Tuesday, November 21, 2017

Sala ya Mama Mjamzito kwa Mtakatifu Gerald Majella(16Oktoba)

Related image
Mtawa wa nje aliyekuwa na ibada sana ya Ekaristi Takatifu Msimamizi Wamama wajawazito.
Mtakatifu Gerald mtumishi mpendwa wa Yesu Kristu, mfano wa Mkombozi wetu kwa fadhila yako ya unyenyekevu na unyofu;
pia mwana mpenziwa Mama wa Mungu, dondokeza moyoni mwangu angalau kijicheche tu cha Moto wa upendo wa KiMungu,uliotawala mno na kuwaka ndani mwako.

Mtakatifu8 Gerald, mwenye sifa,Mungu amekuteua na kukuweka mlinzi na msimamizi wa kina mama wanaotazamia kujifungua.

Naomba unilinde na unisimamie ili saa yangu ya kujifungua ifikapo mambo yote yawe salama kabisa. Kwa kushirikiana na Mtakatifu Maria Magdalena na kusimamiwa na Mama Bikira Mariaunisimamie na kunijalia nijifungue kwa njia za kawaida tu na bila matatizo wala kuingiliwa na ibilisi mwovu.

Nakukabidhi na mtoto atakayezaliwa ili afike salama duniani na mapema iwezekanavyo azaliwe pia upya kwa maji na RohoMtakatifu, kwa njia ya Sakramentiya Ubatizo AMINA

soma hapa;

Saint Gerard Majella - The Redemptorists


Maisha ya Mtakatifu Camillius

Image of St. Camillus de Lellis
Mtakatifu Camillius, alizaliwa mwaka 1550, May 25,huko Bucchianico, Chieti , Napoli - Italia. Mama yake alikufa mwaka 1562.Familia yake haikumjali , hivyo alivyofikisha miaka 16, alijiunga na jeshi ambalo muda huo lilikuwa vitani na Waturuki .Mwaka 1575 alitoka jeshini, na kuanza kufanya kibarua katika kituo cha watawa wa Capuchin, mjini Manfredonia. Alipata shida kutokana na jeraha alilopata jeshini - vitani, ambalo halikupona.Baada ya majaribu kadhaa, alijiunga na wa Capuchin.
Akaenda Roma, ambako alifanya kazi katika hospitali ya mtakatifu James, ambayo ilishughulikia magonjwa sugu. Akafanya kazi katika ngazi mbalimbali, mpaka kufikia ukurugenzi. Muda huo wote alifuata kila taratibu,kulingana na wa Capuchin walivyopaswa kuishi . Kiongozi wake wa kiroho alikuwa Philip Neri. Hapo akaudumia maskini na kuwa kuwasaidia katika mambo mbalimbali.
Akaenda kusoma seminari na Mwaka 1584,katika sikukuu ya Pentekoste, alipata daraja la upadri. Akaanzisha shirika la Wa Camillians.
Mwaka 1591, shirika lilikubaliwa na Papa Gregory XIV, na mwaka huo 1591- 1605 watawa wa shirika lake Walienda kuhudumia majeruhi ,wanajeshi huko Hungary na Croatia.
Mtakatifu Camillius alikufa mwaka 1614, July 14, huko Roma, Italia.Akatangazwa mwenye heri mwaka 1742 na Papa Benedict XIV , na akatangazwa mtakatifu mwaka 1746 na Papa Benedict XIV.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Kateri Tekakwitha
Mt. Cyrus wa Carthage
Mt. Heraclas
M/h. Humbert of Romans
M/h. Humbert
Mt. Justus
Mt. Libert
Mt. Nicodemus wa mlima mtakatifu
Mt. Optatian
Mt. Procopius
M/h. Richard Langhorne
Mt. Ulrich
Mt. William Breteuil
Read more

St. Camillus de Lellis - Saints & Angels - Catholic Online

Maisha ya Mtakatifu Pambo

Mtakatifu Pambo , alikuwa mwanafunzi wa mtakatifu Antony mkuu.Aliishi katika jangwa la Nitrian, na huko alianzisha nyumba nyingi za watawa.
Alikuwa mwenye busara mno, na watu wengi walimfuata kumwomba ushauri, wakiwemo ,mtakatifu Athanasius, mtakatifu Melanie, na mtakatifu Rufinus.
Mtakatifu Pambo, alijifunza mengi kutoka kwa mtakatifu Antony. Ndio ikawa dira ya maisha yake.Alijitolea katika kazi za Mungu, akijitahidi kuishi kwa haki.
Mtakatifu Pambo, alikufa mwaka 375, kwa amani.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Watawa wa Carmelite wa Compiegne
Mt. Acllinus
Mt. Alexis
Mt. Andrew Zorard
Mt. Ansueris
M/h. Antoinette Roussel
M/h. Ceslaus
Mt. Charbel
Mt. Clement wa Okhrida
Mt. Cynllo
Mt. Ennodius
Mt. Felix wa Pavia
M/h. Frances Brideau
Mt. Frances de Croissy
Mt. Fredegand
Mt. Generosus
Mt. Hedwig wa Poland
Mt. Hyacinth
M/h. Juliette Verolot
Mt. Kenelm
Mt. Madeleine Brideau
Mt. Madeleine Lidoine
Mt. Marcellina
Mt. Marie Claude Brard
Mt. Marie Croissy
Mt. Marie Dufour
Mt. Marie Hanisset
Mt. Marie Meunier
Mt. Marie Trezelle
Mashahidi wa Scillitan
Mt. Nerses Lambronazi
Wt. Nicholas, Alexandra, na wenzao
M/h. Pavol Peter Gojdi
M/h. Rose Chretien
Mt. Theodosius
Mt. Theodota
Mt. Turninus

Maisha ya Mtakatifu Maria Magdalena

Image result for Life of Saint Maria Magdalena
Mtakatifu Maria Magdalena, alizaliwa huko Magdala, Galilaya. Tunaona katika kukutana kwake na Bwana Yesu alitolewa mapepo 7 (Lk 8: 2)
Katika Maandiko tunaona pia kuwa alikuwa mmoja wa wanawake walioshuhudia kaburi tupu, baada ya ufufuko wa Bwana Yesu. (Yn 20: 1-2)
Na katika maandiko tena ( Yn 20 :11-18) tunaona jinsi Bwana Yesu alivyojidhihirisha kwa Maria Magdalena.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Alberic Crescitelli
Mt. Dabius
Mt. Joseph wa Palestine
Mt. Meneleus
Mt. Movean
Mt. Pancharius
Wt. Philip Evans na John Lloyd Mashahidi
Mt. Plato
Mt. Theophilus
Mt. Wandrille
Read More

