Wednesday, September 13, 2017

Historia ya Mtakatifu Mt.Margareta wa Hungaria,Mtawa(Life of Saint Margareta de'Hungaria)



Mtakatifu Margareta  alizaliwa tarehe 28 Januari 1242. Baba yake alikuwa mfalme wa Hungaria akijulikana , ambaye alijenga konventi kwa ajili ya Masista wa Shirika la Mt. Dominiko huko Budapest, mji mkuu wa Hungaria. Mtakatifu Margareta aliishi maisha ya kujitesa sana kwa sababu alikuwa tayari hata kukatwa pua na midomo yake kuliko kukubali kutoka utumwani. Alikufa tarehe 18 Januari, mwaka 1270, akiwa ana umri wa miaka 28 tu.Alishika sana ufukara  na maisha ya malipizi  na alijaliwa njozi mbalimbali

Mtakatifu Margareta  alikuwa binti wa mwisho wa mfalme Bela IV  wa Hungaria ,kaka wa Elizabeti wa Hungaria .Kama shangazi  yao huyo, yeye na dada  yake Kinga pia wanaheshimiwa kama mtakatifu, mbali ya dada mwingine,Yolanda, anayeheshimiwa kama mwenye heri.Utakatifu wake ulikubaliwa tangu zamani na ulitangazwa rasmi  na Papa Pius XII  tarehe 19 Novemba 1943.

Mtakatifu Margareta alizaliwa uhamishoni kwa sababu Wamongolia walikuwa wameteka Hungaria. Basi wazazi   wake walitoa nadhiri  kwa Mungu kwamba hao wavamizi wakiondoka, wao watamtolea binti yao utawani.

Wamongolia walifukuzwa mwaka uleule, na baada ya miaka michache Mtakatifu Margareta alikabidhiwa kwa masista Wadominiko  kwa malezi.
Mnamo mwaka 1254  aliweka nadhiri za kitawa na baadae mwaka 1261 alivaa shela.Inasemekana mtakatifu Margareta hakupata elimu sana, lakini alipenda kusomewa Biblia akasali  sana, akiheshimu hasa mateso ya Yesu na ekaristi.

Jan 18 - St Margaret of Hungary (1242-70) - Catholicireland ...






No comments:

Post a Comment