania amani yake,*
Na uhuru
wake wa kuabudu.”
Lakini, ee
Bwana ndiwe nguvu na wokovu wetu/
Warudi nyuma
wenye kutuumiza.* na
Upigane nao
wale wanaotushambulia.
Atukuzwe
Baba na Mwana na Roho Mtakatifu*
Kama mwanzo
na sasa na siku zote, na milele Amina.
3.Bwana ndiye hakimu mwenye haki
Bwana ndiye
hakimu mwenye haki.*
Wala
hakijali cheo cha mtu.
Hatamkubali
yeyote juu ya maskini*
Naye
ataisikiliza sala yake aliyedhulumiwa.
Hatadharau kamwe malalamiko ya yatima,*
Wala ya
mjane amwelezezapo habari zake.
Malalamiko
yake aliyeonewa yatapata kukubaliwa,*
Na dua yake
itafika hima mbinguni.
Sala zake
mnyenyekevu hupenya mawingu.*
Wala
haitatulia hata itakapowasili.
Wala
haitaondoka hata aliye juu atakapoingilia/
Akaamua kwa
adili,*
Akatekeleza
hukumu.
Wala Bwana
hatalegea,*
Wala
hatakuwa mvumilivu kwa binadamu.
Atukuzwe
Baba na Mwana na Roho Mtakatifu*
Kama mwanzo,
na sasa, na hata milele. Amina.
4.Watu jeuri wakanyaga mzabibu wako
Kiitikio.Bwana Yesu linda mzabibu wako
Ee Bwana
Yesu Kristu, uliyewaambia Mitume wako”Nawaachieni amani, nawapeni amani yangu.”
Ona jinsi amani uliyotujalia Watanzania tangu mwanzo wa uhuru wetu ilivyo
hatarini hivi sasa(K)
Kwa miaka
yapata thelathini na mitatu hivi sasa, kipindi cha umri wako mwenyewe ulioishi
duniani, Ee Bwana umelitunza taifa letu ukishirikiana na Mama yako mpendwa,
mfano wa mzabibu ambao wewe mwenyewe umeupenda hapa Afrika, bara la ahadi.(K)
Wewe
mwenyewe umeupalilia huu mzabibu upate kukua, nao ukautoa miziz, ukaenea kote
nchini. Uliufunika kwa kivuli cha bushuti salama la Mama yako na Mama yetu,
Bikira Maria, na matawi yake yakawa kama mierezi mikubwa. Matawi yake yameenea
mpaka baharini, machipukiziyake mpaka mabara yote.(K)
Vipi leo
unyamaze na kulitia taifa lako katika mikono ya adui zetu ambao wamepanga
kutumeza? Wanaotaka kuua mzabibu wako na kuukanyaga kabisa waametega mitego
yao, wanatutakia maovu, wantishia kuua. Mchana kutw wanafanya mipango dhidi yao
kwa siri kabisa.(K)
Bwana Yesu,
wewe wajua jinsi gani shetani amepania kumwaga damu hapa Tanzania ili kuvuruga
amani, nao watu waovu na jeuri wanavyotamani kuona mzabibu huu wako unatupilia
mbali imani yake kwako na wewe Mungu, hazipotosha hatua zake na kunyakua uhuru
wake wa kuabudu Mwenyezi Mungu.(K)
Ee Bwana,
mikakati ya shetani ni mikubwa mno na hila za watu jeuri na mataifa waoteao
vita ni nyingi. Adui wengi wanauzunguka mzabibu wako kama fahali, wanausonga
kama fahali wakali, wanafunua vinywa vyao kama samba, tayari kuushambulia na
kuurarua.(K)
Wewe wayajua
hayo yote, na kwamba Watanzania ni watu wapenda amani. Tegemeo letu, mzabibu
wako, ni wewe Mfalme wa amani na Mama yetu mpendwa, Malkia wa amani.(K)
Basi,
twakusihi, msikae mbali nasi kwani taabu inakaribia. Muwe karibu, maana hakuna
wa kutusaidia. Mtuokoe na upanga wa watu jeuri, mtuepushe na mbwa wakali, mtuokoe
mbele ya nyati hawa.(K)
Kwa maombezi
yake Mama yako na mdhamini hodari wa Tanzania tangu uhuru wetu, Mama
Bikira Maria, na kwa maombezi ya ndungu