St. Mary Magdalene - Saints & Angels - Catholic Online

Maisha ya Mtakatifu Simeon Salus

Mtakatifu Simeon Salus alizaliwa mwaka 522 huko Misri. Alienda kuhiji nchi takatifu, huko Jerusalem .Aliporudi alikaa jangwani, karibu na bahari nyekundu.Huko alikaa miaka 29,katika maisha ya uchaji, na majitoleo.Alipoondoka hapo alienda katika mji ulioitwa Emesus, ambapo alikaa miaka 7.Mwaka 588 mji huo uliteketezwa na tetemeko la ardhi.
Mtakatifu Simeon Salus alikufa na kuzikwa katika makaburi ya watu maskini katika mji huo wa Emesus
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. John Boste
Mt. Declan
Mt. Dictinus
Mt. Godo
M/h. Joseph Fernandez
Mt. Kinga wa Poland
Mt. Kundegunda
Mt. Lewina
M/h. Maria Angeles wa mtakatifu Joseph
M/h. Maria Mercedes Prat
M/h. Maria Pilar Martinez Garcia na wenzake
Mt. Menefrida
Wt. Meneus na Capito
M/h. Modestino wa Yesu na Maria
M/h. Niceforo wa Yesu na Maria
Wt. Niceta na Aquilina
Mt. Ursicinus
Wt. Victor, Stercntius, na Antigones
Mt. Vincent
Wt. Wulfhade na Ruffinus

Heshima ya Mtakatifu Yosefu Baba Mlishi wa Yesu

Image may contain: one or more people
SALA KWA MTAKATIFU YOSEFU.
Ee Yosefu mwenye heri, tunakimbilia kwako, katika masumbuko yetu, na kisha omba shime ya Mchumba wako Mtakatifu, tunaomba pia kwa matumaini usimamizi wako. Kwa ajili ya mapendo uliyompenda nayo Bikira Mtakatifu, Mzazi wa Mungu, na kwa ajili ya tunza ya Baba, uliyomtunza nayo Mtoto Yesu.
Tunakuomba sana, utuangalie kwa wema, sisi tuliokuwa fungu lake Yesu Kristo, tuliokombolewa kwa damu yake, utusimamie katika masumbuko yetu, kwa enzi na shime yako.
Ee Mlinzi amini wa Jamaa Takatifu, uwakinge watoto wateule wa Yesu Kristo, ee Baba uliyetupenda mno, utuepusha na kilema chochote cha madanganyo na upotevu.
Ee kinga yetu mwezaji,utusimamie huko juu mbinguni ulipo, tunaposhindana na wenye nguvu wakaao gizani. Kama vile siku za kale ukamwokoa Mtoto Yesu katika hatari ya kuuawa, na leo hivi, ulikinge Kanisa Takatifu la Mungu katika mitego ya adui, na katika shida yote.
Mtunze daima kila mmoja wetu, tupate mfano wako, tusaidie kwa msaada wako, kukaa na utakatifu maisha, kufa kifo chema, na kupokelewa mbinguni makao ya raha milele. Amina.

Maisha ya Mtakatifu Yohana mbatizaj

Yohana mbatizaji alikuwa mwana wa Mtakatifu Zakaria kuhani na mkewe , Mtakatifu Elizabeth (Luka 1: 5-25) .
Hizo zilikuwa nyakati ambapo Herode, akiwa mtawala mdogo wa Galilaya, chini ya dola ya Warumi . Herode alimkamata Yohana na kumuweka jela, kwa kuwa Yohana alimkemea na kumsema wazi wazi kutokana kitendo cha Herode kumuacha mkewe, aliyeitwa Phasaelis ( binti wa Mfalme Aretas wa Nabataea, sasa Jordan ) na kumuoa Herodia ambaye alikuwa mke wa nduguye (Herode Philip I) .
Herodia alimchukia Yohana, kwa kuwa alikuwa akikosoa jambo hilo, bila kificho. Herodia kwake aliona fahari kuolewa na Herode.
Herodia alikuwa na binti aliyemzaa katika ndoa yake ya awali aliyeitwa Salome.
Mfalme Herode alipoandaa sherehe kubwa ya kukumbuka kuzaliwa kwake, alialika wageni wengi na katika sherehe hiyo, binti wa Herodia (Salome) alicheza vizuri mno mbele za Mfalme na wageni. Mfalme akaamua kumpa zawadi, akamwambia Salome aombe chochote naye angempa. Binti yule aliamua kumuuliza mama yake, kitu gani aombe kwa mfalme.
Herodia akamwambia aombe kichwa cha Yohana Mbatizaji, ili kusudi aendelee kuishi kwa raha.
Mfalme Herode alipoambiwa kuwa yule binti ameomba kichwa cha Yohana Mbatizaji, alipata wakati mgumu mno, lakini kwa kuwa alikwisha ahidi kwa kiapo kuwa chochote kile akitakacho atampa, basi hakuwa na njia nyingine, akaamuru Yohana Mbatizaji akatwe kichwa na aletewe yule binti.
Ndipo, Yohana mbatizaji akakatwa kichwa na kikawekwa katika sinia, na kupelekwa kwa binti wa Herodia. ( Mathayo 14:1-12 )
Wanafunzi wa Yohana Mbatizaji, waliuchukua mwili wake, wakauzika huko Sabaste (sasa Nablus -West Banks).
Herodia akakizika kichwa cha Yohana Mbatizaji kwa kificho. Lakini mwanamke mmoja ambaye aliitwa Joanna, aliyekuwa mke wa mmoja wa watumishi katika kasri ya Herode alimuona. Akachukua kichwa hicho na kukizika katika mlima wa mizeituni.
Maajabu mengi yalitokea yakipelekea kugunduliwa mahali kichwa hicho kilipozikwa, na mwisho mabaki ya kichwa hicho kupelekwa katika kanisa la San Silvestro huko Roma Italia.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Sabina
Mt. Adelphus
Mt. Basilla
Mt. Candida
Mt. Edwold
Mt. Euthymius
Wt. Hypatius na Andrew
Mt. Medericus
Wat. Nicaeas na Paul
Mh. Richard Herst
Mt. Sebbi
Mt. Velleicus

Maisha ya Mtakatifu Donatian

Mtakatifu Donatian, na wenzake, maaskofu wa Tunisia na Algeria, waliuwawa na Mfalme Hunneric wa himaya ya Vandal (Mauritania, Sudan, Tunisia na Algeria) mwaka 484. Mfalme huyo aliwaua maaskofu hao, baada ya kukataa kufunga makanisa, kwa amri yake.
Baada ya mateso makali, Askofu Donatian na wenzake, waliachwa jangwani, ambapo walikufa kwa majeraha, kiu na njaa.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Eleutherius
Mt. Arator
Mt. Cagnoald
Mt. Chainaldus
Wt. Cottidus, Eugene, na wenzao
Mt. Dionysius
Mt. Faustus
Wt. Felix na Augebert
Mt. Maccallin
Mt. Magnus
Mt. Onesiphorus
Mt. Petronius
M/h. Thomas Tsughi

