Imebeba sala na muongozo juu ya Ukatoliki katika kuutafuta utakatifu ila na mwanadamu yoyote apendezwaye na sala hizi naomba aungane kwenye jumuiya hii maana sote ni baba mmoja katika itikadi tofauti Amina
Saturday, September 30, 2017
Wednesday, September 27, 2017
Mtakatifu Sharbel Maklhouf
Sala
Ee Bwana uliye Mtakatifu usiye na mwisho na unayetukuzwa katika watakatifu wako,uliyemwongoza Mtawa Mtakatifu na Mweremita Sharbel kuishi na kufa katika njia ya Yesu Kristu,ukampa nguvu ya kujiepusha na mambo ya dunia ili kumfanya katika ueremita wake ashinde na kupata fadhila za kimonaki za Ufukara,Utii na Usafi Tunakuomba utujalie neema ya kukupenda na kukutumikia kwa kufuata mfano wake
Mungu Mwenyezi uliyedhihirisha nguvu ya maombezi ya mtakatifu Sharbel Maklhouf kwa miujiza na fadhili zisizo na idadi,utujalie neema hii(......) kwa maombezi yake Amina
Maisha yake
Mtakatifu Charbel Makhlouf, alizaliwa tarehe 8 Mei 1828 na kufariki tarehe 24 Desemba 1898,awali aliitwa kwanza Youssef Antoun Makhlouf alipozaliwa huko Bekaa Kafra katika nchi ya Lebanon kaskazini mpaka kufikia hatua ya kuwa mmonaki wa Kanisa la Wamaroni, halafu pia kama padri.
Alitangazwa na Papa Paulo VI kuwa mwenye heri tarehe 5 Desemba 1965 , na baadae mtakatifu tarehe 9 Oktoba 1977.
Bonyeza hapa upate zaidi:
Novena a san Charbel Makhlouf - Programu za Android kwenye ...
Maisha ya Mtakatifu Gertrudi wa Thuringia
Mtakatifu Gertrudi alizaliwa katika mji wa Eisleben , kwenye mkoa wa Thuringia, kwenye nchi ya Ujerumani mnamo Tarehe 6 Januari 1256 na alifariki tarehe 17 Novemba 1302.
Mtakatifu Gertruda katika utoto wake alilelewa na watawa wa kike ambao ni Wabenedikto wa urekebisho wa Citeaux huko Helfta , ambako alifaulu vizuri katika masomo yake, hasa falsafa,historia na fasihi.
Mtakatifu Gertruda akijulikana kama Getrudi mkuu alijiweka kabisa mikononi mwa Mungu, akasonga mbele haraka sana katika utakatifu, akitumia muda wake katika kusali na kufanya tafakari.Mtakatifu Getruda alikuwa mmonaki katika maisha yake.Mtakatifu Getruda anatambuliwa na Kanisa Katoliki kuwa mtakatifu kama bikira ambapo hukumbukwa kila mwaka tarehe 16 Novemba.
Sala ya Mtakatifu Gertrudi wa Thuringia
Mungu, unayestahili upendo usio na mipaka, sina chochote cha kupimia vema ukuu wako, lakini hamu yangu kwako ni hivi kwamba, kama ningekuwa na yale yote uliyonayo wewe, ningekupa yote kwa furaha na shukrani.
Kwa ajili ya uongofu nakutolea, Baba mpenzi sana, mateso yote ya Mwanao mpendwa sana tangu wakati ule ambapo, akilazwa horini juu ya nyasi, alianza kulia, halafu akavumilia mahitaji ya utoto, mapungufu ya ubalehe, mateso ya ujana, hadi alipoinamisha kichwa akafa msalabani kwa mlio mkubwa.
Vilevile, kwa kufidia makosa yangu ya uzembe, nakutolea, Baba mpenzi sana, mwendo wote wa maisha matakatifu sana ambayo Mwanao pekee aliyaishi kikamilifu kabisa katika mawazo, maneno na matendo yake tangu atumwe kutoka ukuu wa kiti chako cha enzi kuja katika dunia yetu, hadi alipouonyesha mtazamo wako wa Kibaba utukufu wa mwili wake mshindi.
Kama shukrani nazama katika kilindi kirefu sana cha unyenyekevu, na pamoja na huruma yako isiyolipika, nasifu na kuabudu wema wako mtamu sana.
Wewe, Baba wa huruma, nilipokuwa ninapoteza maisha yangu hivyo, ulikuza kwangu mawazo ya amani, si ya mabaya, ukaamua kuniinua kwa wingi na ukuu wa fadhili zako.
Kati ya mengine, ulitaka kunijalia ujirani usiothaminika wa urafiki wako kwa kunifungulia kwa namna mbalimbali hazina ile azizi sana ya umungu, ambayo ni moyo wako wa Kimungu, na kwa kunitolea kwa wingi mkubwa kila utajiri wa furaha ndani yake.
for more
Saint Gertrude the Great - Mary Pages
Tuesday, September 19, 2017
Sala Kwa Mtoto Yesu Wa Prague
Ee Mtoto Yesu mwenye huruma, ninajua Miujiza yako kwa wagonjwa....... nionapo neema zako na uponyaji unaojalia watu.... kwa njia ya kuuheshimu Utoto wako Mtakatifu, na hasa picha yako ya Prague. Ninasema kwa uhakika mkuu: Ee Mtoto Yesu mpendevu sana, unaweza ukaniponya. Nyoosha mkono wako Mtakatifu na kwa Nguvu Yako uniondolee maumivu yote na Udhaifu.
Amina.
Maisha ya Mtakatifu Veronica Giuliani
Mtakatifu Veronica Giuliani alizaliwa mnamo tarehe 27 Desemba 1660,Umbraria huko Italia na alifariki mnamo tarehe 9 Julai 1727.Mtakatifu Veronika Giuliani alikuwa Mmonaki wa urekebisho wa Wakapuchini wa utawa wa Shirika la Mt.Klara.
Mtakatifu Veronica Giuliani anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu bikira .Maandiko yanatuambia Mtakatifu Veronica Giuliani aliheshimiwa mara baada ya kufa, na kesi ya kumtangaza rasmi ilicheleweshwa na uchunguzi wa maandishi yake marefu.
Mtakatifu Veronica Giuliani alitangazwa kuwa mwenye heri mnamo Juni 1804 na Papa Pius VII na baadae alitangazwa kuwa mtakatifu tarehe 26 Mei 1839 na Papa Gregori XVI.
Maandishi ya Mtakatifu Veronica Giuliani yanasimulia alivyoanza kujaliwa karama za pekee akiwa na umri wa miaka 3 tu, alipokuwa anaitwa Orsola.
Pia alijiunga na Waklara Wakapuchini wa monasteri ya Città di Castello mwaka 1667 ambapo alikuja kuwa abesi tangu mwaka 1716 hadi kifo chake.
