KWELI TUNASHIRIKI
KUMTESA YESU?
Ebu tujiulize kuhusu upendo wa namna ya kupendeza jinsi
Bwana Yesu anateseka kwa ajili yangu na wewe pia.
Tujiulize ni mara ngapi tunaendelea kuyafanya pengine ni
kufuru na kumdharirisha ndani ya kanisa na nje ya kanisa kwa kumunyo za
kumdhihaki ukosefu wa heshima kwenye nyumba ya Mungu tukijidanganya kuwa
twaenda na wakati ambayo hayatofautiani na ya Wayahudi waliomtesa.
Awali ya yote kwanza tufanye tafakari fupi katika siku za
kuelekea ushindi wa Yesu.
i)JUMAPILI YA MATAWI.
Tunashangilia mkombozi kuingia Yerusalemu kama walivyofanya
Wayaudi. Kama tushirikiavyo katika kupeperusha matawi tukiimba Hosana Mwana wa Daudi. Lakini wakati tunafanya hivyo
tujiulize tunafahamu maana ya kutumia rangi nyekundu? Tusaidiane kwa hilo ili
kuyaelewa makuu hayo.
ii)ALAMISI KUU.
Tujiulize juu ya mapendo ya kumpendeza kukubali kutoa mwili
na damu yake katika mafumbo ya mkate na divai ili lengo lake aishi nasi
milele daima.
Tujiulize hivi kweli tunayaheshimu matendo hayo hasa ya
mkate na divai au hatujui nap engine inawezekana tunashiriki kumzihaki kwa
namna tunavyompokea? Tukijifariji tunaendana na mabadiliko ya ulimwengu? Mfano
kuogopa kuchafua mavazi yetu tukipiga magoti? Je tunaungana na Yule mwovu
aliyetaka Yesu ampigie magoti? Au hatutaki
kuonesha ishara ya unyenyekevu kwake tukijidanganya ishara ya nje sio lazima?
Ushauri.
Tuulinde utukufu wake, hasa wakati wa kumpokea tusije
tukajikuta tunajiandalia adhabu kali.Pia ni vyema tumpokee ulimini zaidi hii
itutusaidia kumlinda mwokozi kudondoshwa chini hali inayopelekea kumkanyaga
hiyo ni ishara ya kumdhihaki kama Wayahudi walivyofanya baadhi yao.
Je? Tujiulize ni mara ngapi tunampokea katika hali hiyo.
Basi hii ni tafakari yangu je we wasemaje au waonaje njia sahihi?
iii)IJUMAA KUU.
Je? Tunajifunza nini hivi leo? Wakati dunia inaangaika kwa
mateso mengi watoto wasiokuwa na hatia wanatolewa mimba, ukatili wa kijinsia,
unyanyasaji kwa wanyonge na mengineyo. Hivi tunashiriki vyema katika
kuyaepusha?
Hivi tena tujiulize tunapokatazwa kula nyama tunajifunza
nini kuhusu tendo hilo? Basi tumwombe Bwana Yesu atufundishe maana yake ili
tunapoikumbuka siku hiyo kuhusu kifo tupate Baraka zake kwa kwa kuyatafakari
matendo hayo kwa usahihi.
iv)JUMAPILI YA
PASAKA.
Ni shangwe kuu tunaposherekea ushindi wa Bwana Yesu na
ukombozi wa mwanadamu.Je? tujiulize hivi tunafufuka naye kweli au tunajiona
tunafufuka kimwili lakini tumekufa bado kiroho. Mtoto,kijana, mzee na kikongwe
yatupasa kukaa chini na kuyatafakari makuu haya.
SALAMU ZA PASAKA.
Yesu alipoingia Yerusalemu Wayahudi walitandika nguo zao
chini ili Yesu apite. Haohao walipaza sauti zao wakisema asulubiwe, acha
kuchanganyikiwa tambua kuwa mwanadamu anabadilika, alisema anakupenda ipo siku
atasema anakuchukia, aliyesema mtatenganishwa na kifo ipo siku atakupa talaka,
aliyesema wewe ni mwema ipo siku atasema una roho mbaya, na Yule unampenda
sana atageuka kuwa adui mkubwa.
Je, Tusiwe na marafiki? Yesu alisema uwe mjanja kama nyoka
na mpole kama ua, ishi kwa akili ukimkumbatia Yesu katika maisha ya kila siku naye
atakufunulia yote upate mwanga wake. Sherekea Pasaka njema.
No comments:
Post a Comment