Tuesday, November 21, 2017

Maisha ya Mtakatifu Lawrence Giustiniani

Image result for Life of saint Lawrence Giustiniani
Mtakatifu Lawrence alizaliwa tarehe 1 Julai 1381, huko Venice, Italia. Alizaliwa katika familia maarufu, ambayo ilishakuwa na watakatifu kadhaa.
Mwaka 1404 alipata daraja la ushemasi, na akajiunga na shirika la mapadri katika kisiwa cha San Giorgio, huko Alga. Mwaka 1407, alipata daraja la upadri na shirika alilokuwemo likaanza kufuata taratibu za mtakatifu Augustine.
Kwa jinsi alivyokuwa na maisha halisi ya kumcha Mungu, alikubalika mno katika jumuia yake. Akachaguliwa kuwa mkuu wa kwanza katika Jumuiya yake. Akasaidia kubadili baadhi ya vipengere katika miongozo ya shirika. Akachaguliwa kuwa mkuu wa shirika.
Mwaka 1433, Papa Eugene IV, ambaye alikuwa mmoja wa waanzilishi wa shirika San Giorgio, alimtangaza Lawrence Gustiniani kuwa Askofu wa Castello. Katika Castello, alifanya pia mabadiliko yaliyoleta ufanisi na maendeleo.
Mwaka 1451, Papa Nicholas V, aliunganisha jimbo la Castello na Grado, akaanzisha jimbo la Venice. Hivyo mtakatifu Lawrence akawa Askofu wa kwanza wa Venice.
Katika nyakati hizo, kukatokea mji wa Constantinople kutekwa na majeshi ya waislam.Watu wa Venice walipata mashaka makubwa, kwa kuwa walikuwa wakifanya biashara na Constantinople. Lakini Askofu Lawrence, aliwatuliza, akajadiliana na watawala jinsi ya kulikabili tatizo hilo.
Mtakatifu Lawrence alikufa mwaka 1456, Januari 8, huko Venice. Akatangazwa Mwenyeheri mwaka 1524, akatangazwa mtakatifu Oktoba16, 1690 na Papa Alexander VIII.

St. Lawrence Giustiniani - Saints & Angels - Catholic Online


*Watakatifu wengine wa leo*
Mt.Teresa wa Calcutta
Mt. Alvitus
Mt. Bertin
Mt. Bertinus
Mt. Charbel
Mt. Eudoxius
Mt. Herculanils
Mt. Joseph Canh Luang Hoang
Mt. Obdulia
Mt. Peter Tu
Mt. Quintius
Mt. Romulus
Mt. Victorinus
M/h. William Browne

No comments:

Post a Comment