Tuesday, November 14, 2017

Maisha ya Mtakatifu Wilfrid

Mtakatifu Wilfrid, alizaliwa Northumberland, mwaka 634. Alipata elimu yake Lindesfarne, kisha akaenda Lyons (Ufaransa ) na kisha Roma.
Mwaka 658 , alichaguliwa kuwa Abati wa Ripon, ambako alitambulisha sheria zilizotoka Roma.
Mwaka 669, alichaguliwa kuwa Askofu wa York. Akajenga na kafungua manosteri nyingine za Benedictine. Akalazimika kwenda Roma kuzuia mgawanyiko wa jimbo, uliotaka kutokea kutokana na Askofu Theodore wa Canterbury, kuchukua sehemu ya jimbo la York. Akalazimika kukaa uhamishoni, kusubiri suluhisho la tatizo hilo. Akiwa huko alifanya kazi kubwa ya kuhubiri Injili huko Saxons.
Akarudi tena jimboni kwake mwaka 686. Na mwaka 691 aliamua kumpumzika na akaitwa tena na mamlaka kufanya kazi. Mwaka 703, alistaafu nafasi zake na kwenda kukaa katika Manosteri ya Ripon. Huko alitumia muda wake kusali na kusoma maandiko.
Mtakatifu Wilfrid, alikufa mwaka 709.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Amicus
Mh. Camillus Constanzi
Mt. Cosmas wa Maiuma
Mt. Domnina wa Anazarbus
Mt. Edistius
Mt. Edwin wa Northumbria
Mt. Eustace
Mt. Evagrius
Wat. Felix na Cyprian
Mt. Fiace
Mt. Heribert wa Cologne
Mh. Maria Teresa Fasce
Mt. Maximilian wa Lorch
Mt. Monas
Mt. Pantalus
Mt. Salvinus
Mt. Seraphinus

No comments:

Post a Comment