zetu Watakatifu Mashahidi wa Uganda ambao tutawaita hivi punde, ikupendeze ewe
Mwenyezi Mungu kuendelea kuulinda huu mzabibu wako, Tanzania na watu wake.(K)
La, siyo tu
Tanzania, bali ulimwengu mzima. Rejesha amani kila penye ugonvi na vita,
upendo penye chuki, imani thabiti kwa
Mungu Mwenyezi hata kwa zile roho sugu
zilizokukana Muumba wao. Stawisha uhuru wa kuabudu kila penye dhuluma na siasa
kali ya uonevu.(K)
Hali
kadhalika pisha mbali balaa zote za maisha, mikasa, ajal, gharika na mafuriko,
vimbunga na matetemeko ya inchi, volcano, ukame na njaa, maradhi ya fani zote,
udhaifu, dhiki na ulegevu kiafya, mavamizi ya shetani na madhara yake, vifo vya
gafla aidha na moto wa milele kwa kuepuka dhambi.(K)
Ee Mungu,
epusha vita vyote vya kimwili na kiroho pamoja na maafa yake. Mwisho uwajalie
roho wote walioko toharani na watoto
wachanga wanaokufa bila ubatizo raha ya milele.(K)
Tukiwa daima
chini ya ulinzi wake Malkia wa mbingu na dunia, tukutukuze wewe Mungu unayeishi na kutawala pamoja na
Baba na Roho Mtakatifu daima na milele. Amina.(K)
ROZARI YA FATIMA:Matendo ya Utukufu.
5.Wimbo:Ndungu zetu wa Uganda(Ud632T 339)
Kiitikio:Ndungu zetu wa Uganda mliomfia Yesu
toka mbingu mlipopanda! Tuombeeni.
1.Huko bara
la Uganda, Mungu katukuzwa,
Wale
wakristu wachanga, wakimshuhudia.
2.Mmoja wamwita Kizito, Na Mwingine Lwanga.
Wengi wao ni watoto, mara
wakafungwa.(K)
3.Waambiwa:”Kiacheni,
ni amriye Mtesa
Chama hicho
cha kigeni, sivyo, twawatesa”
4.Nao:”Mungu ni mkarimu, Na tajiri
sana,
Atoavyo vinadumu, Vyenu si vya
maana”.(K)
5Wakaaga wa
njiani,”Kwa herini, ndungu,
Siye twaenda
nyumbani, Kwa babate Mungu”
6.Wengi ndani ya Matita,
Wakateketezwa
Hata mmoja
hakusita, Akibembelezwa.(K)
7.Damu hizo
ni Sadaka, kwa Mwenyezi
Zitakuwa na
Baraka kwa Afrika yetu.
8.Kwa Mwenyezi ombeeni, Wapagani wote,
Nasi tusaidieni, Kuokoka sote.(K)
6.Litania ya Mashahidi wa Uganda.
Ndungu zetu
wa Uganda mliofia Yesu
Toka mbingu
mlipopanda ndungu tuombeeni X2
1.Wa kwanza
Karoli Lwanga, na mwingine Kizito,
Mathias
Mulumba, tunawakumbuka leo.
2.Wa nne Yusufu Mkasa, Ponsiano
Ngondwe,
Achiles Kiwanuka,
tunawakumbuka leo.(K)
3.Wa saba
Andrea Kagwa, nane ni Dionisi
Babake
Sebugwao, tunawakumbuka leo.
4.Athanasi Bazekuketa, na
Gonzaga Gonza
Pia Noe Mawagali,
tunawakumbuka leo.(K)
5.Na Luka
Banabakintu, Gyavila Musoke,
Na Bruno
Serunkuma, tunawakumbuka leo
6.Yakobo Buzabaliawo, na
Ambrosi Kibuka,
Anatoli Kirigwajo,
tunawakumbuka leo.(K)
7.Mukasa
Kiriwawamvu, Mugaga Lubowa,
Adolfu wa
Ludigo, tunawakumbuka leo.(K)
8.Na John Mary Muzeyi, na
Mbaga Tuzinde,
Ishirini na mbili,
tunawakumbuka leo.(K)
9.Wengine
Daudi na Okelo,
Ishirini na
nne, tunawakumbuka leo.(K)
7.Kuikabidhi kwa mara nyingine
Tanzania kwa Mama Bikira Maria
(Sala ya Papa Yohane Paulo II)
1.Maria
Mtakatifu, Mama wa Kanisa Mama wa binadamu wote pamoja na Baba Mtakatifu Yohana
Paulo wa Pili Halifa wa Mtume Petro. Sisi wanao wote wa Tanzania tunajiweka
chini ya ulinzi wako wa upendo.