Kwa namna ya pekee Mtakatifu Veronica Giuliani aliambatana na Yesu msulubiwa kadiri ya karama ya Fransisko wa Asizi.Na kadiri ya maandishi Kanisa Katoliki linakubali ukweli wa madonda matakatifu aliyosema alikuwanayo tangu tarehe 5 April 1697 hadi kifo chake.
Katika agizo la padri aliyemuongoza kiroho, na aliandika kirefu takribani kurasa 22,000 kwa mikono bila ya sahihisho lolote ambazo ni kumbukumbu za maisha yake yote, ambazo zilitolewa baada ya kifo chake kwa jina Il Tesoro Nascosto (ni magombo 36).
Kwa mujibu wa shajara hiyo, Veronika Giuliani anahesabiwa kati ya Wakristo wanasala waliojaliwa mang'amuzi ya juu zaidi.

St. Veronica Giuliani - Saints & Angels - Catholic Online
CATHOLIC ENCYCLOPEDIA: St. Veronica Giuliani - New Advent
Maisha ya Mtakatifu Brigita(Life of Saint Brigita)
Mtakatifu Brigita(Wengine wanaliandika Mtakatifu Brigida) alizaliwa nchi ya Ireland kwenye mji wa Kildare kwa misingi hiyo pengine anaandikwa kama Mtakatifu Brigita wa Ireland na wengine wanamtaja kama Mtakatifu Brid wa Kildare.
Mtakatifu Brigita alizaliwa nchini Ireland mnamo mwaka 451 na alifariki mwaka 525 japo vyanzo vingine vinaonesha kuwa alizaliwa mwaka 453 na kufariki mwaka 524.Ukisoma baadhi ya vyanzo vingine inaonesha palikuwepo mjadala ambao ulikuwa ukizungumziwa kuhusu wazazi wake ila kwa ukubwa inasemekana mama yake alikuwa anaitwa Brocca ambaye alikuwa mtumwa kwa mantiki hiyo Mtakatifu Brigita alizaliwa ndani ya Utumwa.
Mtakatifu Brigita aliweza kupata ubatizo wake ambao alibatizwa na Mtakatifu Patriki na Baba yake alikuwa anaitwa Dubthach.Mtakatifu Brigita ni mjawapo wa msimamizi wa nchi ya Ireland pamoja na Mtakatifu Patricki na Mtakatifu Kolumba.
Mtakatifu Brigita wa Ireland kadri ya maandiko inasemekana alikuwa mmonaki abesi mwanzili wa monasteri mbalimbali za kike, ikiwemo ile maarufu ya Kildare nchini Ireland.Mtakatifu huyu inasemekana alitoa mchango mkubwa katika uinjilishaji kwenye hicho kisiwa mpaka leo unamchango mkubwa kiimani. Na hivyo anahesabika Anahesabiwa na madhehebu mbalimbali ya Kikristo ambayo ni Wakatoliki,Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu.
Sikukuu yake huazimishwa kila mwaka Februari mosi(1 February) pamoja na ya Mtakatifu Dar Lugdach ambaye alikuwa mwanafunzi wake aliyekuwa amerithi mamlaka yake.
kwa kusoma zaidi bonyeza hapa:
St. Brigid of Ireland - Saints & Angels - Catholic Online
Friday, September 15, 2017
Mama Bikira Maria wa Mateso
Leo tarehe 15 Septemba ni siku inayokumbukwa kila mwaka katika kukumbuka mateso ya Mama Bikira Maria. Wakati tukikumbuka Mama Bikira Maria wa Mateso hatuna budi kuzidi kushikamana naye katika mateso yetu katika maisha yetu mbalimbali.
Bikira Maria wa Mateso ni jina mojawapo linalotumika kumheshimu Mama wa Yesu kama mshiriki wa mateso na kifo cha Mwanae msalabani .
Liturujia ya Kanisa la Kilatini inaadhimisha kumbukumbu yake tarehe 15 Septemba, siku inayofuata sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba.
Ndivyo ilivyopangwa na Papa Pius X kwa Dunia nzima mwaka 1913, baada ya heshima hiyo kuenea sana katika ya Wakatoliki kuanzia karne ya 11.
Msingi wake ni hasa habari za Injili ya Luka (2:34-35,41-51; 23:27-31,55-56) na ya Yohane (19:25-27), lakini pia ile ya Mathayo (2:13) kuhusu mtoto Yesu alipokimbizwa ili asidhuhulike na mpango wa Mfalme Herode Mkuu .
Katika liturujia ya Neno,Misa ya siku hiyo ina sekwensya ya pekee, ambayo kwa Kilatini inayojulikana "Stabat Mater" ("Mama alisimama"), ambayo ndiyo maneno ya kwanza ya shairi hilo lenye muziki wa huzuni lakini mtamu.
Kama wanadamu tunayo mateso mbalimbali ambayo tunakuwa tunakumbana naye kupitia mfano wa mama yetu Bikira Maria na Mama wa Mkombozi wetu yatupasa kujifunza na kuendelea kumheshimu kwa kuwa alitesekana sana katika safari nzima ya Mwanae Yesu kwa lengo la kushiriki katika kumkomboa mwanadamu.
Rozari ya Mateso Saba ya Bikira Maria
Teso la Kwanza
Mzee Simeoni aliagua kuwa Moyo wa Mama Maria utachomwa kwa upanga.Tuombe neema ya kuvumilia mateso.
Mama wa mateso utuombee.
Baba Yetu ……… Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba ……
Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.
Teso la Pili
Maria na Yosefu walikimbilia Misri usiku ili kumficha Mtoto Yesu asiuawe na Herodi.Tuombe neema ili miili yetu iwe kimbilio lake Yesu.
Mama wa mateso utuombee.
Baba Yetu ……… Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba ……
Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.
Teso la Tatu
Mama Maria aliona uchungu sana Mtoto Yesu alipopotea kwa siku tatu.Tuombe neema ya kudumu na Yesu mioyoni mwetu.
Mama wa mateso utuombee.
Baba Yetu ……… Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba ……
Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.
Teso la Nne
Mama Maria aliona uchungu sana alipokutana na Mwanae Yesu katika njia ya Msalaba.Tuombe neema ya kudumu na Yesu siku zote.
Mama wa mateso utuombee.
Baba Yetu ……… Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba ……
Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.
Teso la Tano
Mama Maria aliona uchungu sana alipomwona Mwanae Yesu akisulibiwa Msalabani.Tuombe neema ya kufa mikononi mwa Yesu na Maria.
Mama wa mateso utuombee.
Baba Yetu ……… Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba ……
Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.
Teso la Sita
Mama Maria aliona uchungu sana alipopakata maiti ya Mwanae Yesu baada ya kushushwa Msalabani.Tuombe neema ya kutotenda dhambi.
Mama wa mateso utuombee.
Baba Yetu ……… Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba ……
Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.
Teso la Saba
Mama Maria aliona uchungu sana aliporudi nyumbani baada ya kumzika Mwanae YesuTuombe neema ya kitulizo kwa Mama Maria.
Mama wa mateso utuombee.
Baba Yetu ……… Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba ……
Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.
Litania ya Mateso Saba ya Mama Bikira.
