Mtakatifu Veronica Giuliani anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu bikira .Maandiko yanatuambia Mtakatifu Veronica Giuliani aliheshimiwa mara baada ya kufa, na kesi ya kumtangaza rasmi ilicheleweshwa na uchunguzi wa maandishi yake marefu.
Mtakatifu Veronica Giuliani alitangazwa kuwa mwenye heri mnamo Juni 1804 na Papa Pius VII na baadae alitangazwa kuwa mtakatifu tarehe 26 Mei 1839 na Papa Gregori XVI.
Maandishi ya Mtakatifu Veronica Giuliani yanasimulia alivyoanza kujaliwa karama za pekee akiwa na umri wa miaka 3 tu, alipokuwa anaitwa Orsola.
Pia alijiunga na Waklara Wakapuchini wa monasteri ya Città di Castello mwaka 1667 ambapo alikuja kuwa abesi tangu mwaka 1716 hadi kifo chake.
Kwa namna ya pekee Mtakatifu Veronica Giuliani aliambatana na Yesu msulubiwa kadiri ya karama ya Fransisko wa Asizi.Na kadiri ya maandishi Kanisa Katoliki linakubali ukweli wa madonda matakatifu aliyosema alikuwanayo tangu tarehe 5 April 1697 hadi kifo chake.
Katika agizo la padri aliyemuongoza kiroho, na aliandika kirefu takribani kurasa 22,000 kwa mikono bila ya sahihisho lolote ambazo ni kumbukumbu za maisha yake yote, ambazo zilitolewa baada ya kifo chake kwa jina Il Tesoro Nascosto (ni magombo 36).
Kwa mujibu wa shajara hiyo, Veronika Giuliani anahesabiwa kati ya Wakristo wanasala waliojaliwa mang'amuzi ya juu zaidi.
No comments:
Post a Comment