Tuesday, November 14, 2017

Maisha ya Mtakatifu Mwenyeheri Dorothea

Mwenyeheri Dorothea, alizaliwa mwaka 1347 February 6, huko Montau, Prussia (Ujerumani sasa). Alikuwa Binti wa Willem Schwartze ambaye alikuwa mkulima tajiri.
Akiwa na miaka 17 , aliolewa na mhunzi aliyeitwa Adalbrecht wa Danzig, ambaye alikuwa na miaka 40, na mwingi wa hasira.
Muda mfupi baada ya kuolewa , alianza kupata maono. Mwenyeheri Dorothea na mumewe , walikwenda kuhiji katika miji mbalimbali ndani ya Ujerumani .Na alipata ruhusa ya mumewe kwenda kuhiji Roma. Akiwa huko mumewe alikufa.
Katika ndoa yake, alipata watoto 9.Wanne walikufa wakiwa wadogo na wanne wengine walikufa baada ya kupatwa na ugonjwa wa kuambukiza, uliotokea mjini kwao.Aliyebaki mmoja, aliitwa Gertrud, alijiunga na watawa wa Benedictine.
Mwaka mmoja baada ya kifo cha mume wake (1391), Dorothea alihamia katika mji wa Marienwerder. Tarehe 2 May 1393 alijenga chumba kidogo mno katika ukuta wa Cathedral kwa ruhusa maalum,ambako alianza maisha ya sala na ibada, na hakutoka tena humo mpaka mwisho wa maisha yake.
Mwenyeheri Dorothea alikufa tarehe 25 June 1394 na akatangazwa mwenye heri mwaka 1976 na Papa Paul VI.
*Mwenyeheri Contardo Ferrini*
Mwenyeheri Contardo Ferrini alizaliwa mwaka 1859 April 5, huko Milan, Italia. Alikuwa mwana wa Rinaldo Ferrini na Luigia Buccellati.
Alibatizwa na akapata komunio ya kwanza akiwa na miaka 12. Baba yake alikuwa na Profesa wa hesabu na sayansi, hivyo alimfunza mwanawe vitu vingi mapema. Alimfunza pia lugha mbalimbali.Lakini Contardo, alikuwa mtu aliyemcha Mungu, tokea utoto wake.
Mwenyeheri Contardo, alijiunga na chuo kikuu cha Pavia, akiwa na miaka 17 tu. Akiwa na miaka 21 tayari alikuwa daktari wa sheria. Akapewa nafasi ya kusoma katika chuo kikuu cha Berlin Ujerumani.
Akiwa huko, aliandika machapisho mbalimbali kuhusu Sakramenti ya kitubio. Na alipomaliza masomo yake, alirudi Italia, na akaanza kufundisha katika vyuo mbalimbali, pamoja na chuo kikuu cha Pavia.
Alikuwa Profesa akiwa na miaka 26

No comments:

Post a Comment