Bwana utuhurumie Bwana utuhurumie
Kristo utuhurumie Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie Bwana utuhurumie
Kristo utusikie – Kristo utusikilize
Mungu Baba wa Mbinguni, Utuhurumie
Mungu Mwana, Mkombozi wa dunia Utuhurumie
Mungu Roho Mtakatifu Utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu MMoja Utuhurumie
Maria Mtakatifu Utuombee (iwe kiitikio)
Mama wa Mkombozi wetu,
Mama mwenye mateso,
Malkia wa mashahidi,
Mama wa wenye uchungu,
Mfariji wa wenye taabu,
Msaada wa wenye shida,
Mlinzi wa wenye upweke,
Nguvu ya dhaifu moyoni,
Makimbilio ya wakosefu,
Afya ya wagonjwa,
Matumaini ya wanaozimia,
Kwa ajili ya ufukara wako ulioona pangoni Bethlehemu, - Utusaidie ee Mama wa mateso (iwe kiitikio)
Kwa ajili ya mateso yako uliyoona katika uaguzi wa Simeoni,
Kwa ajili ya taabu zako ulizopata katika safari ya Misri,
Kwa uchungu wako, Mwanao alipopotea,
Kwa ajili ya huzuni yako Mwanao alipodhulumiwa,
Kwa ajili ya hofu yako Yesu alipokamatwa,
Kwa ajili ya uchungu wako ulipokutana na Yesu katika njia ya Msalaba,
Kwa ajili ya mateso ya Moyo wako aliposulibiwa,
Kwa ajili ya mateso yako makali Yesu alipokufa,
Kwa ajili ya kilio chako juu ya Mwanao mpenzi,
Kwa ajili ya uchungu wako penye kaburi la Mwanao,
Kwa ajili ya upweke wako baada ya maziko ya Mwanao,
Kwa ajili ya uvumilivu wako katika shida zote,
Katika uchungu wetu wote,
Katika ugonjwa na mateso,
Katika huzuni na shida,
Katika umaskini na upweke,
Katika mahangaiko na hatari,
Katika vishawisho vyote,
Katika saa ya kifo chetu,
Katika hukumu ya mwisho,
Mwanakondoo wa Mungu, unayeondoa dhambi za dunia, Utusamehe ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu, unayeondoa dhambi za dunia, Utusikilize ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu, unayeondoa dhambi za dunia, Utuhurumie.
Kristo utusikie – Kristo utusikilize
Bwana utuhurumie – Kristo utuhurumie
Bwana utuhurumie.
Baba Yetu ….
Utuombee, ee Mama wa Mateso
Tujaliwe kupewa ahadi za Kristo.
TUOMBE: Ee Bwana Yesu Kristo, utusaidie sasa na saa ya kifo chetu msaada wa Bikira Maria Mama yako, ambaye moyo wake mtakatifu ulichomwa na upanga wa mateso ulipoteswa na kufa msalabani. Unayeishi na kutawala milele na milele. Amina.
Sala kwa Mama Bikira Maria Katika Ukiwa wake
Nakusikitikia sana Mama Mtakatifu Maria kwa sababu ya ukiwa wako mkuu. Uchungu wako ulikuwa mkubwa sana ulipotazama mateso na kifo cha Mwana wako mpenzi. Muda ule uliweza kutuliz kidogo kwa sababu ya kumwona angali hai. Lakini je, baada ya kufa na kumzika? Sasa wewe ni mkiwa mkubwa mno! Uh, ukiwa wa pekee, uniombee mimi ninayempoteza mara nyingi kwa dhambi zangu. Unijalie nisimpoteze tena Yesu wangu kwa ubaya wa uvivu wangu, bali nimtumikie kiaminifu duniani hapa ili nimwone na kumfurahia milele mbinguni. Amina.
Sala ya Majitoleo Kwa Mama Wa Huzuni
Mama Mtakatifu, Mama wa Mungu na Malkia wa Mashahidi, leo nakuchagua Wewe uwe mfano wangu, mkingaji na mteteaji wangu. Naweka roho fukara katika moyo wako uliotobolewa na panga nyingi za mateso. Unipokee mimi niwe mtumishi wako wa pekee na mshiriki wa mateso yako. Nijalie nguvu niwe daima karibu na msalaba ule alikosulibiwa Yesu. Nakutolea nafsi yangu na mali yangu yote. Pokea kila tendo langu jema ukalisindikize kwa Mwanao, Mama, nifanye nistahili kuitwa mtumishi wa Maria, Simama karibu yangu katika matendo yangu yote ili yafanwe kwa sifa ya Mungu. Ulivyosimama karibu kabisa ya Mwanao alipokufa msalabani uwe karibu nami saa ya kufa kwangu. Nijalie niweze kutaja jina lako na la Mwana wako nikisema: “Yesu, Maria na Yosef mnisaidie saa ya kufa kwangu. Yesu, maria na Yosef, naomba nife kwa amani kati yenu!” . Amina.
Sala Kwa Mama Wa Uchungu Kuomba Neema ya Pekee
Ee Mama mbarikiwa na Bikira mwenye uchungu, Malkia wa Mashahidi, uliyesimama chini ya msalaba na uliyemtazama Mwana wako akifa, unitazame kwa huruma ya kimama ninayekusikitikia. Kwa sababu ya upanga uliochoma moyo wako, kwa mateso ya maisha yako nakuomba uniangalie kwa wema ukasikilize maombi yangu. Nakuomba, ee Mama, uniombee daima kwa Mwana wako, najua hawezi kukuvyima wewe kitu chochote. Basi, ufanye, Moyo wa Mwanao ukubali kunijalia ombi langu hili …………………(taja ombi lako).
Maana nitamkimbilia nani katika mahitaji na misiba yangu isipokuwa kwako, ee Mama wa huruma? Wewe hasa unaweza kutusaidia sisi tulio bado katika bonde la machozi kwa sababu ulishiriki mateso ya Mwanao kutukomboa. Umtolee Yesu tone moja la Damu yake takatifu. Umkumbushe ya kuwa wewe ni matumaini, furaha na maisha yetu ukanipatie jambo ninalokuomba kwa Yesu Kristo, bwana wetu. Amina.
Utukufu wa Msalaba
Leo tarehe 14 Septemba ni siku inayokumbukwa kwa utukufu wa msalaba.Tunapozungumza msalaba mtakatifu tunazungumzia ushindi uliopatikana pale Bwana Yesu alipotundikwa juu yake na hatimaye kutupatia wokovu.
Hadithi zilizoenea sana zinadai mwaka 326 msalaba halisi wa Yesu uligunduliwa na mtakatifu Helena wa Konstantinopoli,mama wa Kaisari Konstantino I,aliohiji Yerusalemu. Hapo kanisa la Kaburi na Ufufuo wa Yesu lilijengwa mahali penyewe, kwa amri ya Helena na Konstantino, na sehemu ya msalaba iliachwa huko, ila sehemu nyingine zilipelekwa Roma na Konstantinopoli .