Maisha ya Mtakatifu Rosalia


Mtakatifu Rosalia alizaliwa huko Palermo, Sicily mwaka 1130. Baba yake aliitwa Sinibald na mama yake aliitwa Quisquina.
Akiwa bado kijana, aliamua kuondoka nyumbani kwao, na kwenda kuishi katika pango la mlima Pellegrino .Aliandika katika ukuta wa pango, " Mimi, Rosalia, binti wa Sinibald na Quisquina, nimeamua kuishi katika pango hili, kwa mapenzi yangu, kwa Bwana wangu ,Yesu Kristo".
Alikaa katika pango hilo mpaka alipokufa mwaka 1166, huko Pellegrino, Sicily.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Caletricus
Mt. Candida
M/h. Dina Belanger
Mt. Hermione
Mt. Magnus
Mt. Marinus
Mt. Monessa
Mt. Rhuddlad
Wt. Rufinus, Silvanus, na Victalicus
Mt. Salvinus
Mt. Thamel na wenzake
Mt. Theodore
Mt. Ultan wa Ardbraccan
Read more

Saint Rosalie - Best of Sicily Magazine

Maisha ya Mtakatifu Lawrence Giustiniani

Image result for Life of saint Lawrence Giustiniani
Mtakatifu Lawrence alizaliwa tarehe 1 Julai 1381, huko Venice, Italia. Alizaliwa katika familia maarufu, ambayo ilishakuwa na watakatifu kadhaa.
Mwaka 1404 alipata daraja la ushemasi, na akajiunga na shirika la mapadri katika kisiwa cha San Giorgio, huko Alga. Mwaka 1407, alipata daraja la upadri na shirika alilokuwemo likaanza kufuata taratibu za mtakatifu Augustine.
Kwa jinsi alivyokuwa na maisha halisi ya kumcha Mungu, alikubalika mno katika jumuia yake. Akachaguliwa kuwa mkuu wa kwanza katika Jumuiya yake. Akasaidia kubadili baadhi ya vipengere katika miongozo ya shirika. Akachaguliwa kuwa mkuu wa shirika.
Mwaka 1433, Papa Eugene IV, ambaye alikuwa mmoja wa waanzilishi wa shirika San Giorgio, alimtangaza Lawrence Gustiniani kuwa Askofu wa Castello. Katika Castello, alifanya pia mabadiliko yaliyoleta ufanisi na maendeleo.
Mwaka 1451, Papa Nicholas V, aliunganisha jimbo la Castello na Grado, akaanzisha jimbo la Venice. Hivyo mtakatifu Lawrence akawa Askofu wa kwanza wa Venice.
Katika nyakati hizo, kukatokea mji wa Constantinople kutekwa na majeshi ya waislam.Watu wa Venice walipata mashaka makubwa, kwa kuwa walikuwa wakifanya biashara na Constantinople. Lakini Askofu Lawrence, aliwatuliza, akajadiliana na watawala jinsi ya kulikabili tatizo hilo.
Mtakatifu Lawrence alikufa mwaka 1456, Januari 8, huko Venice. Akatangazwa Mwenyeheri mwaka 1524, akatangazwa mtakatifu Oktoba16, 1690 na Papa Alexander VIII.

St. Lawrence Giustiniani - Saints & Angels - Catholic Online


*Watakatifu wengine wa leo*
Mt.Teresa wa Calcutta
Mt. Alvitus
Mt. Bertin
Mt. Bertinus
Mt. Charbel
Mt. Eudoxius
Mt. Herculanils
Mt. Joseph Canh Luang Hoang
Mt. Obdulia
Mt. Peter Tu
Mt. Quintius
Mt. Romulus
Mt. Victorinus
M/h. William Browne

Maisha ya Mtakatifu Cloud

Mtakatifu Cloud, alizaliwa mwaka 522 huko Paris, Ufaransa. Baba yake alikuwa mfalme Clodomir. Mfalme huyo aliuwawa katika vita na binamu yake, aliyeitwa Gondomar, akiacha ufalme kwa wanawe watatu, Cloud akiwa mdogo . Bibi yao (mtakatifu Clotilda) aliwachukua watoto hao, kusudi wasome.
Wakati mtakatifu Cloud akiwa na miaka 8 tu, baba yake aliyeitwa Childebert na kaka yake, waliamua kumuua Cloud na kaka zake, ili wagawane ufalme wao.
Walifanikiwa kuwauwa kaka wawili Theodoald na Gunther . Mtakatifu Cloud, alifanikiwa kukimbia .
Huko mafichoni Mtakatifu Cloud, aliamua kuacha mambo ya dunia na kumtumikia Mungu.
Akagawa vichache alivyokuwa navyo, akaamua kumfuata mtawa aliyeitwa Severinus.
Akawa mtiifu akiishi maisha ya kawaida, lakini watu wakamjua, na baba yake mdogo pia anajua. Lakini baba huyo hakumjali tena kwa kuwa alijua kuwa ameamua kumtumikia Mungu.
Mwaka 551, akapewa daraja la upadri na Askofu Eusebius wa Paris. Lakini kwa kuogopa umaarufu aliamua kwenda kuishi katika mji ulioitwa Nogent (Saint Cloud sasa) .
Hapo Nogent, alijenga makao ya watawa, ambako alipokea watu, walioamua kuacha mambo ya dunia, kumfuata Mungu. Watawa hao, walimchagua mtakatifu Cloud kuwa kiongozi wao.
Mtakatifu Cloud aliwaonyesha mfano wa maisha masafi na ya uaminifu, mpaka alipokufa mwaka 560 , katika mji wa Nogent-sur-Seine , Ufaransa.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Alcmund
Mt. Anastasius
Mt. Augustalus
Mt. Carissima
Mt. Diuma
M/h. Eugenia Picco
Mt. Eupsychius
Mt. Eustace
Mt. Eustace
Mt. Evortius
Mt. Faciolus
Mt. Gratus
Mt. Grimonia
Mt. Hilduard
M/h. John Duckett
M/h. John Maid
Mt. John wa Lodi
Mt. John wa Nicomedia
M/h. Louis Maki
Mt. Madalberta
Mt. Marko Krizin
Mt. Memorius
Mt. Pamphilus
M/h. Ralph Corby
Mt. Regina
Mt. Regina
Mt. Tilbert

Watakatifu Andrea Kim na Wenzake,Mashahidi

Watakatifu Andrea Kim na Wenzake,Mashahidi*
Uinjilishaji katika nchi ya Korea, ulianza katika karne ya 17, kupitia kwa kikundi cha walei.Kikundi hicho kilifanya kazi hiyo mpaka wamisionari kutoka Ufaransa walipofika.
Katika miaka ya 1839,1866 na 1867, wakristo waamini wapatao 103, walipoteza maisha , kwa kushikiria imani zao. Kati yao walikuwepo Padri wa kwanza Mkorea Andrew Kim Taegon, kiongozi wa walei Paul Chong Hasang .
Pamoja nao walikuwemo pia Maaskofu na mapadre , pamoja na walei, ambao walimwaga damu zao , kutetea imani.
Walitangazwa wenye heri mwaka 1925
Papa John Paul II, aliwatangaza kuwa watakatifu, tarehe 6 May 1984, alipotembelea Korea
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Agatha Chon Kyonghyob
Mt. Agatha Kim
Mt. Agatha Yi
Mt. Agatha Yi Kannan
Mt. Agatha Yi Kyong-i
Mt. Agatha Yi Sosa
Mt. Anna Kim
Mt. Candida
Mt. Cecilia Yu
Mt. Dionysius
Mt. Eusebia
Mt. Eustace
Mt. Eustachius
Mt. Fausta and Evilasius
Mt. John Charles Cornay
Mt. Jose Maria de Yermo y Parres
Mt. Lawrence Imbert
Mt. Lucia Park Huisun
Mt. Magalena Ho Kye-im
Mt. Martha Kim
Mt. Paul Chong Hasang
Mt. Agapitus
Mt. Susanna U Surim
Mt. Teresa Yi Mae-im
Wt. Theodore, Philippa, na wenzao
M/h. Thomas Johnson
Mt. Thomas Son Chason
Mt. Vincent Madelgarus

