Tuesday, November 14, 2017

Maisha ya Mtakatifu Didas wa Sevila Mtawa(Life of Saint Didas of Sevila)


Mtakatifu Didas alizaliwa mwaka 1400, huko San Nicolas del Puerto , Seville Hispania.Alizaliwa katika familia ya kimaskini na wazazi wake walimuita Diego.Akiwa mdogo alionyesha kupenda maisha ya kitawa.Baadae akaamua kuishi katika mwelekeo wa kitawa.Akaishi kwa kumfuata Padri mmoja aliyekuwa akiishi nao pale.
Akaomba kujiunga na shirika la watawa lililokuwa pale Arruzafa, karibu na Cordoba, ambako alipokelewa.Katika muda aliokuwa pale, alitembea katika vijiji na miji ya Cordoba, Cardiz na Seville ,akihubiri na kufundisha.Akatumwa na shirika kwenda huko Arrecife ,katika kisiwa cha Lanzarote kati ya visiwa vya Canary.

Mwaka 1445 alichaguliwa kuwa msimamizi wa Wafransiscani katika kisiwa cha Fuerteventura ambapo walifungua kituo cha Mtakatifu Bonaventure. Mwaka 1450 aliitwa Hispania , baadae akaenda Roma katika mwaka wa jubilee uliotangazwa na Papa Nicholas V, na kuwakilisha katika sherehe ya kutangazwa mtakatifu Bernadine wa Siena.Watawa, na mahujaji wengi walienda Roma muda huo, hali iliyosababisha mlipuko wa magonjwa mbalimbali.Mtakatifu Didas alikaa miezi mitatu akisaidia wagonjwa katika kituo cha watawa kilichokua karibu na Basilika la Maria Mtakatifu hapo Ara Coeli.Hapo miujiza mingi ya kiuponyaji ilijitokeza.

Akaitwa tena Hispania na wakuu wake, ambako alipangiwa kwenda kufanya kazi katika kituo cha Santa Maria de Jesus katika mji wa Alcala.Aliishi na kufanya kazi mpaka alipokufa , mwaka 1463, Novemba 12, hapo hapo Alcala de Henares, Toledo, Castile Hispania.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Lawrence O'Toole
Mt. Alberic wa Utrecht
Mt. Clementinus
Mt. Dubricus
Mt. Gregory Palamas
Mt. Hypatius wa Gangra
Mt. Joseph Pignatelli
Mt. Jucundus wa Bologna
Mt. Lawrence O'Toole
Mt. Modanic
Mt. Serapion
Mt. Venaranda

No comments:

Post a Comment