Tarehe 14 Septemba ndiyo siku ya pili ya kutabaruku kanisa hilo mwaka 335.
Msalaba nini? Msalaba mtakatifu ni ishara ya upendo kwa mwanadamu kwa kuwa bila Yesu kukubali kuutoa uhai wake pale msalabani tusingelipata ukombozi. Tunapozungumza msalaba tunazungumza ukombozi wa mwanadamu kwa Kuwa tuliupata kupitia msalaba.
Sikukuu ya msalaba ni adhimisho la liturujia ya madhehebu mbalimbali ya Ukristo wa mashariki na vilevile ya Ukristo wa magharibi, ingawa tarehe zinatofautiana
Lengo ni kutukuza chombo cha wokovu wa wanadamu wote kilichotumiwa na Mungu kadiri ya imani ya dini hiyo, yaani Yesu Kristo aliyeuawa juu ya msalaba huko Yerusalemu mwaka 30 hivi.
Wakati wa Ijumaa Kuu hazimisho la kuuabudu msalaba unalenga zaidi mateso ya Yesu Mwanakondoo wa Mungu aliyeondoa dhambi ya ulimwengu,sikukuu hiyo inashangilia utukufu wa fumbo hilo, ambalo Mtume Paulo alilitangaza kuwa fahari yake pekee (Gal 6:14).
Kabla yake, Yesu mwenyewe alizungumzia "kuinuliwa" kwake (Yoh 3:14-15), akimaanisha kuinuliwa msalabani na mbingunivilevile. Hivyo alidokeza kwamba msalaba wake haukuwa aibu, bali hasa utukufu.
Kama wanadamu tunayo misalaba yetu mbalimbali inayotuzunguka na itokeapo atuna budi kuomba neema ya kuweza kuibeba na kuifikisha maala salama kwa ajili ya kujipatia neema na baraka mbalimbali katika kuutafuta ufalme wa mbinguni.
Wednesday, September 13, 2017
Historia ya Mtakatifu Mt.Margareta wa Hungaria,Mtawa(Life of Saint Margareta de'Hungaria)
Mtakatifu Margareta alizaliwa tarehe 28 Januari 1242. Baba yake alikuwa mfalme wa Hungaria akijulikana , ambaye alijenga konventi kwa ajili ya Masista wa Shirika la Mt. Dominiko huko Budapest, mji mkuu wa Hungaria. Mtakatifu Margareta aliishi maisha ya kujitesa sana kwa sababu alikuwa tayari hata kukatwa pua na midomo yake kuliko kukubali kutoka utumwani. Alikufa tarehe 18 Januari, mwaka 1270, akiwa ana umri wa miaka 28 tu.Alishika sana ufukara na maisha ya malipizi na alijaliwa njozi mbalimbali
Mtakatifu Margareta alikuwa binti wa mwisho wa mfalme Bela IV wa Hungaria ,kaka wa Elizabeti wa Hungaria .Kama shangazi yao huyo, yeye na dada yake Kinga pia wanaheshimiwa kama mtakatifu, mbali ya dada mwingine,Yolanda, anayeheshimiwa kama mwenye heri.Utakatifu wake ulikubaliwa tangu zamani na ulitangazwa rasmi na Papa Pius XII tarehe 19 Novemba 1943.
Mtakatifu Margareta alizaliwa uhamishoni kwa sababu Wamongolia walikuwa wameteka Hungaria. Basi wazazi wake walitoa nadhiri kwa Mungu kwamba hao wavamizi wakiondoka, wao watamtolea binti yao utawani.
Wamongolia walifukuzwa mwaka uleule, na baada ya miaka michache Mtakatifu Margareta alikabidhiwa kwa masista Wadominiko kwa malezi.
Mnamo mwaka 1254 aliweka nadhiri za kitawa na baadae mwaka 1261 alivaa shela.Inasemekana mtakatifu Margareta hakupata elimu sana, lakini alipenda kusomewa Biblia akasali sana, akiheshimu hasa mateso ya Yesu na ekaristi.
Jan 18 - St Margaret of Hungary (1242-70) - Catholicireland ...
Wednesday, September 6, 2017
Tuwaombee wanaouguwa kansa(We pray for those people suffered from cancer)
We pray together:(We pray through the prayer of St.Jude)
God of healing mercy, in Jesus your Son you stretch out your hand in compassion, restoring the sinner, healing the sick, and lifting up those bowed down. Embrace us now in your loving care, particularly those afflicted with cancer, for whom this intention is offered. May the Spirit of Jesus bring us all health in soul and body, that with joy and thanksgiving we may praise you for your goodness, through the same Jesus Christ our Lord. Amen.
as prepared by Fr. Mark Brummel, CMF
Director, St. Jude League

Tuesday, September 5, 2017
Maisha ya Mtakatifu Papa Gregori Mkuu(Life of Saint Pope Gregori)
Mtakatifu Papa Gregori Mkuu alizaliwa Roma, Italia, mwaka 540 hivi katika familia ya ukoo maarufu ya Anicia, akiwa mtoto wa seneta Gordianus na wa Silvia, ambao wanaheshimiwa kama watakatifu.Shangazi zake Emiliana na Tarsila, wakiishi nyumbani mwao kwa sala na toba kama mabikira wa Kristo, walimtia pia hisia za Kikristo kweli. Kati ya mababu wake kulikuwa na Papa Felis II toka mwaka 483 hadi 492 na mwingine Papa Agapito I toka mwaka 535 hadi 536.Mtakatifu Papa Gregori alifariki Roma tarehe 12 Machi 604.
Alipokuwa na umri wa miaka 25 tu alifuata nyayo za baba yake katika shughuli za utawala na mwaka 572 alichaguliwa kuwa mkuu wa jiji la Roma. Kutokana na ugumu wa nyakati hizo, kazi hiyo ilimdai awajibike katika masuala mengi tofauti ikimuandaa kwa majukumu yake ya baadaye.
Kwa namna ya pekee alidumisha hisi ya kuwepo haja ya utaratibu na nidhamu katika mambo yote. Ndiyo sababu baadaye, akiwa papa, alihimiza maaskofu waendeshe shughuli zao kwa kufuata mfano wa uwajibikaji na utekelezaji wa sheria wa watawala wa kisiasa.
Hata hivyo maisha hayo hayakuweza kumridhisha. Kwa hiyo, baada ya muda mfupi aliyaacha, na akivutiwa na mfano wa Mtakatifu Benedikto wa Nursia, aligeuza nyumba yake mjini kuwa monasteri na kujifanya mmonaki, halafu akajitahidi katika maisha ya sala na kutafakari Biblia na maandishi ya mababu wa Kanisa. Pia alianzisha monasteri 6 katika kisiwa cha Sicilia. Maisha hayo ya kuhusiana na Bwana tu yalimuandaa kutoa mafundisho yake bora na yalizidi kumvutia hadi mwisho, kama alivyoandika mara nyingi baadaye.
