Mtakatifu Leo Mkuu na Baadhi ya historia imemuandika kama ni Papa Leo katika enzi za uhai wake akiwa Papa. Historia yake haioneshi maisha yake ya kuzaliwa kwake japo inasemekana alizaliwa nchini Italia ila sehemu nyingine inaonesha aliishi to miaka ya 400 hivi mpaka tarehe 10 Novemba 461 na hii tarehe ndo tunakuwa tunasherekea sikukuu yake ya Utakatifu.Jina lake la kuzaliwa lilikuwa hilo hilo yaani Leo.
Kwa ufupi katika maisha yake ujanani.alizaliw3a na familia ya kisharifu ama Roma ama mkoa wa Toscana ambapo ni Italia ya Kati mnamo huo mwaka wa 400. kutokana na umaridadi wake na umaarufu wake mwaka 431 akiwa shemasi tu na pengine aliandikwa na sirili wa Aleksandria ili amuunge mkono dhidi ya Juvenali wa Yerusalemu. Wakati huo huo Yohane Kasiano alimuandikia kitabu dhidi ya Nestori wa Konstantianopoli. Na zaidi Malkia wa Magharibi alimteua kuwapatanisha maofisa wakuu wa Galia ambapo leo hii inajulikana Ufaransa na wakati huo akiwa kwenye kazi ya upatanishi Papa Sixtus III alifariki tarehe 11 Agosti 440 hapo ndo alichaguliwa na umati kwa kauli moja kushika nafasi ya Papa Sixtus III.
Mtakatifu Leo Mkuu alianza kazi ya Upapa mara baada ya Papa aliyekuwa anamuudumia kufariki na alikuwa ametumwa kwenda kufanya kazi ya kupatanisha. Mtakatifu Leo Mkuu alikuwa Papa wa muda mrefu kuanzia tarehe 29 Septemba,440 hadi kifo chake kipindi ambacho usalama wa Roma ulikuwa unatishwa na makabila yasiyostrabika.Tarehe 29 Septemba alianza kazi rasmi kama Papa ambayo ilichangia sana kukusanya mamlaka ya Kanisa lote katika jimbola Roma, ambapo alifanikiwa kuliunda upya pamoja na majimbo mengine ya Italia.Ili kuimarisha nafasi hiyo ya Kanisa pekee la Magharibi lililoanzishwa na mitume Mtakatifu Leo Mkuu, alijitafutia hati maalumu kwa Kaisari Valentiniano II na inasemekana haikuwapendezesha Wakristo wa Mashariki.
Nafasi bora ya kusisitiza kwa busara mamlaka hiyo hata upande wa mashariki ilitolewa na mabishano kuhusu nafsi ya Yesu Kristo yaliyosababishwa na Eutike kukanusha ubinadamu halisi wa Kristo.
Katika waraka maarufu aliomuandikia Patriarki Flavianus wa Konstantinopoli mnamo mwaka 449 ili kumuangalisha kuhusu uzushi uzushi wa mtu huyo, Leo alifafanua wazi namna umungu na utu na wa Kristo yanavyounganika katika nafsi yake.
Hata hivyo mwaka huohuo mtaguso unaojulikana kama Wizi wa Efeso ulipuuzia waraka huo usisomwe, ukamtetea Eutike. Hapo Leo akashika uongozi wa mapambano dhidi yake.
Mwaka 451 katika Mtaguso wa Kalsedonia , baada ya barua yake kwa Flavianus kusomwa, maaskofu wote 350 walisimama na kulia: "Ndiyo imani ya mababu... Mtume Petro amesema kwa njia ya Leo..." Hivyo ilithibitishwa imani katika hali mbili za Kristo zisizochanganyikana wala kutenganika.
Hata hivyo mabalozi wa Leo hawakuwekwa kati ya viongozi wa mtaguso, na kanuni ya 28 ilidai Kanisa la Konstantinopoli kuwa muhimu sawa na la Roma. Kwa hiyo Leo aliikataa, akisisitiza nafasi ya kwanza ya Roma ili kudumisha umoja hasa katika kipindi hicho cha fujo.
Vilevile, Leo alipambana kwa nguvu na Wapelaji,Wamani na Waprishila akitetea daima imani kadiri ya mapokeo ya mitume, akiunganisha vizuri ajabu unyenyekevu wake mwenyewe na hakika juu ya ukuu wa cheo chake kama mwandamizi wa Mtume Petro ; vilevile alipambana na ushirikina na Wapagani.
Lakini pia akuishia mambo ya kiroho pia aliweza kufanya hata shughuli za kisiasa kupitia mambo mbalimbali kama ifuatavyo.Wakati Dola laRoma lilipokuwa likisambaratika, Leo alipata umaarufu pia kwa kutumia mamlaka yake ya kiroho tu ili kuzuia uvamizi wa Roma uliohofiwa kufanywa na Atila , mfalme wa Wauni mwaka 452 na ili kupunguza madhara ya ule uliofanywa na Wavandali kwa wiki mbili mwaka 455. Tena alistawisha matendo ya huruma mjini kwa waliopatwa na njaa,dhuluma na ufukara, kama vile umati wa wakimbizi.
Na inasemekana ndo Papa wa kwanza kuitwa Mkuu ndo maana anaitwa Mtakatifu Leo Mkuu kutokana na mchango mkubwa alioutoa upande wa dini na wa siasa ambapo aliwajibika kuhudumia taifa la Mungu kwa kila namna. Ni kati ya Mapapa bora kuwahi kutokea katika Kanisa la Roma sifa na kuliimarisha mamlaka yake wakati ile ya serikali ya jiji hilo ilikuwa inafifia zaidi na zaidi na inasemekana anaheshimika kama Mtakatifu na babu wa Kanisa na mwaka 1754 Papa Benedikto XIV alimuongezea sifa nyingine kama mwalimu wa Kanisa
Mambo ya Pekee kuhusu Mtakatifu Leo Mkuu.
Mtakatifu Leo Mkuu aliunganisha vizuri ajabu unyenyekevu wake mwenyewe na hakika ya ukuu wa cheo chake kama mwandamizi wa Mtume Petro, akiingilia kati masuala mbalimbali magharibi na mashariki vilevile kwa njia ya barua na ya mabalozi wake.
Umuhimu wa Upapa wa Leo, ambao ulidumu muda mrefu kuliko Mapapa karibu wote, ni katika kusisitiza hata kwa madondoo ya Biblia mamlaka ya pekee ambayo Kanisa la Roma linayo juu ya makanisa yote duniani kutokana na Mtume Petro kuwekwa na Kristo na kufia Roma walipo waandamizi wake.
Ndilo fundisho linalojitokeza mfululizo katika barua zake 143 na hasa katika hotuba 96 zilizopo hata leo.
Humo unajitokeza utajiri na uwazi wa mafundisho aliyoyatoa kwa lugha sahili na safi. Ndio mkusanyo wa kwanza wa hotuba za Kipapa zilizochangia sana ustawi wa Kanisa baadaye.
Aliunganisha matendo ya ibada na maisha ya kila siku ya Wakristo , k.mf. saumu na matendo ya huruma. Alionyesha kuwam liturujia ya Kikristo si kumbukumbu ya matukio yaliyopita, bali utimiaji wa mambo yasiyoonekana katika maisha ya kila mmoja. Hivyo ni lazima Psaka iadhimishwe kila wakati wa mwaka , “si kama jambo la zamani, bali kama tukio la leo”. Hata siku hizi Liturujia ya Roma inazidi kutumia matini yake mengi na kufuata mtindo wake bora katika sala.
For reading more source"
For reading more source"
No comments:
Post a Comment