Imebeba sala na muongozo juu ya Ukatoliki katika kuutafuta utakatifu ila na mwanadamu yoyote apendezwaye na sala hizi naomba aungane kwenye jumuiya hii maana sote ni baba mmoja katika itikadi tofauti Amina
Thursday, November 2, 2017
Mtakatifu Christopher(25 Julai)
Ni msimamizi wa wasafiri na madreva.Mtakatifu Christopher anatajwa sana huko Ulaya na katika Makanisa ya Magharibi kuwa masimamizi wa wasafiri na madreva. Hata hivyo lakini hatuna historia ya uhakika kuhusu maisha yake.Masimulizi yasema alikuwa anasaidia kuvusha watu kwenye mkondo mkali wa maji kwamba siku moja alibahatika kumbeba mtoto mmoja ambaye alimshinda uzito wakati wakiwa katikati ya mkondo. Katika kustajabia , Mtakatifu Christopher alifunuliwa kwamba huyo mtoto siyo wa kawaida, bali ni Kristo Yesu. Ndio maana ya jina lenyewe Christopher,mchukuwa Kristo.
Sala
Mtakatifu Christopher msimamizi wa wasafiri najikabidhi kwako sasa na wote hawa tutakayofanya pamoja safari hii Utulinde na hatari zote, tufike salama huko tuendako.Naomba sana msaada wako, hasa niwezekuepuka kabisa dhambi na kushinda maana ndilo ovu kupita maovu yote. Unilende pamoja na marafiki zangu wote dhidi ya tetetmeko la nchi,vimbunga na dhoruba, radi na moto, mafuriko na maafa ya aina yote
Utuongoze salama kati ya hatari na mauti hadi tufikie maskani ya daima, mbinguni.
Amina
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment