Wednesday, September 27, 2017

Maisha ya Mtakatifu Gertrudi wa Thuringia

Mtakatifu Gertrudi alizaliwa katika mji wa Eisleben , kwenye mkoa wa Thuringia, kwenye nchi ya Ujerumani mnamo Tarehe 6 Januari 1256 na alifariki tarehe 17 Novemba 1302.
Mtakatifu Gertruda katika utoto wake alilelewa na watawa wa kike ambao ni Wabenedikto  wa urekebisho wa Citeaux huko Helfta , ambako alifaulu vizuri katika masomo yake, hasa falsafa,historia na fasihi.
Image result for Life of saint Gertrude of Thuringia
Mtakatifu Gertruda akijulikana kama Getrudi mkuu alijiweka kabisa mikononi mwa Mungu, akasonga mbele haraka sana katika utakatifu, akitumia muda wake katika kusali na kufanya tafakari.Mtakatifu Getruda alikuwa mmonaki katika maisha yake.Mtakatifu Getruda anatambuliwa na Kanisa Katoliki kuwa mtakatifu kama bikira ambapo hukumbukwa kila mwaka tarehe 16 Novemba.

Sala ya Mtakatifu Gertrudi wa Thuringia
Mungu, unayestahili upendo usio na mipaka, sina chochote cha kupimia vema ukuu wako, lakini hamu yangu kwako ni hivi kwamba, kama ningekuwa na yale yote uliyonayo wewe, ningekupa yote kwa furaha na shukrani.

Kwa ajili ya uongofu nakutolea, Baba mpenzi sana, mateso yote ya Mwanao mpendwa sana tangu wakati ule ambapo, akilazwa horini juu ya nyasi, alianza kulia, halafu akavumilia mahitaji ya utoto, mapungufu ya ubalehe, mateso ya ujana, hadi alipoinamisha kichwa akafa msalabani kwa mlio mkubwa.
Vilevile, kwa kufidia makosa yangu ya uzembe, nakutolea, Baba mpenzi sana, mwendo wote wa maisha matakatifu sana ambayo Mwanao pekee aliyaishi kikamilifu kabisa katika mawazo, maneno na matendo yake tangu atumwe kutoka ukuu wa kiti chako cha enzi kuja katika dunia yetu, hadi alipouonyesha mtazamo wako wa Kibaba utukufu wa mwili wake mshindi.
Kama shukrani nazama katika kilindi kirefu sana cha unyenyekevu, na pamoja na huruma yako isiyolipika, nasifu na kuabudu wema wako mtamu sana.
Wewe, Baba wa huruma, nilipokuwa ninapoteza maisha yangu hivyo, ulikuza kwangu mawazo ya amani, si ya mabaya, ukaamua kuniinua kwa wingi na ukuu wa fadhili zako.
Kati ya mengine, ulitaka kunijalia ujirani usiothaminika wa urafiki wako kwa kunifungulia kwa namna mbalimbali hazina ile azizi sana ya umungu, ambayo ni moyo wako wa Kimungu, na kwa kunitolea kwa wingi mkubwa kila utajiri wa furaha ndani yake.

for more 

Saint Gertrude the Great - Mary Pages


No comments:

Post a Comment