Lakini mapema, kutokana na sifa na mang'amuzi yake, Papa Pelagio II alimfanya shemasi akamtuma kama balozi kwenye ikulu ya Konstantinopoli, alipobaki miaka sita akiendelea kuishi kimonaki na wenzake kadhaa kati ya fahari za mazingira ya Kikaisari. Majukumu yake makuu yalikuwa kukomesha mabaki ya mabishano kuhusu ubinadamu wa Kristo na hasa kupata msaada wa Kaisari dhidi ya uvamizi wa Walombardi nchini Italia. Hata miaka hiyo ilimuandaa kwa kazi zake za baadaye.
Aliporudi Roma,mnamo mwaka 586, akarejea monasterini, lakini Papa huyo alimfanya katibu wake. Ilikuwa miaka migumu kwa mvua za mfululizo,mafuriko na njaa mjini Roma na sehemu mbalimbali za Italia. Hatimaye tauni ilifyeka watu wengi, Pelaji II akiwa mmojawao.
Hivyo tarehe 3 Septemba 590 alishangiliwa na wakleri,maseneta na umati wa watu kwa kauli moja awe Papa wa 64. Ndiye mmonaki wa kwanza kufikia Upapa, ingawa hakutaka, hata akajaribu kukimbia, lakini bure. Ilimbidi akubali mapenzi ya Mungu, akaanza mara kuwajibika.
Mapema alionekana kuwa na mitazamo na maamuzi sahihi na kujitokeza kama mtendaji bora upande wa Kanisa na hata upande wa jamii na siasa (kwa sababu hiyo aliitwa "Mrumi wa mwisho"), ingawa alikuwa na afya mbovu, kiasi cha kulazimika mwishoni kubaki kitandani kwa siku kadhaa. Hasa mafungo makali ya kimonaki yalikuwa yamesababisha matatizo makubwa ya tumbo.
Tena sauti yake ilikuwa ndogo kiasi kwamba mara nyingi ilimbidi kumpa shemasi kazi ya kutangaza hotuba yake alipoendesha ibada makanisani kati ya waumini waliomheshimu sana kwa kumuona anawafanya wajisikie salama. Hotuba hizo zinaonyesha alivyotekeleza alichoandika: “Ni lazima mhubiri achovye kalamu kalamu yake katika damu ya moyo wake; hapo ataweza kufikia masikio ya majirani wake”.
Aliwasiliana na viongozi wa nchi mbalimbali za Ulaya, na hasa wa kabila la Wafaranki ambalo lilikuwa la kwanza kati ya yale ya Kijerumani kuingia Ukatoliki moja kwa moja tena lilijitokeza lenye nguvu kuliko yote.
Vilevile alifanikisha uongofu wa makabila ya aina hiyo yaliyoteka Uingereza, alipomtuma kama mmisionari Augustino wa Canterbury,priori wa monasteri yake ya Mt. Andrea.
Alilinda pia Roma dhidi ya uvamizi wa Agilulf , mfalme wa Walombardi, lakini, kinyume na Kaisari aliyewaona ni washenzi na wavamizi tu ambao wadhibitiwe au kuangamizwa, Gregori, kwa mtazamo wa kichungaji, alijenga nao uhusiano mpya ili kuwaleta kwenye Kanisa Katoliki kutoka uzushi wa Ario, kama alivyofanya pia na Wagoti wa Hispania na walioendelea kufuata dini za jadi.
Akilenga amani ya kudumu nchini Italia, kwa msaada wa Theodolinda,malkia Mkatoliki wa Walombardi, alifanikiwa kwanza kusimamisha mapigano na Walombardi kwa miaka mitatu mwaka 598-601, na kuanzia mwaka 603 kwa muda mrefu zaidi.
Lakini mafanikio yake hayo, yaliyoandaa mengine kwa siku za mbele, yalimfanya achukiwe na watu wa Konstantinopoli.
Alipambana na matatizo mengine ya Italia, kama vile mafuriko, njaa, tauni, akisimamia kwa usawa masuala ya kijamii yaliyopuuziwa na wawakilishi wa kaisari. Kwa mapato ya mali ya Kanisa, aliyoisimamia vizuri na kwa kuzingatia haki, kati ya mambo mengine alilisha wenye njaa na kukomboa watumwa. Alishughulikia hata huduma ya maji.
Alirekebisha liturujia ya Kiroma, akipanga matini ya zamani na kutunga mengine mapya, pamoja na kushughulikia muziki wa ibada za Kilatini ambao kwa heshima yake unaitwa wa Kigregori.
Vitabu vyake, hasa vya maadili na vya ufafanuzi wa Maandiko matakatifu unaolenga utekelezaji, barua 848 zilizotufikia pamoja na hotuba mbalimbali vinashuhudia kazi zake nyingi na ujuzi wake wa Biblia.
Pia aliandika maisha ya watakatifu kadhaa wa Italia walioishi si zamani sana, kama vile Benedikto wa Nursia ambaye tunamfahamu kwa njia hiyo tu. Ni kwamba rafiki yake, Petro shemasi, alidhani wakati ule maadili yameharibika kiasi cha kuzuia upatikanaji wa watakatifu kama walivyotokea zamani. Basi, Gregori alimuonyesha kwamba, kinyume chake,utakatifu unawezekana daima, hata katika mazingira magumu. Masimulizi ya maisha yao yanaendana na hoja za kiteolojia zinazofafanua masuala mbalimbali.
Kitabu kingine kilichoacha athari kubwa ni "Mwongozo wa Kiuchungaji" kwa ajili ya maaskofu, ambao ulitafsiriwa mapema hata kwa Kigiriki na kwa Kisaksoni. Alikiandika mwanzoni mwa Upapa wake akautekeleza mwenyewe. Humo anasisitiza ukuu wa cheo hicho na majukumu yanayoendana nacho, ambayo yanadai askofu awe kielelezo kwa wote. Kwa ajili hiyo anapitia kwa makini aina mbalimbali za waumini na saikolojia zao ili kuonyesha namna ya kuwasaidia. Hatimaye anakazia unyenyekevu wa kutojiona sawa mbele ya Hakimu mkuu kutokana na mafanikio fulanifulani: “Mtu anaporidhika kwa kutimiza maadili mengi, ni vema afikirie mapungufu yake na kujinyenyekesha: badala ya kuzingatia mema aliyofanya, ni lazima azingatie yasiyofanyika”. Kwake uchungaji ni “ars artium”, yaani sanaa kuu kuliko zote.
Katika maandishi yake, hakukusudia kamwe kutoa mafundisho mapya, bali kuwa mwangwi mnyenyekevu wa mapokeo ya Kanisa. Alieneza mafundisho ya Augustino wa Hippo, akisisitiza kama yeye hali ya dhambi ya binadamu, nafasi ya kwanza ya neema katika wokovu pamoja na imani katika uteuzi wa watakaookoka uliofanywa na Mungu.
Pia alichangia ustawi wa fundisho la uwepo wa toharani.
