Tuesday, November 14, 2017

Maisha ya Mtakatifu Benvenuta Bojani

Mwenyeheri Benvenuta Bojani, alizaliwa mwaka 1254 May 4, huko Cividale ,Friuli, Italia. Alikuwa mtoto wa mwisho katika familia iliyokuwa na mabinti 7.
Alipozaliwa, baba yake alikuwa na matumaini makubwa ya kupata mtoto wa kiume, hata hivyo alipoambiwa kuwa amezaliwa mtoto mwingine wa kike, alisema kuwa " hata huyo pia anakaribishwa" .Ndio maana ya jina lake Benvenuta.
Dada mkubwa wa mtakatifu Benvenuta, alijaribu kumfundisha kuvaa na kuishi kwa namna ilivyostahili kwa binti aliye katika familia ya kitajiri. Lakini Benvenuta, alikataa, na kuvaa mavazi ya kawaida kabisa.
Alijiunga na shirika la watawa wa Dominican, lakini hakukaa katika nyumba ya watawa ( Convent ). Katika maisha yake aliishi kwa sala za majitoleo, akifunga na kukesha akiomba.
Afya yake ilikuwa mbaya na alikuwa akishindwa hata kutembea .Nyakati zingine alisaidiwa na dada zake ili aweze kufika na kuwahi ibada. Kutokana na hali hiyo alikaa kitandani miaka mitano akiugua.
Muda wote wa maisha yake ya sala, alipata maono mbalimbali. Na pia, alipata majaribu mengi kutoka kwa shetani, kutokana na maradhi yake. Lakini aliyashinda .
Mwenye heri Benvenuta alikufa tarehe 30 October, 1292, katika mji wa Cividale, Friuli, Italia. Akatangazwa mwenye heri mwaka 1763, February 6 na Papa Clement XIV.
Mwenye heri Benvenuta, utuombee
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Bean
Mt. Albinus
Mt. Alfred mkuu
Mt. Cedd
Mt. Cuthbert wa Canterbury
Mt. Demetrius wa Thessaloniki
Mt. Eadfrid
Mt. Eata
Mt. Evaristus
Mt. Fulk wa Pavia
Mt. Gibitrudis
Mt. Lucian
Mt. Quadragesimus
Mt. Quodvultdeus
Mt. Rogatian
Mt. Rusticus wa Narbonne

No comments:

Post a Comment