Friday, October 6, 2017

Maisha ya Mtakatifu Bruno Mkartusi(Padri)


Mtakatifu Bruno Mkartusi  alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mmonaki aliyeanzisha ambaye aliweza kuanzisha shirika la kitawa  kwa wakaapweke  ambalo linadumu mpaka leo .Mtakatifu Bruno anaheshimiwa kama Mtakatifu.Mtakatifu Bruno alizaliwa mwaka 1030.Mnamo Juni 1101 Roger alifariki dunia, akiwa na Bruno karibu naye. Tarehe 6 Oktoba Bruno pia akafariki, akizungukwa na wafuasi wake.
Sikukuu yake inaazimishwa kila tarehe 6 Oktoba.
Mtakatifu Bruno utuombee

Akiwa kijana alikwenda Reims nchini Ufaransa, ambapo mwaka 1057 Askofu  Gervas alimkabidhi uongozi wa shule iliyomlea. Mnamo mwaka 1076 aliacha shughuli zake shuleni na jimboni akiwa kama katibu mkuu akamkimbilia mtawala mdogo Ebal wa Roucy, kutokana na askofu Mnase wa Gournay  kumchukia kwa sababu ya kumlaumu kwa kosa la usimoni . Aliamua kurudi Ufaransa mwaka 1080, baada ya Manase kuondolewa na mtaguso  maalumu.

Katika miaka hiyo migumu, ndipo wito wake wa kimonaki ulipojitokeza. Katika barua yake aliyoandika Mtakatifu Bruno alisimulia jinsi alivyoweka nadhiri ya kujitoa wakfu kwa Mungu pamoja na marafiki wawili.
Baada ya kurudi Ufaransa, alikwenda kwenye makao ya upwekeni  ya Molesme, chini ya uongozi wa Robert wa Molesme ,mwanzilishi wa urekebisho wa Citeaux  wa shirika la Mtakatifu Benedikto. Halafu akiwa na wenzake sita yaani mapadri 4 na mabruda 2,ambapo  alitafuta mahali pa faragha kabisa ili kuanzisha monasteri, akapewa na askofu wa Grenob,Ugo wa Grenoble, ambaye alisukumwa na njozi. Eneo hilo la kufaa lilikuwa bonde katika milima iliyoitwa «Cartusia»

Monasteri ilianza kujengwa katikati ya mwaka 1084, kwenye mita 1175 juu ya usawa wa bahari.Inasemekana Kanisa  tu lilijengwa kwa mawe, ili liweze kuwekwa wakfu, kama ilivyofanyika mwaka 1085.
Miaka sita baadaye Papa Urban II , aliyekuwa mwanafunzi wake huko Reims, alimuita Roma, atumikie Ukulu mtakatifu. Mtakatifu Bruno hakuweza kukataa, hivyo aliacha upweke kwa wenzake.

Mtakatifu Bruno alipotii wito wa Papa, alihisi kuwa jumuia yake kwa kukosa uongozi wake itaingia jaribuni; na kweli ilisambaratika. Lakini alifaulu kuwarudisha Kartusi waendelee chini ya Landuino.
Pamoja na hayo, Bruno hakuweza kuzoea mazingira na majukumu ya Roma, akitamani kurudi upwekeni.
Urbano II alipokimbia Roma, kutokana na kaisari Henri IV kuvamia Dola la Papa  na kumteua antipapa Klementi III, Mtakatifu Bruno alimfuata Papa Italia Kusini.
Kwa pendekezo la Papa, alichaguliwa askofu mkuu wa Reggio Calabria, lakini alikataa.
Hatimaye alikubaliwa kwenda upwekeni Italia kusini.

Mwaka 1090  mtawala Roger I wa Sicilia alimtolea eneo kwenye mita 790 juu ya usawa wa bahari, mahali palipoitwa Torre, leo Serra San Bruno , katika mkoa wa Calabria .
Huko  Mtakatifu Bruno alianzisha makao ya upwekeni ya Mtakatifu Maria, na karibu kilometa 2 bondeni - ambapo leo ipo Certosa di Serra San Bruno  - alianzisha kwa ajili ya mabruda monasteri ya Mtakatifu Stefano.
Halafu, mwaka 1094 hivi, Roger alipompatia msaada wa familia ya Mulè, Bruno aliipangia mahali pa mbali kidogo, ambapo sasa ipo  Serra San Bruno.
Bruno, akirudia maisha aliyoyacha Ufaransa, alimalizia maisha yake kwa miaka 10 upwekeni. Wakati huo alitembelewa na Landuino, mwandamizi wake huko Kartusi.

No comments:

Post a Comment