Mtu huyo alikuwa wa ajabu kuliko kazi zake, akivutia kwa nguvu na upendevu wa tabia. Ndani mwake upana wa moyo na roho ya Kikristo vilitegemeza yote.Inawezekana kusema ndiye Papa wa kwanza kutumia mamlaka upande wa siasa pia, lakini bila kuweka pembeni majukumu yake ya kiroho kama mtu aliyeungana kweli na Mungu na hivyo aliweza kuona la kufanya. Kwake ilikuwa muhimu kila mmoja atafakari matukio ya maisha katika mwanga wa Neno lake kwa sababu historia ya wokovu haikumalizika zamani, bali inaendelea moja kwa moja hata katika nyakati ngumu kama zile alizopitia mwenyewe.
Nguvu ya Njia ya Msalaba(Power of Holy Cross)
Njia ya msalaba ni nguvu tosha ya kushiriki mateso moja kwa moja ya Yesu na ni moja ya kujipatia baraka nyingi za kimbingu.Hivyo natamani kila mwanadamu kuisali hii ibada ya njia ya msalaba katika kushiriki mnyororo wa moja kwa moja na Bwana Yesu.
Kuhusu njia ya Msalaba
Njia ya Msalaba ni desturi ya sala inayolenga kumfuata Yesu Kristo hadi msalabani na kaburini.
Desturi hiyo ilianzia na Wakristo wa Ulaya walipozidi kutembelea Nchini takatifu katika Karne za Kati. Ni hasa wafuasi wa Mtakatifu wa Asizi walioeneza desturi hiyo kila mahali
Mengi ya makanisa ya Wakatoliki yana vielelezo 14 vilivyopangwa kwa kawaida ukutani kwa umbali fulani ili kuwezesha waamini kutembea kati ya moja na nyingine huku wakiendelea kutafakari juu ya mateso ya Yesu, jinsi ambavyo wangefanya mjini Yerusalemu, ili kuelewa zaidi upendo wa Mungu , kuchukia dhambi na kuzifidia
Hata hivyo baadhi ya Walutheri na Waaglikana wanapenda desturi hiyo.
Desturi hiyo inaweza kufuatwa na mtu mmojammoja au kwa makundi hata makubwa.
Mbali ya kila ijumaa ya mwaka, waamini wengi wanafuata njia hiyo wakati wa Kwaresima, na kwa namna ya pekee ijumaa kuu
Mbali ya vituo 14 vilivyozoeleka zaidi, wengine wanapenda kuviongeza, kuvipunguza au kuvibadilisha hasa kwa kufuata zaidi habari za injili na kumalizia na ufufuko wake.

NJIA YA MSALABA KATIKA TAFAKARI YA HAKI NA AMANI
Sala ya kuanzia Ibada:
Yesu Mkombozi wetu tunakuja mbele yako kutafakari ulivyoteswakwa ajili yetu. Tunaomba tafakari hii itusaidie kupendana zaidi, na kusaidiana kuishi magumu tunayokutana nayo katika maisha yetu. Kwa Sala hii yenye kutafakari juu ya haki na amani, tunakuomba utusaidie tutambue kwamba wewe umekuja kati yetu kushiriki maisha yetu na kutuonyesha njia ya kuepuka dhambi na uovu kwakufuata mafundisho yako.
Ee Yesu mwema, Bikira Maria Mama yako alikuwa nawe katika njia yako ya msalaba. Nasi tunamwomba awe nasi katika sala hii ya Njia ya Msalaba ili hatimaye tunaposhiriki kujenga jamii iliyo bora zaidi, tupate nguvu na msaada kwa njia ya maombezi yake.
Kituo cha Kwanza
YESU ANAHUKUMIWA AFE
Katika jamii yetu tunawakuta watu wengi wanaonyimwa haki zao. Mbinu zinazotumiwa kupotosha haki za watu ni pamoja na ucheleweshaji wa kesi unaoambatana na kupotea kwa majalada kunakoambatana na rushwa. Mfumo mzima unaohusika na utetezi wa haki za watu una kasoro nyingi. Tujifunuo mbele ya Mwonyozi Mungu tuone ni kwa njia zipi tumewakosea watu haki.
Ee Yesu, wewe ulikuja kuwaponya wenye dhambi. Tunakuomba utusamehe kwamakosa yetu ya kupotosha haki, hasa pale tuliposhiriki rushwa au udanganyifu. Tunakuomba utusaidie kuvishinda vishawishi vinavyotuvuta kupotosha haki za watu wako, hasa watu wanyonge na maskini
Kituo cha Pili
YESU ANAPOKEA MSALABA
Tukichunguza jamii yetu tunaona watu mbalimbali ambao wanatumikia adhabu wasiostahili. Miongoni mwa hawa ni wale waliomo magerezani kwa tuhuma za uongo, ama hukumu zisizo za haki, wanyonge wanaonyanyaswa na kunyimwa haki zao zikiwemo huduma za kijamii na hivyo kuishi maisha duni na ya mateso. Wapo pia wale wanaouawa kwa tuhuma za wizi. Ni mambo ya namna hii ndio tunaitwa kuyatafakari leo na kutambua kuhusika kwetu.
Ee Yesu, tunakuja kwako kukuomba utusaidie kubadilika nakuacha kufanya mambo yanayoleta mateso na shida kwa wengine. Utusaidie mateso tunayoyapata tuyapokeekama changamoto ya kukua kiroho na kiutu. Pia utujalie moyo wa kushiriki mateso yanayowakabili wenzetu na tufanye kazi kwa bidii katika kupunguza shida na mateso miongoni mwetu.
Kituo cha Tatu
YESU ANAANGUKA MARA YA KWANZA
Umaskini ni mzigo unaoielemea jamii yetu na kutuangusha wengi dhambini. Vijijini na mijini hali ya maisha ya wanyonge ni mbaya. Mahitaji na huduma muhimu ni mambo magumu kwa wanyonge kuyafanikisha - hata wengine hufa kwa kukosa tiba. Hali ya umaskini inachangiwa kwa kiasi kikubwa na sera pamoja na mipango mibovu na tabia ya kutowajibika. Uvivu, rushwa na ufisadi, ubinafsi, uchoyo, matumizi mabaya ya muda na mali, yote haya hukwamisha jitihada zinazofanywa dhidi ya umaskini.Tumwombe Mungu atusaidie kuwa na moyo wa uwajibikaji na kusaidiana, na hasa kujali manufa na maslahi ya kila mmoja.
Ee Yesu, Mfalme wa Haki naAmani uwajalie maskini wote moyo wa kuungana na kuwajibika katika kukabiliana na umaskini kwa kufanya kazi kwa bidii na kushauri marekebisho ya sera na mipango mibovu. Uwaangazie wanaojinufaisha kutokana na umaskini wa wanyonge watambue ubaya wake, utusaidie kuushinda ubinafsi na uchoyo miongoni mwetu, tukatimize agizo lako la kufanya kazi ya kuleta nafuu ya maisha ya watu wako.
