Mtakatifu Marcellus, alikuwa askari mwenye cheo kikubwa katika jeshi la Warumi, chini ya mfalme Maximian. Alipangiwa kufanya kazi katika mji wa Tingis (Tangier Morocco )
Ikatokea sikukuu ya kumbukizi ya kuzaliwa ya mfalme Maximian, ambayo iliadhimishwa na raia na wana jeshi, katika himaya ya mfalme huyo. Katika sherehe hiyo, ilikuwa lazima kwa Marcellus kutoa sadaka kwa miungu ya Kirumi ambayo mfalme aliiamini.
Marcellus aliamua kutokushiriki katika jambo hilo, kwani yeye alikuwa mkristo, na kwa kuamua hivyo, alijiuzuru nafasi yake jeshi na akavua vyeo vyake, pamoja na silaha zake.
Kutokana na jambo hilo, Marcellus alikamatwa, akawekwa jela. Akapelekwa kwa kiongozi aliyeitwa Aurelius Agricolaus, ambaye alimuhukumu kifo, baada ya Marcellus kukubali alichokiamua na kukifanya.
Mtakatifu Marcellus aliuwawa kwa kukatwa kichwa, katika mwaka 298, katika mji wa Tingis.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Wolfgang
Mt. Abaidas
Mt. Antoninus
Mt. Arnulf
Mt. Bega
Mt. Erth
Mt. Notburga
Mt. Quentin
Mt. Wolfgang
Mt. Abaidas
Mt. Antoninus
Mt. Arnulf
Mt. Bega
Mt. Erth
Mt. Notburga
Mt. Quentin
No comments:
Post a Comment