Friday, October 6, 2017

Maisha ya Mtakatifu Josemaria Escriva

Image result for image of Saint Josemaria Escriva

Mtakatifu Josemaria Escriva alizaliwa mjini Barbastro, Uhispania, mnamo tarehe 9 Januari, 1902. Alipata sakramenti ya upadri tarehe 28 Machi, 1925 mjini Saragosa. Kwa mwongozo wa Mungu, tarehe 2 Oktoba 1928, aliianzisha Opus Dei. Tarehe 26 Juni 1975, alikufa ghafla mjini Roma chumbani mle alimozoea kufanyia kazi yake, baada ya kuitupia jicho la upendo picha ya mama yetu, Maria. Kufikia hapo, Opus Dei ilikuwa imekwisha kusambaa katika mabara yote matano ya ulimwengu, ikiwa na wanachama zaidi ya 60,000 kutoka mataifa 80, wanaolitumikia kanisa kwa moyo mmoja, wakijiuga kikamilifu na Baba Mtakatifu pamoja na Maaskofu, kama ilivyokuwa desturi yake Mtakatifu Josemaria. Baba Mtakatifu John Paul II alimfanya mwanzilishi wa Opus Dei kuwa Mtakatifu tarehe 6 Oktoba 2002 mjini Roma. Sikukuu yake inasherehekewa tarehe 26 Juni. Mwili wa Mtakatifu Josemaria umelazwa katika kanisa kuu la Prelature ya Opus Dei liitwalo ‘Mama Yetu wa Amani’, katika barabara ya Bruno Buozzi 75, mjini Roma.

Sala:Ee Mungu, kwa maombezi ya Bikira Maria, ulimjalia padri wako Mtakatifu Josemaria neema nyingi, ukamchagua kuwa mtume wako mwaminifu ili aanzishe Opus Dei, njia ya kujitakasa katika kazi ya kila siku na katika kutimiza wajibu wa kawaida wa Mkristu. Nisaidie mimi pia ili nami niweze kuyafanya mambo yote ya maisha yangu yawe nafasi ya kukupenda na kulitumikia Kanisa, Baba Mtakatifu na watu wote, kwa furaha na moyo mwepesi, nikiangaza njia zote duniani kwa mwanga wa imani na upendo. Kwa maombezi yake Mtakatifu Josemaria, nijalie msaada ninaokuomba… (taja ombi lako hapa). Amina. Baba yetu, Salamu Maria, Atukuzwe Baba.




No comments:

Post a Comment