Ee Yesu Bwana wetu mwema mno,uliyeikomboa dunia kwa upendo wa Moyo wako na Damu yako ya thamani kuu,uutazame kwa huruma yako ubinadamu wetu maskini,ulio bado kwa kiasi kikubwa katika giza la upotevu na katika kivuli cha mauti, uifanye nuru yote ya kweli yako iuangaze huu ubinadamu wetu.
Ee Bwana,utuzidishiwe idadi ya Mitume wa Injili yako, uwatilie bidii,uwajalie mafanikio ya kazi yao,ubariki juhudi yao na jasho lao kwa neema yako,ili hao wote wasio na imani ya kweli hadi hivi sasa wapate kukujua na kukukufuata wewe, uliye Muumba na Mkombozi wao. Uwarudishe katika umoja wa Kanisa lako wote waliofarakana na umoja huo.
Ee Mkombozi mwema mno,fikiwsha hima hapa duniani ufalme wako kwa wanaouwania, uwavutie watu wote kwenye Moyo wako Mtakatifu, ili wote waweze kushiriki baraka zisizo na mfano za Ukombozi wako katika ile heri ya milele huko mbinguni. Amina
No comments:
Post a Comment