Maisha ya Mtakatifu Januarius

Mtakatifu Januarius alizaliwa katika mji wa Benevento huko Italia, katika familia ya kitajiri.
Akiwa na miaka 15 tu alipata daraja la upadri, na akafanya kazi katika parokia ya Benevento. Muda huo kulikuwa na wapagani wengi katika mji huo.
Akiwa na miaka 20, alipata daraja la Uaskofu na kuwa Askofu wa Naples. Katika muda huo, mfalme Diocletian, ambaye alikuwa mpinga Kristo alitawala. Mfalme huyo aliendesha madhulumu kwa wakristo, akiwakamata, kuwafunga na kuwauwa.
Mtakatifu Januarius, aliwaficha baadhi ya wakristo, na kuwaepusha na mateso. Lakini rafiki yake alikamatwa. Huyo alikuwa Mtakatifu Sissou.
Mtakatifu Januarius, aliamua kwenda kumtembelea gerezani, naye pia akakamatwa. Mfalme akaamuru wauwawe kwa kutupwa kati ya wanyama wakali, katika uwanja huko Pozzuoli.
Lakini kwa kuogopa fujo kutoka kwa watu wa mji ule, hukumu ikabadilishwa. Ikatakiwa auwawe kwa kukatwa kichwa.
Mtakatifu Januarius, aliuwawa kwa kukatwa kichwa, katika kreta ya Solfatara, karibu na mji wa Pozzuoli. Ilikuwa mwaka 305.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mh. Alphonsus de Orozco
Mt. Arnulf
Mt. Emily de Rodat
Mt. Eustochins
Mt. Goeric wa Metz
Mt. Maria de Cerevellon
Mt. Peleus
Mt. Pomposa
Mt. Sequanus
Mt. Theodore of Tarsus
Mh. Thomas Akafuji
Mt. Trophimus

Maisha ya Mtakatifu Ignatius


Mtakatifu Ignatius, alizaliwa mwaka 35, huko Syiria. Alizaliwa katika familia isiyo kuwa ya kikristo. Lakini akiwa na umri mdogo, aliamini na kuwa mkristo.
Mtakatifu Ignatius, alikuwa mwanafunzi wa Mtume Yohana. Na baadae mwaka 69, alichaguliwa kuwa Askofu wa Antiokia ( Uturuki ).
Askofu Ignatius, alionyesha mwelekeo wa utakatifu tokea mwanzo. Alisimamia mafundisho ya kweli na kuelekeza njia sahihi kwa wakristo.
Mwaka 107, Mfalme Trajan ambaye alikuwa mkatili na mpinga Kristo, alianza kutawala katika dola ya Warumi.
Mfalme huyo, alimuhukumu kifo Askofu Ignatius, kwa sababu aliendelea kuikiri na kuifundisha imani ya kanisa. Askofu Ignatius alikataa kuikana imani yake.
Hivyo basi, alichukuliwa na askari, kupelekwa Roma, ili akatupwe na kuraruliwa na wanyama wakali, huku watu wakishuhudia.
Safari ya kwenda Roma ilikuwa ndefu, iliyochukua siku nyingi. Hivyo basi, Askofu huyo shujaa, alitumia muda huo, kuandika barua saba, za kuwatia moyo, na kuwaelekeza wakristo, katika sehemu mbalimbali.
Mwaka 108, baada tu ya kufika Roma, mtakatifu Ignatius, aliuwawa kwa kutupwa kati ya simba wenye njaa. Mabaki yake yalichukuliwa na waamini wengine mpaka Antiokia na kuzikwa nje ya mji .
Alipotawala mfalme Theodosius II, aliamuru mabaki hayo kuzikwa upya sehemu iliyoitwa Tychaeum, ambako kulikuwa na hekalu. Hekalu hilo baadae liliwekwa wakfu, kuwa kanisa kwa heshima ya mtakatifu Ignatius.
Mwaka 637, mabaki hayo yalipelekwa Rome na kuzikwa katika Basilica di San Clemente.
Mtakatifu Ignatius, Askofu na shahidi, Utuombee!!!
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Anstrudis
Mt. Berarius
Wt. Ethelbert na Etheired
Mt. Florentius
Mt. Francis Isidore Gagelin
Mt. Francois Gagelin
Mt. Herodion
Wh. Jane Louise Barre na Jane Reine Prin
Mt. John
Mt. Louthiem
Mt. Mamelta
Mt. Marie Magdalen Desjardin
Mt. Nothlem
Mt. Regulus
Mt. Richard Gwyn
Mt. Rudolph wa Gubbio
Wat. Victor, Alexander, na Marianus

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kuuishi utakatifu

HISTORIA FUPI YA MWALIMU NYERERE
MPAKA MAUTI YALIPOMFIKA;Kama nilivyoinukuu kutoka https://www.jamiiforums.com