Mama Maria, utuombee sasa
na saa ya kufa kwetu. Amina
2.Kwa moyo
moja, leo na daima tunajiweka upya mikononi mwako kama taifa change katika Bara
hili la ahadi. Kwa matumaini mapya na matarajio halali ya sasa na halafu
tunaomba msaada wenye nguvu wako wewe, Mama wa Mkombozi na Bwana wetu Yesu
Kristu.
Mama Maria utumbee sasa na saa kufa kwetu. Amina
3.Mama wa
Familia Takatifu ya Nazareti
Ndiwe Mama
wa “Kanisa la Nyumbani”.
Tunakuomba
msaada wako
Kwa ajili ya
familia zote nchini Tanzania.
Utufariji
katika mateso na usumbufu,
Utuimarishe
kwa neema zile zote
Zilizopamba
maisha ya familia yenu
Wewe Mama,
Mwanao Yesu na mumeo Yosefu,
Yaani kwa
neema na mwanga,faraja,utulivu na ujasiri.
Mama Maria,utuombee sasa na saa ya
kufa kwetu.Amina
4.Maria
Mtakatifu Mama wa Mungu,
Kwa moyo
wote tunakukabidhi pia
Kanisa zima
chini ya ulinzi wako,
Wewe Mama
mwajibika,kila Jimbo na kila Parokia ili
waumini wote wanapokutana pamoja na wachungaji wao, kwa nguvu ya Roho
Mtakatifu, kwa nguvu ya injili na adhimisho la Sadaka ya Ekaristi Takatifu
wadhihirishe kikamilifu uwepo wa Kanisa moja Takatifu, Katoliki, la Kitume,
lake Yesu Kristu.
Mama Maria utuombee sasa na saa ya kufa kwetu.
Amina
5.Kwa upendo
wa kimama uwasimamie na kuwasaidia Maaskofu, Mapadre na Watawa, waishi
kikamilifu miito yao waliyoipokea ndani ya moyo wa Kanisa, walitumikie Taifa la
Mungu na waushuhudie ukweli na maadili ya kiroho, ya ufalme wa Kristu.
Mama Maria utuombee sasa
na saa ya kufa kwetu.Amina.
6.Kwa namna
ya pekee, uwakumbuke watumishi wote waliopewa upadrisho mikononi mwake Halifa wa mtume Petro wakati ametembelea
Tanzania ili wawe watumishi waaminifu na watangazaji hodari wa injili.
Mama Maria utuombee sasa
na saa ya kufa kwetu. Amina.
7.Malkia wa
Amani, sikiliza sala za Taifa la Tanzania
tuombao amani ya kudumu na mshikamano thabiti katika nchi yetu na Afrika
nzima. Utufundishe moyo wa kusameheana
na moyo wa kupatana yatokeapo mafarakano katika familia zetu, aidha katika
masuala ya kijamii na kisiasa. Utujalie Watanzania wote kujua namna bora ya
kumpokea na kumstahi kila mtu na kuaminiana kidugu aidha moyo wa kufanya
kazi kwa bidii kwa Maendeleo ya ya inchi yetu huku tumezingatia kila siku
ujamaa ndiyo haki na umoja.
Mama Maria utuombee sasa na
saa ya kufa kwetu. Amina.
8.Maria Mama
yetu, upokee tendo la hili la kuiweka Tanzania chini ya ulinzi wako, na utujalie
kupata hayo tunayoomba kutoka kwa Moyo wa Mwanao, Bwana wetu Yesu Kristu.
Amina.
Mama Maria utuombee sasa na
saa ya kufa kwetu. Amina
ROZARI YA MATESO 7 YA MAMA BIKIRA
MARIA
BARAKA KUU:
1.O salutaris hostia.
