Mtakatifu John Brebeuf alizaliwa mwaka 1593 March 25 huko Normandy, Ufaransa. Alijiunga na shirika la Wa Jesuit mwaka 1617, na mwaka 1622, alipata daraja la upadri huko Pontoise.
Mwaka 1625 aliwasili Quebec (Canada),ambako alitumwa na shirika, kufanya umishenari. Alienda huko akiwa na mapadri wengine wawili na watawa wawili (Brothers )
Akaishi na watu wa kabila ya Algonquin kwa miezi 5 na baadaye akapangiwa kufanya umishenari katika kabila ya Huron, akiwa na Padri Anne Nouee.
Huko alijaribu mno kuwafundisha wenyeji juu ya kanisa bila mafanikio. Akaitwa kurudi Quebec kutokana na vita ya makoloni mwaka 1628.
Mwaka1629 mtakatifu John , pamoja na wamishenari wengine walirudi Ufaransa, katika mji wa Rouen.Hapo aliweka nadhiri zake na kufanya kazi mbalimbali, huku akihubiri na kufundisha.
Mwaka 1633, akiwa na mapadri wengine, walirudi tena Quebec. Wakachagua mji wa Ihonatiria, kuwa makao yao.Katika nyakati hizo watu wa kabila ya Huron, walikuwa wakisumbuliwa na ugonjwa wa kuambukiza, ambao waliupata kutoka kwa mabaharia wa kizungu. Ugonjwa huo uliuwa watu wengi.
Mtakatifu John, alijifunza lugha yao,pamoja na desturi zao.Akawafundisha wamisionari wenzie lugha za wenyeji. Mwaka 1635 aliwabatiza wenyeji 14, mwaka uliofuata 86.
Mwaka 1649 , wenyeji ambao hawakupenda mabadiliko, waliwakamata mapadri ,wakachoma makazi yao.Mwaka huo huo mwezi March 16, walimuua mtakatifu John, na wenzake baada ya mateso makali.
Mtakatifu John Brebeuf alitangazwa mwenye heri mwaka 1925 na akatangazwa mtakatifu mwaka 1930 na Papa Pius XI
*Mtakatifu Isaac Jogues*
Mtakatifu Isaac Jogues alizaliwa mwaka 1607, Januari 10 huko Orleans, Ufaransa. Mwaka 1624, alijiunga na wa Jesuit huko Rouen.
Mtakatifu Isaac Jogues alizaliwa mwaka 1607, Januari 10 huko Orleans, Ufaransa. Mwaka 1624, alijiunga na wa Jesuit huko Rouen.
Mtakatifu Isaac, aliweka nadhiri za kwanza mwaka 1626 na akaenda kusoma filosofia katika chuo cha La Fleche, na mwaka 1629, alirudi Rouen kufundisha vijana. Mwaka 1633 alienda tena kusoma katika College de Clermont huko Paris, akisoma teolojia. Na mwaka 1636, akapata daraja la upadri huko Clermont.
Mtakatifu Isaac, alivutiwa na wamisionari waliorudi Ufaransa, toka Quebec mwaka 1636, na akapangiwa kwenda nao tena kufanya uinjilishaji. Na Akapangiwa kwenda kuinjilisha katika kabila ya Huron. Alifika huko 2 Julai 1636.
Aliishi katika mji wa Ihonatiria kwa miaka 4, baadae kuanza kuzunguka katika vijiji kadhaa kwa miezi mingi .Huko walipokewa kwa u baridi mno, kutokana na wenyeji kutaka kuishi maisha yao, na kufuata dini zao za asili.
Mwaka 1652 August 3, mtakatifu Isaac na mapadri wengine, pamoja na kundi la wakristo wa Huron, walijikuta katikati ya mapigano makali ya kabila za wenyeji wenye uadui mkubwa.
Yeye alimudu kujificha katika shamba lililokuwa jirani, lakini alipoona wakristo wengi wamekamatwa , alijitokeza .Mtakatifu Isaac , aliteswa sana , na alishikiliwa mateka kwa muda wa miezi 10.Akarudi Ufaransa.
Mtakatifu Isaac, aliachiwa na akarudi Ufaransa. Lakini mwaka 1644, alirudi tena Quebec na mwaka 1646 alikwenda tena katika kabila ya Huron na akajaribu kuwa msuluhishi kati yao na kabila ya Mohawk.
Lakini tarehe 18 October 1646 watu wa kabila la Iroquois na Mohawk, walimuua mtakatifu Isaac na kuitupa maiti yake mtoni ,na kesho yake wakauwa Padri mwingine.
Isaac Jogues alitangazwa mwenye heri mwaka 1925 June 21 na Papa Pius XI na kutangazwa mtakatifu mwaka 1930 June 29 na Papa Pius XI.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
M/h. Agnes de Jesus Galand
Mt. Altinus
Mt. Anthony Daniel
Mt. Aquilinus
Mt. Beronicus
Mt. Charles Garnier
Mt. Cleopatra
Mt. Desiderius
Mt. Eadnot
Mt. Ethbin
Mt. Eusterius
Mt. Frideswide
Mt. Gabriel Lalement
Mt. John wa Rila
Mt. Laura
Mt. Lupus wa Soissons
Mt. Philip
Mt. Theofrid
Mt. Varus
Mt. Veranus wa Cavaillon
M/h. Agnes de Jesus Galand
Mt. Altinus
Mt. Anthony Daniel
Mt. Aquilinus
Mt. Beronicus
Mt. Charles Garnier
Mt. Cleopatra
Mt. Desiderius
Mt. Eadnot
Mt. Ethbin
Mt. Eusterius
Mt. Frideswide
Mt. Gabriel Lalement
Mt. John wa Rila
Mt. Laura
Mt. Lupus wa Soissons
Mt. Philip
Mt. Theofrid
Mt. Varus
Mt. Veranus wa Cavaillon
No comments:
Post a Comment