Tarehe ya kuzaliwa 13 Aprili 1922
Mahali pa kuzaliwa Butiama
Tarehe ya kifo 14 Oktoba 1999
Rais wa Tanzania
Alingia ofisini 1964
Aliondoka ofisini 1985
Alitanguliwa na (alikuwa rais wa kwanza)
Alifuatwa na Ali Hassan Mwinyi
Dini Mkristo Mkatoliki
Elimu yake Chuo Kikuu cha Edinburgh - Uskoti Digrii
anazoshika M.A. ya historia na uchumi
Kazi mwalimu, mwanasiasa Mengine Nyerere alikuwa
mwenyekiti wa chama cha TANU na baadaye wa CCM.
Mara nyingi aliitwa "Mwalimu Nyerere".
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa rais wa
kwanza wa Tanzania. Alizaliwa Butiama, mkoani Mara
pembezoni mwa Ziwa Nyanza tarehe 13 Aprili, 1922.
Alifariki dunia 14 Oktoba, 1999. Aliiongoza Tanzania toka
mwaka 1961 hadi mwaka 1985.
Yeye ni mwasisi wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea.
Kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa ni mwalimu. Kazi
hii ndiyo ilimpatia jina ambalo lilimkaa maisha yake yote la
"Mwalimu." Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi wachache
wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiyari baada
ya kutawala kwa muda mrefu. Alipostaafu urais mwaka
1985 alirudi kijijini kwake Butiama ambako aliendesha
shughuli za kilimo. Aliendelea kuwa na athari kubwa
katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.
Maisha Ya Mwalimu
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922
( katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa
Mara, Tanzania (wakati ule: Tanganyika). Alikuwa
mojawapo kati watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa
kabila la Wazanaki. Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga
mifugo ya babake; katika umri wa miaka 12 aliingia shule
akitembea kilomita 30 hadi Musoma. Baada ya kumaliza
shule ya msingi aliendelea kusoma shule ya wamisionari
Wakatoliki huko Tabora. Katika umri wa miaka 20
alibatizwa akawa mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa
maisha yake.
Mapadre wakaona akili yake wakamsaidia kusoma ualimu
huko Makerere, Kampala, Uganda kuanzia 1943 - 1945.
Makerere akaanzisha tawi la Umoja wa wanafunzi
Watanganyika pia amejihusisha na tawi la Tanganyika
African Association (TAA). Baada ya kumaliza masomo ya
ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya St.Mary´s.
Mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma
kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Uskoti /Uingereza
akasoma M.A. ya historia na uchumi(alikuwa mtanzania
wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na
mtanzania wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya
Tanzania).
Aliporejea Tanganyika kutoka masomoni, Nyerere
alifundisha Historia, Kingereza na Kiswahili katika shule ya
St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam. Mwaka 1953
alichaguliwa kuwa raisi wa chama cha Tanganyika African
Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga
alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere.
Mwaka 1954 alikibadilisha chama cha TAA kwenda katika
chama cha Tanganyika African National Union (TANU)
ambacho kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya
mwaka mmoja chama cha TANU kilikuwa tayari chama cha
siasa kinachoongoza Tanganyika.
Uwezo wa mwl. Nyerere uliwashitua uongozi wa kikoloni
na kumlazimisha Nyerere kuchagua kati ya siasa na kazi
ya ualimu. Nyerere alisikika akisema kuwa alikuwa
mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati
mbaya. Alijiuzuru ualimu na kuzunguka nchini Tanganyika
kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta
muungano katika mapigano ya uhuru. Pia alizungumza
kwa niaba ya TANU katika Trusteeship council na Fourth
committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York.
Uwezo wake wa kimaongezi na kuunganisha watu
ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila
umwagaji wa damu. Ushirikiano mzuri aliouonyesha
aliyekuwa gavana wa wakati huo bwana Richard Turnbull
ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru. Nyerere
aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na
kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960. Mwaka 1961
Tanganyika ilipata uhuru wake na tarehe 9/12/1961
Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika
huru na mwaka mmoja baadae Nyerere alikuwa raisi wa
kwanza wa jamhuri ya Tanganyika. Nyerere alikuwa kiungo
muhimu katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar
kutengeneza Tanzania baada ya mapinduzi ya Zanzibar
mwaka 1964 yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar
Jamshid bin Abdullah.
Sifa zake
Bado anakumbukwa na watanzania hasa wa hali ya chini
kutokana na sera zake za kujali utu na ubinadamu.Pia
ataendelea kukumbukwa na waafrika kote barani hasa kwa
mchango wake mkubwa wakati wa harakati za kupigania
uhuru katika nchi mbali mbali barani Afrika.
Ni mmoja wa viongozi wachache wanaokumbukwa kwa
kutojilimbikizia mali pamoja na kutawala kwa miaka zaidi
ya 24.
Mwishoni mwa maisha yake Nyerere aliishi kama mkulima
wa kawaida kijijini kwake Butiama. Alipatwa na kansa ya
damu (leukemia) na kufariki Uingereza wakati wa kutibiwa
katika mji wa London tarehe 14 Oktoba, 1999. Alizikwa
mahali pa kuzaliwa kwake, kijiji cha Butiama.
Machapisho ya mwl.Julius K. Nyerere.
• Freedom and Socialism.Mkusanyiko wa maandiko na
hotuba, 1965-1967 (1968)
• Freedom & Development, Uhuru Na Maendeleo (1974)
• Ujamaa - Essays on Socialism' (1977)
• Crusade for Liberation (1979)
Image result for maisha ya mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Mtazamo wangu kuhusu Mwalimu Julius Nyerere
Mwalimu katika kuishi kwake alitekeleza mambo mengi yakiwa yanashaabiana katika kumpendeza Mungu kwakuwa alikuwa tiari kujitoa kwa ajili ya manufaa ya wengine na inaonesha angeliweza kujinufaisha lakini akufanya hivyo hakika kwa mambo aliyotenda anastaili kuwa mmoja wa Watakatifu siku moja.

Kikubwa nashauri tuzidi kumuombea ili siku moja Mwenyezi Mungu amfanye Mtakatifu na kumtumia katika maombi yetu siku zote

Maisha ya Mtakatifu Andrea Avelino Mtawa(Life of Saint Andrea Avelino)

Image of St. Andrew Avellino

Mtakatifu Andrea Avelino Mtawa alizaliwa mwaka 1521b huko Italia kwenye mji wa Castronuovo Jina lake la ubatizo ni  Lancelotto ambalo lilikuwa nje na upendo wa Msalaba na kwa kuwa alitamani kuupenda msalaba kama Mtakatifu Andrea aliamua kuchaguwa kupewa jina hilo.

Inasemekana alifanya kazi kubwa ya kuwahudumia watu kiroho kwa moyo wote ambapo matendo yake yalikuwa yanaudhihirishia jumuiya kuwa nguvu ya Mungu ilikuwa ndani yake.Mtakatifu Andrea Avelino ni msomi wa shahada ya sheria.Na kupitia hiyo elimu aliitumia kutoa haki katika maamuzi yake akiwa akiudumia kwenye maswala ya kikanisa baadae alikuja kupata daraja la upadri.

Mtakatifu Andrea Avelino alifariki tarehe 10 Novemba 1608 baada ya kuugua gafla ugonjwa wa Moyo akiwa kwenye maadhimisho ya Misa Takatifu .
Fundisho ninalojifunza Binafsi.Kuupenda msalaba kwa kuwa wokovu wetu umetokana na msalaba hasa baada ya kifo cha mkombozi wetu Yesu Kristu na pia mwanadamu anaweza kupata mabadiliko kutokana na historia ya watu wengine na zaidi kujifunza yaliyomema siku zote.
Read here more