O salutaris
hostia, quae coeli pandis ostium:
Bella
premunt hostilia, da robur, fer auxilium.
Unitrinoque
Domino, sit sempiterna Gloria,
Qir vitam
sine termino, nobis donet in patria.Amen
2.Tantum
ergo Sacramentum,veneremur cernui:
Et antiquum
documentum, novo cedat ritui:
Prestet
fides supplentum, sensuum defectui.
Genitori,
Genitoque, Laus et jubilation,
Slaus,honor,virtus
quoque, Sit et benection
Procedenti
ab utroque, Compar sit laudation. Amen
V.Panem de
coelo praestitisti eis.(Alleluia)
R.Omne
delectamentum in se habentem.(Alleluia)
Oremus, Deus
qui nobis sub Sacramento mirabilis
Passionis
tuae memoriam, reliquisti, tuibue Question
Ita nos
corporis et sanguinis tui scra mysteria
Venerari; ut
redmptionis tuae fructum
In nobis
jugiter sentiamus,
Qui vivis et
regnas, in saecula seculorum. Amen.
3.Adoremus
Adoremus in
aeternum
Sanctissimum
sacramentum.
Psalm 116
Ladate
Dominum, omnes gentes
Laudate eum,
omnes populi.
Quoniam
confirmata est super nos
Misericordia
ejus
Et veritas
Domini manet in aeternum
Gloria
Patri, et Filio, et Spiritui sancto
Sicut erat
in principio, et nunc et simper,
Et in
saeculorum. Amen
7.Wimbo wa kusindikiza
Sakrament(Ufuatao au mwingine)
Tawala Bwana Yesu Kristu
Tawala Bwana Yesu Kristu
Tawala Bwana, tawala Bwana.
Tawala Mwana wa Maria
Tawala Bwana, tawala Bwana.
Mungu Baba kakupa vyote
Tawala Bwana, tawala Bwana.
1.Twaja
kukusifu, mshindi wa mauti,
Tawala
Bwana. Tawala Bwana.
2.Kwa mateso
yako, sote tumepona,
Tawala
Bwana. Tawala Bwana.
3.Tunakushukuru-kwa
kutukomboa,
Tawala
Bwana. Tawala Bwana.
4.Twakukaribisha-
Mfalme wa amani,
Tawala
Bwana. Tawala Bwana.
5.Shetani na
dhambi-wote wamekimbia.
Tawala
Bwana. Tawala Bwana.
6.Sala ya kuombea Familia.(Sir
10:9:21:5)
Ee Mwenyezi
Mungu, usitutupe wanao wanyonge na wakosefu. Je,mtu aliye vumbi na majivu atajivunia
nini? Dua ya maskini husikika kwa Mungu, na uamuzi wake Mungu huwasili haraka.
Baba Mungu,
ndoa zako hufungwa mbinguni mbele ya jeshi zima la Malaika na Watakatifu wako,
na altareni mbele ya mashahidi binadamu. Nawe umeagiza”Alichounganisha Mungu, binadamu
asitenganishe”.
Mwenyezi
Mungu twakusihi, ubariki familia zote za zamani na change hata zile zilizo katika hatari ya kuvunjika, Uzijalie upendo, umoja, amani na
riziki za kutosha, zipate kudumu.
Uwabariki na
watoto wote, uwadumishe usafi wa moyo na usalama. Wanaosoma Bwana Yesu uwasindikize
daima na kuwafanikisha ,na siku zote wabaki katika familia zao. Amina
7.Sala ya kuombea Taifa.
Baba wa
milele, ubariki ombi letu. Kwa amri yako kila unachopenda hufanyika, wala
hakuna awezaye kupunguza uwezo wako wa kuokoa. Baba Mwenyezi, kwa maombezi ya
Mama Bikira Maria na Mashahidi wa Uganda,siku zote utujalie na uwalinde,
viongozi wa chaguo lako. Uliepushe taifa letu na utumwa mpya wa jinsi zote,
hasa na maisha ya kuombaomba yenye moto unaochoma. Baba, badilisha mioyo ya
viongozi wote wasiokujali, kama ulivyomgeuza Mtakatifu Paulo, hivyo Baraka zako
zijaze nchi yetu kama mto. Amina
No comments:
Post a Comment