Padre Pio ameitumia sana ili kuwaombea watu waliomwomba awakumbuke katika sala zake.
Ee Yesu,ulisema ombeni mtapewa,tafuteni mtapata,pigeni hodi mtafunguliwa.Kwa maombezi ya Bikira Maria Mama yako mtakatifu,naomba,natafuta napiga hodiili sala zangu zisikilizwe. Naomba(Taja ombi lako)
Baba yetu.....,Salamu Maria.........,Atukuzwe Baba.....
Moyo Mtakatifu wa Yesu,ninaweka matumaini yangu yote kwako.
Ee Yesu, ulisema
Lolote mtakalomwomba Baba kwa jina langu,atawapa.Kwa maombezi ya Bikira Maria,Mama yako Mtakatifu kwa unyenyekevu na juhudi, ninamwomba Baba yako Mtakatifu kwa jina lako , sala zangu zisikilizwe(taja ombi lako)
Baba yetu......,Salamu Maria........Atukuzwe Baba......
Moyo Mtakatifu wa Yesu,ninaweka matumaini yangu kwako.
Ee Yesu ulisema,
Mbingu na nchi zitapita,lakini maneno yangu hayatapita kamwe.Kwa maombezi ya Bikira Maria,Mama yako Mtakatifu natumaini kwamba sala zangu zitasikilizwa(Taja ombo lako)
Baba yetu....,Salamu Maria.....,.,Atukuzwe Baba
Moyo Mtakatifu wa Yesu, ninaweka matumaini yangu yote kwako.
Ee Moyo Mtakatifu wa Yesu ambao daima unawahurumia wenye shida, utuhurumie sisi wanyonge na wakosefu. Utupatie neema tunazokuomba kupitia Moyo Safi wenye huzuni wa Maria,Mama yako na Mama yetu
Salamu Malkia.....
Mtakatifu Yosef, Baba mlishi wa Yesu utuombee
No comments:
Post a Comment