St. Andrew Avellino - Saints & Angels - Catholic Online

Wednesday, November 15, 2017

Maisha ya Mtakatifu Mathayo


Mtakatifu Mathayo, alizaliwa katika karne ya 1, huko Galilaya. Alikuwa mwana wa Alpheus. Mtakatifu Mathayo alikuwa msomi katika lugha za Aramaic na Kigiriki.
Mtakatifu Mathayo, alifanya kazi ya kukusanya ushuru, chini ya serikali ya Warumi.
Alipoitwa na Bwana Yesu, watu walishangaa mno.Lakini alipofanya karamu na kumualika Bwana Yesu, waandishi na Mafarisayo walimshangaa Bwana, kwa kula na mwenye dhambi.Lakini Bwana Yesu aliwajibu kuwa yeye alikuja kwa ajiri ya wadhambi (Marko 2:17) .
Mtakatifu Mathayo, alishuhudia ufufuko wa Kristo na kupaa kwake mbinguni.Baada ya Pentekoste alianza kuhubiri katika Judea na baadae akaenda Hierapolis (Denizli Province,Turkey) ambako aliuwawa katika mwaka 74 ( baada ya Kristo )
Mabaki yake yapo Salerno , Italy.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Alexander
Wt. Chastan na Imbert
Mt. Eusebius
Mt. Francis Jaccard
Mt. Gerulph
Mt. Hieu
Mt. Maura Troyes
Mt. Meletius
Mt. Pamphilus
Mt. Thomas Dien

Maisha ya Mtakatifu Jerome

Image may contain: 1 person, text
Mtakatifu Jerome, alizaliwa Machi 27, 342 katika mji wa Stridon Dalmatiae (Croatia ). Akaitwa Eusebius Sophronius Hieronymus.
Akiwa na miaka 12, alisafiri kwenda Roma, kwa masomo, alijifunza uandishi, filosofia, kilatini na Kigiriki.
Mwaka 366, mtakatifu Jerome, aliamua kuwa mkristo, akabatizwa na Papa Liberius. Huko akaamua kusoma teolojia.
Mtakatifu Jetome alisafiri kwenda Tier, akifuatana na rafiki yake aliyeitwa Bonosus, kutafuta elimu zaidi. Katika safari zake, alienda katika manosteri ya Aquileia, Italia mwaka 370. Manosteri hiyo ilikuwa chini ya Askofu Valerian, ambaye alikuwa mwenye busara mno. Hapo, Mtakatifu Jerome akakutana pia na Rufinus na wakawa marafiki . Rufinus alijulikana kwa umahiri wake wa kutafsiri maandiko ya Kigiriki kwa kilatini.
Mtakatifu Jerome naye alikuwa na uwezo wa kutafsiri lugha tofauti pia.
Kutoka katika manosteri ya Aquileia, Mtakatifu Jerome alienda Treves, Gaul (Ufaransa ), ambako alitafsri vitabu mbalimbali kwa matumizi yake, akiwa na lengo la kuanzisha maktaba.
Mwaka 373, alirudi Aquileia, ambapo rafiki yake Bonosus aliamua kwenda kuishi pweke akitafakari makuu ya Mungu katika kisiwa cha Adriatic. Mtakatifu Jerome naye akasafiri kwenda Antiokia (Uturuki sasa), akipitia Athens (Ugiriki). Mwaka 374 mtakatifu Jerome alifika Antiokia, baada ya kusimama katika vituo mbalimbali. Akiwa huko alianza kuandika kitabu chake cha kwanza.
Mwaka huo huo, mtakatifu Jerome, aliugua ugonjwa uliosababisha vifo vya wenzake kadhaa. Wakati akitaabika na ugonjwa, alipata maono mbalimbali, ambayo yalimuimarisha mno katika imani. Baadae naye aliamua kwenda kuishi jangwani, akiwa peke yake, ambapo alikaa kwa miaka 4.
Japokuwa mtakatifu Jerome aliporudi toka jangwani, aliendelea kuwa mtawa, akikaa pweke na kutafakari maandiko, lakini mababa wa kanisa, pamoja na Papa Damasus, walitaka awe padri. Mtakatifu Jerome aliomba endapo atakuwa Padri, basi aruhusiwe kuendelea na maisha ya kitawa na nyakati zingine aruhusiwe kwenda kukaa mwenyewe. Hivyo mtakatifu Jerome, akapata daraja la upadri.
Akasafiri kwenda Constantinople (Istanbul Uturuki) ambako alienda kusoma kwa mtakatifu Gregory wa Nazianzus, ambaye alikuwa bingwa wa teolojia.
Mwaka 382, Mtakatifu Jerome aliondoka Constantinople kwenda Roma, huko alionana na Papa Damasus. Papa alimtaka akae pale na awe Katibu wake. Papa Damasus alikufa mwaka 384 na Mtakatifu Jerome akabaki hapo. Kutokana na misimamo yake ya ukweli, Mtakatifu Jerome akawa na maadui wengi na wakamtengenezea shutuma nyingi mbaya, na hivyo aliamua kuondoka Roma.
Mwaka 386 alikwenda Antiokia na akaondoka hapo na kikundi cha waamini kwenda nchi takatifu. Mtakatifu Jerome aliendelea kuandika mafundisho mbalimbali kuhusu mama Bikira Maria na kutafsiri biblia kutoka kihebrania kwenda kilatini.
Mtakatifu Jerome alikufa tarehe 30 Septemba 420, kwa amani huko Bethlehem, Israeli.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Enghenedl
Mt. Gregory
Mt. Honorius wa Canterbury
Mt. Laurus
Mt. Leopardus
Mt. Midan
Wat. Victor na Ursus

Mtakatifu John

Image may contain: 2 people, text
Mtakatifu John, alijifunza lugha yao,pamoja na desturi zao.Akawafundisha wamisionari wenzie lugha za wenyeji. Mwaka 1635 aliwabatiza wenyeji 14, mwaka uliofuata 86.
Mwaka 1649 , wenyeji ambao hawakupenda mabadiliko, waliwakamata mapadri ,wakachoma makazi yao.Mwaka huo huo mwezi March 16, walimuua mtakatifu John, na wenzake baada ya mateso makali.
Mtakatifu John Brebeuf alitangazwa mwenye heri mwaka 1925 na akatangazwa mtakatifu mwaka 1930 na Papa Pius XI
*Mtakatifu Isaac Jogues*
Mtakatifu Isaac Jogues alizaliwa mwaka 1607, Januari 10 huko Orleans, Ufaransa. Mwaka 1624, alijiunga na wa Jesuit huko Rouen.
Mtakatifu Isaac, aliweka nadhiri za kwanza mwaka 1626 na akaenda kusoma filosofia katika chuo cha La Fleche, na mwaka 1629, alirudi Rouen kufundisha vijana. Mwaka 1633 alienda tena kusoma katika College de Clermont huko Paris, akisoma teolojia. Na mwaka 1636, akapata daraja la upadri huko Clermont.
Mtakatifu Isaac, alivutiwa na wamisionari waliorudi Ufaransa, toka Quebec mwaka 1636, na akapangiwa kwenda nao tena kufanya uinjilishaji. Na Akapangiwa kwenda kuinjilisha katika kabila ya Huron. Alifika huko 2 Julai 1636.
Aliishi katika mji wa Ihonatiria kwa miaka 4, baadae kuanza kuzunguka katika vijiji kadhaa kwa miezi mingi .Huko walipokewa kwa u baridi mno, kutokana na wenyeji kutaka kuishi maisha yao, na kufuata dini zao za asili.
Mwaka 1652 August 3, mtakatifu Isaac na mapadri wengine, pamoja na kundi la wakristo wa Huron, walijikuta katikati ya mapigano makali ya kabila za wenyeji wenye uadui mkubwa.
Yeye alimudu kujificha katika shamba lililokuwa jirani, lakini alipoona wakristo wengi wamekamatwa , alijitokeza .Mtakatifu Isaac , aliteswa sana , na alishikiliwa mateka kwa muda wa miezi 10.Akarudi Ufaransa.
Mtakatifu Isaac, aliachiwa na akarudi Ufaransa. Lakini mwaka 1644, alirudi tena Quebec na mwaka 1646 alikwenda tena katika kabila ya Huron na akajaribu kuwa msuluhishi kati yao na kabila ya Mohawk.
Lakini tarehe 18 October 1646 watu wa kabila la Iroquois na Mohawk, walimuua mtakatifu Isaac na kuitupa maiti yake mtoni ,na kesho yake wakauwa Padri mwingine.
Isaac Jogues alitangazwa mwenye heri mwaka 1925 June 21 na Papa Pius XI na kutangazwa mtakatifu mwaka 1930 June 29 na Papa Pius XI.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
M/h. Agnes de Jesus Galand
Mt. Altinus
Mt. Anthony Daniel
Mt. Aquilinus
Mt. Beronicus
Mt. Charles Garnier
Mt. Cleopatra
Mt. Desiderius
Mt. Eadnot
Mt. Ethbin
Mt. Eusterius
Mt. Frideswide
Mt. Gabriel Lalement
Mt. John wa Rila
Mt. Laura
Mt. Lupus wa Soissons
Mt. Philip
Mt. Theofrid
Mt. Varus
Mt. Veranus wa Cavaillon