Kituo cha Nne
YESU ANAKUTANA NA MAMA YAKE
Kwenye jamii zetu tunakutana na watu wanaoteseka kwa shida, dhiki na mateso ya aina mbalimbali. Watu hawa wanaweza kuwa familia zinazofarakana na kukosa amani, yatima na wajane, wagonjwa, wanyonge na wahitajimbalimbali. Pia wapowatu miongoni mwetuwanaotawaliwa na pesa, mali na madaraka na kuusahau ukweli. Watu wa aina hii tunakutana nao kila wakati. Tujiulize na kutafakari kama katika hali hiyo tunasaidianaje? Pia kila mmoja wetu ajiulize anawasaidia namna gani watu wenye shida ndani ya familia na katika jumuiya yake.
Ee Yesu, wewe ulikuja ili tuwe na uzima tena tuwe nao tele, (rejea Yn 10: 10). Tunakusihi utusaidie tushirikiane na kutumia vipaji vyetu katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo mengi ndani ya jamii yetu ambayo yanawaletea watu wako mateso na kuwakosesha amani. Tunaomba kwa maombezi ya Mama yako tukubali kutumika kama vyombo vyako vya kujenga amani.
Kituo cha Tano
SIMONI WA KIRENE ANAMSAIDIA YESU
Katika maisha yetu tunakutana na watu walio taabani kwa mateso. Hawa wanahitaji msaada wa wengine na zaidi ya yote wanahitaji kumwendea Yesu aliyesema “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha” (Mt 11: 28). Nasi tunaalikwa kusaidia watu katika kubeba Msalaba wao unaowaelemea kwa njia ya sala, uwajibikaji na kujali manufaa ya wote na pia kujitolea kwa ajili ya wengine.
Ee Yesu tunakuomba utusaidie tuwe na bidii na ushupavu wa kusaidiana katika shida na mateso ya watu miongoni mwetu. Utuimarishe tudumu katika sala na kushiriki mateso na shida za wengine, ili tuweze kuenenda pamoja nawe katika safari yetu ya pamoja hapa duniani.
Kituo cha Sita
VERONIKA ANAPANGUSA USO WA YESU
Katika kituo hiki tutafakari jinsi wengi tunavyobaki kuangalia tu uovu ukiendelea kutendeka bila kuchukua hatua, na kwa kufanya hivyo tunaufanya uovu uwe ni kitu cha kawaida katika jamii yetu. Tutafakari hali ya huduma katika shule zetu na katika zahanati na hospitali zetu. Huduma kwa jumla ni duni kwa walio wengi wakiwemo wale wanaokosa ndugu wa kuwasaidia. Hapa tunapokea wito wa pekee kama anavyotufundisha na Veronika, tukijua kwamba hizi ni huduma muhimu kwa kila mwanadamu, na ni haki kwa ki la mmoja.
Ee Yesu, Mfalme wa Haki na Amani, tunakuomba utujalie ushujaa na ujasiri wa Mtakatifu Veronika. Katika maisha yetu ya kila siku, tuweze bila woga kuheshimu, kulinda na kutetea haki za watu hasa katika huduma ya elimu na afya. Tunakuomba utujalie umoja na mshikamano kwa kuwa ndio njia bora itakayotusaidia kutimiza wito huo kikamilifu.
Kituo cha Saba
YESU ANAANGUKA MARA YA PILI
Katika jamii yetu tunakutana na watu wengi walio katika shida na mateso makubwa kama ukosefu wa maji safi na salama, ukosefu wa mahitaji muhimu, uduni wa huduma mbalimbali, hali mbaya ya Magereza, na mazingira machafu. Kwa baadhi yetu hali ni taabani na watu wamefika hatua ya kukata tamaa. Njia ya kuwasaidia walio taabani ni kutoa misaada, kurekebisha sera na mipango mibovu na kusukuma utekelezaji wa mipango na sheria nzuri. Pia yatupasa kuchukua wajibu wetu wa pamoja kama jamii katika kuboresha maisha yetu. Yatupasa tujue kwamba njia ya ukombozi wetu ni kubeba msalaba kama Yesu mwenyewe. Tunapokutana na magumu tusikate tamaa kwani Mungu yuko nasi na ndiye tumaini letu.
Ee Yesu, wewe umetufundisha kuwa tutapata tuzo kwa kuwasaidia na kuwahudumia wenye shida mbalimbali, (rej. Mt 25:40,45). Utusaidietufanyebidii kuondoa shidazinazowakabili watu wako.
Kituo cha Nane
WANAWAKE WANAMLILIA YESU
Tunapotafakari kituo hiki, tunajifunza kuwa na moyo wa huruma, kwa Yesu mteseka katika watu wenye shida na mateso mbalimbali. Hawa ni pamoja na wajane na yatima wanaodhulumiwa haki yao ya urithi, wanawake wanaonyanyasika katika familia zao, walezi wanaolemewa mzigo wa kutunza na kulea yatima.
Ee Yesu, unatuambia "Heri wenye rehema, maana hao watapata rehema” (Mt 5: 7). Tunakuomba utusaidie moyo wa huruma na kutuwezesha kuionyesha huruma yetu kimatendo kwa wote tunaokutana nao kila siku ya maisha yetu.
Kituo cha Tisa
YESU ANAANGUKA MARA YA TATU
Sisi leo, tumwone na kumtafakari Yesu anayelemewa na msalaba na mateso na kuanguka mara ya tatu katika waathirika wa ukimwi. Hawa ni watu wenye mateso makali kimwili, kifikra na hata kiroho. Ni watu ambao tayari jamii imekwishawahukumu. Pamoja na majeraha yake, Yesu anainuka na kuendelea na safari ya ukombozi. Yesu anatualika nasi tusibaki katika huzuni na kukata tamaa bali tuinuke na kuendelea kwani naye anateseka katika mateso yetu, na ndiye tumaini letu. Tuwakumbuke hawa kwa moyo wa huruma na ukarimu, tukijua kwamba Mungu ni mwema na mwenye huruma kwetu sote. Pamoja na waathirika tuwaangalie yatima na wajane wa janga la ukimwi. Tuwasaidie pia walezi ambao wanabeba wajibu wa kuwalea na kuwatunza yatima wakati wao wenyewe hawana uwezo. Sisi sote tujitafakari na tufanye bidii kujiheshimu na kuepuka vitendo vinavyoendeleza maambukizi ya ukimwi.
Ee Yesu, tunakushukuru kwa kuwa Ukombozi wako ni kwa ajili yetu sote. Tunawaombea waathirika wote wajue kwamba mateso yao sio mwisho wa yote. Tunaomba msaada wako ili tuweze kuishi nao vizuri na kuwasaidia. Tupe uchaji wa kutambua ubaya wa dhambi ya uzinzi na uasherati ili kuepukana na janga hilo. Na tunakusihi utujalie ufahamu wa kupata tiba ya ugonjwa huo.
