
Mtakatifu Alberto Mkuu alizaliwa nchini Ujerumani mwaka 1205 na alifariki tarehe 15 Novemba 1280. Jina Alberto alilopewa kwa heshima askofu Alberto wa Bollstädt (au wa Cologne) kutokana na mchango wake mkubwa upande wa elimu alioutoa na ule wa dini na vilevile upande wa uchungaji na wa upatanishi wa watu na watawala.
Mtakatifu Alberto alikuwa Mtawa wa Shirika la Wahubiri, anahesabiwa kuwa mwanafalsafa na mwanateologia bora wa Ujerumani katika Karne ya Kati .
Mtakatifu Alberto Alijitahidi kulinganisha imani na akili akiingiza falsafa ya Aristotle katika Ukristo, jambo lililoendelezwa na mwanafunzi wake bora,Mtakatifu Thomasi wa Akwino.
Alitangazwa na Papa Gregori XV kuwa Mwenyeheri mwaka 1622 na baadae alitangazwa kuwa Mtakatifu Na Mwalimu wa Kanisa na Papa Pius XI, tarehe 16 Desemba 1931.Mwaka 1941 Papa Pius XII alimtangaza msimamizi wa wanasayansi .
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 15 Novemba.
No comments:
Post a Comment