Friday, September 15, 2017

Utukufu wa Msalaba

 Image result for msalaba mtakatifu
Leo tarehe 14 Septemba ni siku inayokumbukwa kwa utukufu wa msalaba.Tunapozungumza msalaba mtakatifu tunazungumzia ushindi uliopatikana pale Bwana Yesu alipotundikwa juu yake na hatimaye kutupatia wokovu.
Hadithi zilizoenea sana zinadai mwaka 326 msalaba halisi wa Yesu  uligunduliwa na mtakatifu Helena wa Konstantinopoli,mama  wa Kaisari Konstantino I,aliohiji Yerusalemu. Hapo kanisa la Kaburi na Ufufuo wa Yesu  lilijengwa mahali penyewe, kwa amri ya Helena na Konstantino, na sehemu ya msalaba iliachwa huko, ila sehemu nyingine zilipelekwa Roma  na Konstantinopoli .
Tarehe 14 Septemba  ndiyo siku ya pili ya kutabaruku  kanisa hilo mwaka 335.

Msalaba nini? Msalaba mtakatifu ni ishara ya upendo kwa mwanadamu kwa kuwa bila Yesu kukubali kuutoa uhai wake pale msalabani tusingelipata ukombozi. Tunapozungumza msalaba tunazungumza ukombozi wa mwanadamu kwa Kuwa tuliupata kupitia msalaba.

Sikukuu ya msalaba ni adhimisho  la liturujia ya madhehebu  mbalimbali ya Ukristo wa mashariki na vilevile ya Ukristo wa magharibi, ingawa tarehe zinatofautiana
Lengo ni kutukuza chombo cha wokovu wa wanadamu  wote kilichotumiwa na Mungu  kadiri ya imani  ya dini  hiyo, yaani Yesu Kristo  aliyeuawa juu ya msalaba  huko Yerusalemu  mwaka 30 hivi.

Wakati wa Ijumaa Kuu hazimisho la kuuabudu msalaba unalenga zaidi mateso ya Yesu Mwanakondoo wa Mungu  aliyeondoa dhambi  ya ulimwengu,sikukuu  hiyo inashangilia utukufu wa fumbo hilo, ambalo Mtume Paulo alilitangaza kuwa fahari yake pekee (Gal 6:14).
Kabla yake, Yesu mwenyewe alizungumzia "kuinuliwa" kwake (Yoh 3:14-15), akimaanisha kuinuliwa msalabani na mbingunivilevile. Hivyo alidokeza kwamba  msalaba wake haukuwa aibu, bali hasa utukufu.

Kama wanadamu tunayo misalaba yetu mbalimbali inayotuzunguka na itokeapo atuna budi kuomba neema ya kuweza kuibeba na kuifikisha maala salama kwa ajili ya kujipatia neema na baraka mbalimbali katika kuutafuta ufalme wa mbinguni.



Image result for msalaba mtakatifu

No comments:

Post a Comment