Mtakatifu Andrea Avelino Mtawa alizaliwa mwaka 1521b huko Italia kwenye mji wa Castronuovo Jina lake la ubatizo ni Lancelotto ambalo lilikuwa nje na upendo wa Msalaba na kwa kuwa alitamani kuupenda msalaba kama Mtakatifu Andrea aliamua kuchaguwa kupewa jina hilo.
Inasemekana alifanya kazi kubwa ya kuwahudumia watu kiroho kwa moyo wote ambapo matendo yake yalikuwa yanaudhihirishia jumuiya kuwa nguvu ya Mungu ilikuwa ndani yake.Mtakatifu Andrea Avelino ni msomi wa shahada ya sheria.Na kupitia hiyo elimu aliitumia kutoa haki katika maamuzi yake akiwa akiudumia kwenye maswala ya kikanisa baadae alikuja kupata daraja la upadri.
Mtakatifu Andrea Avelino alifariki tarehe 10 Novemba 1608 baada ya kuugua gafla ugonjwa wa Moyo akiwa kwenye maadhimisho ya Misa Takatifu .
Fundisho ninalojifunza Binafsi.Kuupenda msalaba kwa kuwa wokovu wetu umetokana na msalaba hasa baada ya kifo cha mkombozi wetu Yesu Kristu na pia mwanadamu anaweza kupata mabadiliko kutokana na historia ya watu wengine na zaidi kujifunza yaliyomema siku zote.
Read here more
No comments:
Post a Comment