Tumshukuru Mt.John Bosco kwa maisha aliyayaishi kwa upendo. Hakika Mungu alimteua kuwa mtu wa watu katika kudhihirisha maisha ya upendo. Upendo huu hatuna budi kujifunza matendo haya kuyaishi hata kama yanatokea kuwa na changamoto baina ya pande zote mbili. Lakini Mt.John Bosco aliweza kuzikabili changamoto.
Basi usichoke kumpenda mtu yeyote hata kama unakabiliwa na changamoto kaa chini tafakari nini maana ya upendo na jiulize kwa gani Mungu amekupenda hata unapokengeuka lakini hakuachi kwa kuwa umeumbwa kwa sura ya mfano wake. Hivyo basi tudumishe upendo kama Mt.John Bosco alivyoudumisha, mshirikishe Mungu katika upendo wako hasa wenye kumpendezesha Mungu kwa kupitia maombezi ya Mt.John Bosco naye atakusaidia.
No comments:
Post a Comment