Kituo cha Kumi
YESU ANAVULIWA NGUO
Tunapotafakari moja ya hitaji muhimu kwa mwanadamu ambalo ni mavazi tunaona kuna kasoro nyingi. Miongoni mwetu wapo watu wengi ambao hawawezi kujipatia mavazi kwa ajili ya kusetiri mwili, wengine wananunua mavazi mengi na ya fahari kama kufuru mbele ya Mungu. Baadhi wanavaa mavazi yanayoonyesha kutoheshimu utu wao.Tunaitwa leo kujitafakari kibinafsi na kama jamii kuona upotevu huo na kurekebisha.
Ee Yesu, tunakuomba utufungue macho ya mioyo yetu tupate kuuona ubaya wetu katika matumizi ya mavazi, na kujua kwamba mavazi ni hitaji msingi kwa kila mwanadamu. Tunakuomba utuwezeshe kujirekebisha na kuwa na moyo wa ukarimu kwa wanaokosa mavazi na pia kushiriki katika kupunguza umaskini ili kila mmoja aweze kujipatia mahitaji msingi.
Kituo cha Kumi na Moja
YESU ANASULUBISHWA MSALABANI
Hapa Yesu ni kielelezo cha watu wanaoteseka. Nasi twaweza kuwa tumechangia katika kuleta mateso kwawengine. Miongoni mwetu wako walioingia katika mateso kwa sababu ya kutetea na kuwasaidia walio katika matatizo na shida mbalimbali. Baadhi yetu tumeshiriki vitendo vya kujichukulia sheria mkononi, na wengine tumeiba fedha, mali na rasilimali ya umma hata kuingia katika ufisadi, na kwa njia hii kusababisha maisha duni kwa wenzetu. Hali mbaya ya maisha ya watu imeleta hasira ya jamii ambayo inaendelea kuenea katika nchi yetu. Vitendo vinavyodhihirisha hasira ya jamii ni vingi, na matokeo yake natari kwa jamii yetu na taifa letu.Yesu anatufundisha kujitoa sadaka na kutuonya tuepuke mambo yanayosababisha mateso kwa watu wake. Pia anatuonya kuepuka kuwaka hasira kwani itaangamiza jamii yetu. Badala yake anatualika tushiriki sote kuhakikisha maisha bora kwa wote, na hivyo amani yetu iweze kudumu.
Ee Yesu, tunakuomba utujalie moyo wa ujasiri katika kutetea haki na kuwasaidia walio katika mateso. Utusaidie kuepuka vitendo vinavyowaletea watu wako mateso. Tunaomba neema na msaada wako katika kukamilisha nia ya kujenga ushirikiano kati yetu na kujali manufaa na maslahi ya wote.
Kituo cha Kumi na Mbili
YESU ANAKUFA MSALABANI
Tumwangalie Yesu anayekufa msalabani bila hatia, akibeba dhambi zetu ili tupate kuokoka. Nasi tuna wajibu wakushiriki kazi ya ukombozi wa mwanadamu kimwili na kiroho. Wajibu huo ni katika familia zetu, jumuiya, taifa na jamii nzima. Tukitimiza vizuri wajibu zetu, tunaendeleza kazi ya ukombozi. Na mwisho wa yote tutaweza nasi kusema pamoja na Yesu, “yametimia.” Kama binadamu tunashindwa mara kadhaa kwa sababu ya udhaifu wetu hata kusababisha vifo bila sababu miongoni mwetu. Tumwombe toba Yesu pale tuliposhindwa, na tunapomtafakari Yesu aliyekufa msalabani, tumpe nafasi afishe ndani mwetu na kati yetu udhaifu wetu na kasoro zinazokwamisha kazi ya ukombozi wa mwanadamu.
Ee Yesu, uliyekufa Msalabani kwa ajili ya Ukombozi wetu, tunakuomba utusaidie tushiriki kikamilifu kazi ya ukombozi na ufishe ndani mwetu na katika mifumo na miundo yetu udhaifu unaokwamisha kazi ya ukombozi katika jamii yetu.
Kituo cha Kumi na Tatu
YESU ANASHUSHWA MSALABANI
Yesu anashushwa msalabani akiwa amekamilisha kazi yake, yaani mpango wa Mungu wa ukombozi wetu. Kwa maisha yetu sote zawadi ya uhai ina lengo. Tumekuja duniani tukiwa pia tumepewa wajibu. Ndio kuboresha maisha yetu, ya jamii na mazingira tunamoishi kwa faida ya kizazi cha sasa na vile vijavyo. Tumekwishaona maeneo mengi ya uwajibikaji wetu kwakadiri ya mafundisho ya Maandiko na hali tunamoishi leo. Tunapoendelea na safari yetu ya kushiriki ukombozi, tutumie nafisi na vipaji vyetu kikamilifu kutimiza mafundisho ya Neno katika maisha yetu ya kila siku.
Ee Yesu, tunataka kuweka ahadi leo ya kukufuata kwa matendo, mienendo na fikra zetu. Kuweza kutimiza ahadi yetu tunahitaji msaada wako. Ee Yesu uwe nasi.
Kituo cha Kumi na Nne
YESU ANAZIKWA KABURINI
Ndani yako Yesu, tunataka kuzika udhaifu wetu wa kibinafsi na wa kijamii. Sisi tunapo kutafakari katika njia yako ya Msalaba tunatambua wajibu wetu wa kujitoa sadaka. Tuna mengi uliyotujalia, lakini tunavutwa kuyatumia vibaya ama kutoyatumia kabisa. Tunataka kuzika yote yanayotukwamisha na tunakuomba utusaidie tudumu katika uwajibikaji Kikristu.
Ee Yesu tunatamani sana kutekeleza nia zetu, lakini tunajua tunahitaji msaada wako. Tunakuomba tunapofanya bidii kutekeleza nia hizo wewe uwe nasi kila wakati.
SALA YA MWISHO
Ee Yesu, tunaomba tafakari tuliyofanya na sala tuliyoisali itusaidie kuwa wakamilifu ili tuweze kuyashinda maovu. Utupe ujasiri wa kutetea ukweli, haki na amani. Kwa kazi yetu, tuweze kuleta faraja kwa wale wenye mateso. Ee Yesu, tunaomba msaada na neema yako ili tuweze kuziweka nia zetu katika matendo yetu ya kila siku. Tunaomba Bikira Maria Mama yako awe nasi katika maisha yetu. Maombi yake yatusaidie tuwe na moyo wa kujitakatifuza na kujenga jamii yenye misingi ya Ukweli, Haki na Amani.
Kabla ya kila kituo:
K: Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru;
W: Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako mtakatifu.
Baada ya kila kituo:
'Baba Yetu, 'Salamu Maria' na 'Atukuzwe Baba',
K: Ee Bwana utuhurumie! W: Utuhurumie!
K: Roho za waamini marehemu, wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. W: Amina
(Kutoka “NJIA YA MSALABA KATIKA TAFAKARI YA HAKI NA AMANI” - Kitabu kimechapishwa Tume ya Haki na Amani - TEC, Dar es Salaam (Aprili 2004))

Subscribe to:
Posts (Atom)