Monday, November 13, 2017

Tungo yangu ya Sala binafsi

Sala ya Kuomba Msaada wa Upendo wa Dhati
Ee Mwenyezi Mungu katika fumbo la Utatu Mtakatifu Mungu Baba,Mungu Mwana Na Mungu Roho Mtakatifu ninakuomba unihurumie niwazavyo kinyume na upendo wa kweli.

Ninakuomba unijalie upendo wa dhati kwa marafiki zangu ili wapatapo mafanikio hata kama bado naangaika isiwe ni sehemu ya kujisikia vibaya na pengine kamwe nisipate kinyongo rohono bali unipe subira nitambua mda wangu ukifika utanipatia hata kuzidi wenzangu.

Ninazidi kukuomba unipe moyo wa kupenda kuwashirikisha marafiki zangu na wasio marafiki zangu na wale waliokwisha nikatisha tamaa kufanya hivyo ili nao waweze kunufaika kwa uwepo wangu pia.

Ninakuomba kamwe nisije kutokea hata siku moja nikajikweza pale wanapokuwa wamefanikiwa kupitia mikono yangu kupitia maswala mbalimbali ya mafanikio yawe ya kiroho ama kimwili bali inipatie nafasi zaidi ya unyenyekevu mbele yako nikiendelea kukusifu na kukutukuza milele yote na mwisho iniwezeshe kufika kwako mbinguni siku moja kupitia hazina nitakayokuwa nimeitenda hapa duniani kwa ajili ya watu wako.

Ninaomba na kushukuru kwa njia ya Kristu Bwana Wetu.

            Amina


No comments:

Post a Comment