Maisha ya Mtakatifu Francis wa Borgia


Mtakatifu Francis wa Borgia, alizaliwa mwaka 1510 October 28, huko Ganda, Valencia, Hispania.
Baba yake aliitwa Juan Borgia mtawala wa Gandia.Mama yake aliitwa Juana .
Japokuwa Francis alikuwa na nia ya kuwa mtawa, lakini wazazi wake hawakupenda.Hivyo wazazi wake walimpeleka kufanya kazi , katika Ikulu ya mfalme Charles I wa Hispania. Akafanya kazi, akimsaidia mfalme katika shughuli mbalimbali.
Mwaka 1529,September, alimuoa Leonor de Castro Mello Meneses, ambaye alikuwa Mreno. Wakapata watoto 8.
Kuanzia mwaka 1539, mtakatifu Francis, alifanya kazi mbalimbali zilizomuongeza majukumu ya kiutawala.
Mwaka 1543, baada ya kifo cha baba yake, alirithi kazi ya baba yake, akawa mtawala wa Gandia. Alijaribu kupanga ndoa kati ya mwana wa mfalme Philip na binti wa mfalme wa Ureno, ambayo ilishindikana.
Jambo hilo lilichangia kuamua kwake kujiuzuru kazi za utawala na kurudi katika sehemu aliyozaliwa , ili kujitoa kwa utumishi wa Mungu.
Mwaka 1546, mke wake alikufa, na mtakatifu Francis, aliamua kujiunga na shirika la Wa Jesuit, ambalo lilikuwa limeanzishwa.
Mwaka 1551, aliacha mambo yote ya Dunia, akimwachia mwanae aliyeitwa Carlos de Borja, na akapata daraja la upadri.
Akazunguka sehemu mbalimbali, akifundisha na kuhubiri.Aliporudi kutoka Peru, alipata fununu ya kutaka kupewa madaraka makubwa na Papa.Akaenda kuishi katika mji wa Basque .
Lakini mwaka 1554, alikuwa mkuu wa wa Jesuit katika Hispania.Miaka 2 baadae akapewa jukumu la umishenari katika visiwa mbalimbali.
Mwaka 1565 , akachaguliwa kuwa kiongozi mkuu wa wa Jesuit. Kati ya mwaka 1565-1572, alifanya kazi nyingi na kufanikisha kuanzishwa kwa Collegio Romanum , ambapo baadae kilikuwa chuo kikuu cha Gregorian.
Mtakatifu Francis alikufa mwaka 1572, September 30 ,huko Roma.
Alitangazwa mwenye heri mwaka 1624 November 23, na Papa Urban VIII, na akatangazwa mtakatifu mwaka 1670 June 20, na Papa Clement X.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Aldericus
Mt. Cassius
Mt. Cerbonius
Mt. Daniel
Mt. Daniel Comboni
Wt. Eulampius na Eulampia
Mt. Fulk
Mt. Gercon
Mt. Gereon
Mt. Maharsapor
M/h. Mary Angela Truszkowska
Mt. Patricain
Mt. Paulinus wa Capua
Mt. Paulinus wa York
Mt. Pinytus
Mt. Tanca
Mt. Victor na wenzake

Maisha ya Mtakatifu John Gaulbert

Mtakatifu John Gaulbert, alizaliwa mwaka 985 ,huko Florence Italia. Alipata elimu nzuri katika shule za kikristo.Alikuwa na kaka yake aliyeitwa Hugo, ambaye aliuwawa na mtu ambaye, mtakatifu John ,alimfahamu .Akaamua kuwa atamtafuta mtu huyo,na kumuua, kulipa kisasi cha kifo cha Hugo.
Siku moja ya ijumaa kuu, mtakatifu John, akifuatana na wenzake, wakiwa na silaha,walikutana na mtu aliyemuua Hugo katika uchochoro mjini Florence. Akiwa amejiandaa kumuua, mtu yule,akiwa amekunja mikono yake kwa unyenyekevu, alimuomba mtakatifu John, asimuue ,kwa jina la Kristo, aliyesulubishwa siku ya ijumaa kuu.
Mtakatifu John, alimsamehe, akaenda katika kanisa hapo San miniato kusali.Hapo alikuta msalaba wa Kristo msulubiwa.
Mtakatifu John, akajiunga na watawa, wa Benedictine hapo San Miniato. Lakini kuna njia za kiimani, ambazo hukukubaliana na wakuu wake.Aliondoka hapo,akaenda Camaldoli.Baada ya muda akaondoka,akaenda Vallombrosa, ambako alianzisha nyumba ya watawa. Ardhi pale Vallombrosa ilikuwa kama jangwa wakati huo.Lakini aliamini pakipandwa miti, patakuwa Paz urithi. Kwa hiyo wakaanza taratibu kupanda miti na kutengeneza mazingira.Na sehemu hiyo ikawa nzuri mno.
Mtakatifu John Gaulbert alikufa mwaka 1073,huko Badia Passignano, Florence, Italia.
Alitangazwa mtakatifu mwaka 1193 na Papa Celestine III.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Agnes De
M/h. Andrew Oexner wa Riun
Mt. Ansbald
M/h. David Gonson
Mt Epiphania
Mt. Jason
Mt. John Jones
M/h. John Naisen
M/h. John Tanaka
Mt. John Iberian
Mt. John Wall
Mt. Leo wa Lucca
M/h. Louis Naisen
Mt. Marciana
M/h. Matthias Araki
Mt. Menulphus
M/h. Monica Naisen
Wt. Nabor na Felix
Mt. Paternian
Mt. Paulinus wa Antioch
Bl. Peter Araki Kobjoje
Mt. Peter Khanh
Mt. Veronica
Mt. Viventiolus

Maisha ya Mtakatifu John Eudes


Mtakatifu John Eudes, alizaliwa huko Ri,Normandy, Ufaransa mwaka 1601 November 14.Alijiunga na chuo cha wa Jesuit kilichokuwa Caen .Kinyume cha matarajio ya wazazi wake,ya kuoa, alijiunga na shirika la mapadri la Oratory mwaka 1623.Akasoma katika miji ya Paris na Aubervilliers, na mwaka 1625, akapata daraja la upadri.
Akafanya kazi kujitolea kusaidia waathirika wa mlipuko wa magonjwa yaliyotokea Ufaransa kati ya mwaka 1625-1631.Baada ya hapo, akashiriki katika kazi za kujenga makanisa,kuhubiri na kuungamisha .Akawa na shauku ya kusaidia wanawake walioanguka kiimani.
Mwaka 1641, akashirikiana na Madeleine Lamy, walianzisha nyumba kwa ajiri ya wanawake wa Caen. Mwaka 1643 alitoka katika Oratorians na kuanzisha shirika la Yesu na Maria (Eudists) hapo Caen.Lakini alipata mapingamizi yaliyosababisha asipate kibali toka kwa Papa.
Mwaka 1650, mtakatifu John Eudes, alipata mwaliko toka kwa Askofu wa Coutances, kuanzisha seminari katika jimbo hilo. Akaanzisha seminari katika Lisieux mwaka 1653 na Rouen mwaka 1659.Na pia katika miji ya Evreux mwaka 1666 na Rennes mwaka 1670.
Mtakatifu John Eudes, akashirikiana na mtakatifu Mary Margaret Alacoque heshima ya moyo mtakatifu wa Yesu, akaanza misa za moyo mtakatifu wa Yesu mwaka 1668 na moyo safi wa mama Maria.
Mtakatifu John Eudes alikufa mwaka 1680 August 19 huko Caen, Normandy (Ufaransa ).
Akatangazwa mwenye heri mwaka 1909 April 25 na Papa Pius X, na akatangazwa mtakatifu mwaka 1925 May 31 na Papa Pius XI.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Andrew
M/h. Anthony
Mt. Badulfus
M/h. Bartholomew Monfiore
Mt. Bertulf wa Bobbio
Mt. Calminius
Mt. Credan
Mt. Donatus
Mt. Elaphius
M/h. Emily Bicchieri
Mt. Ezequiel Moreno y Diaz
Mt. Guenninus
M/h. James Denshi
M/h. Joachim Firayama Diz
M/h. John Foyamon
M/h. John Nangata
Mt. John Yano
Mt. Julius
M/h. Lawrence Rokuyemon
M/h. Leo Suchiemon
M/h. Louis Flores
Mt. Louis wa Toulouse
Mt. Magnus wa Avignon
Mt. Marianus
Mt. Marinus
M/h. Michael Diaz
Mt. Mochta
Mt. Namadia
M/h. Paul Sanchiki
M/h. Peter Zuniga
Mt. Rufinus
Mt. Sebald
M/h. Thomas Koyanangi
Wt. Timothy, Thecla, na Agapius

Maisha ya Mtakatifu Monika


Image may contain: 2 people, people sitting
Mtakatifu Monika mwaka 331 huko Tagaste (Algeria). Tangu utoto wake alifundishwa kumtumikia Mungu na kujietenga na dhambi. Monika alizoea kwenda kusali peke yake kanisani, alikuwa akiwapenda maskini na aliwagawia chakula chake. Alipokua wazazi wake wakamwoza kwa kijana mmoja jina lake Patriki, naye ambaye alikuwa mtu wa ukoo bora, lakini hakuwa mkristu na mwepesi wa kukasirika. Monika alistahimili kwa upole alipogombezwa na mumewe. Alizaa watoto watatu na mmoja wao ndiye Augustino, Mwalimu wa Kanisa. Monika aliwafundisha kumpenda bwana wetu Yesu na kulitaja jina lake kwa heshima. Hata mume wake Patriki naye akaongoka akawa mkristu kwa sababu ya mwenendo safi wa Monika.
Augustino mwanawe alienda kukaa Kartago (Tunisia) ili asome shule, akaendelea katika maarifa yote, lakini alizidi kufanya uashereti na mambo yote yasiyofaa. Alimsikitisha sana mama yake. Monika alimwendea askofu mmoja wa huko akamuulizia. Itakuwaje na mwanangu? Naye askofu akamjibu “Usiogope mama, mtoto huyu wa machozi mengi hivi hawezi kuoptea”. Kweli Monika hakumwomba Mungu bure, maana Augustino aliongoka, akabatizwa na Mt. Ambrosi (taz 7 Desemba), akawa mwalimu shujaa wa mafundisho ya kanisa katoliki.
Monika alipojiona karibu kufa, aliwaambia wanawe: “Mnizike mpendavyo ila nawambeni kitu kimoja: Mnikumbuke kwenye altarehe ya Bwana”. Akafa huko Ostia (Italia) mwaka 387.
Sala ya Mama Mkristo kwa Maombezi ya Mt. Monika
Sala:
Mt. Monika, mwanamke na mama mwenye kuteseka, unajua machozi yangu, mahangaiko na uchungu wangu. Wakati fulani uliteseka kama mimi; naomba unionee huruma kwa mateso niliyonayo, Uniombee. Kutoka kwa Roho Mtakatifu ulipokea zawadi ya ufahamu na busara nguvu na sala. Uniombee ili nami nijaliwe zawadi zilezile. Kwa kuwa ulikuwa mpatanishi, daima uwaombee mume na watoto wangu na usali kwa ajili ya amani ya nyumba yetu.
Kwa maombezi yako uliwaokoa mumeo na mwanao. Utuombee neema ya Mungu ili tuwe na imani katika nyumba yetu. Kutokana na kuhudhuria Misa kila siku uliweza kupata nguvu na faraja; basi utuombee nasi nguvu na faraja katika maisha yetu daima. Utuombee kwa ajili ya mahitaji yetu muhimu ya kidunia; kusudi tuweze kufanya kazi na kuwa na amani katika familia yetu. Uwakumbuke watoto wangu, ili daima wajue pendo la kweli na hivyo wamtumikie Mungu kwa mapendo safi. Uniombee, ili niwe mama mwema kwao, na mwisho wa maisha haya, mimi pamoja na mume wangu, watoto wangu na wapendwa wangu wote tuweze kufika kwa Mungu, huko ambako wewe upo pamoja na mume wako na watoto wako wote. Kwa njia ya Kristo, Bwana wetu. Amina.
Mt. Monika, Mlinzi wa akina mama Wakristo. Utuombee.