Alisoma teolojia huko Reims, Ufaransa, na kisha kurudi Cologne. Mwaka 1055 alipata daraja la upadri, na mwaka 1056 aliitwa na Askofu Gervais wa Reims.Huko mtakatifu Bruno, alifundisha na kusimamia shule za jimbo.
Katika shule hizo alifundisha watu mbalimbali pamoja na Papa Urban II, makardinali, maaskofu, wakuu wa mashirika na watakatifu.
Mwaka 1075 mtakatifu Bruno aliteuliwa kuwa Katibu wa jimbo la Reims. Na Pia Askofu Gervais, alikuwa amestaafu , na nafasi yake kuchukuliwa na Manasses de Goumai, ambaye alikuwa na mwelekeo tofauti.
Kutokana na taratibu zake, wakristo katika jimbo la Reims walimkataa Askofu . Na wakawa wakitaka mtakatifu Bruno, ashike nafasi hiyo.Lakini mtakatifu Bruno, hakupendezwa na jambo hilo.
Mtakatifu Bruno aliondoka hapo, akiwa na wenzake wawili na kwenda kwa Askofu wa Grenoble, ambaye alimpokea na kumpeleka sehemu iliyoitwa Dauphine, Chartreuse, karibu na mji wa Grenoble.
Urban II alivyokuwa Papa, alimwita mtakatifu Bruno kwenda Roma mwaka 1090.Akiwa Roma alifanya kazi nyingi, akimsaidia Papa na kumshauri katika mambo mbalimbali.
Mwaka 1091, alikataa tena pendekezo la kuwa Askofu. Mawazo na nia yake, ni kurudi tena Dauphine, ili aendelee kuishi na wenzake aliotoka nao Reims.
Hata hivyo hakurudi Reims, Akajenga kanisa dogo ,pamoja na nyumba chache za watawa, katika mji wa Squillace, Italia.
Mtakatifu Bruno alikufa mwaka 1101, October 06, huko Serra San Bruno, Italia.
Akatangazwa mwenye heri mwaka 1514 na Papa Leo X na mwaka 1623 February 17, akatangazwa mtakatifu na Papa Gregory XV.
Mtakatifu Bruno utuombee
*Watakatifu wengine wa leo ni*
M/h. Adalbero
Mt. Aurea
Mt. Ceollach
M/h. Diego Luis de San Vitores
Mt. Epiphania wa Pavia
Mt. Erotis
Mt. Faith
Mt. Francis Trung
M/h. Isidore wa mtakatifu Joseph
Mt. Magnus
Mt. Mary Frances
M/h. Marie Rose Durocher
Mashahidi wa Trier
Mt. Nicetas
Mt. Pardulphus
Mt. Sagar
Mt. Aurea
Mt. Ceollach
M/h. Diego Luis de San Vitores
Mt. Epiphania wa Pavia
Mt. Erotis
Mt. Faith
Mt. Francis Trung
M/h. Isidore wa mtakatifu Joseph
Mt. Magnus
Mt. Mary Frances
M/h. Marie Rose Durocher
Mashahidi wa Trier
Mt. Nicetas
Mt. Pardulphus
Mt. Sagar
No comments:
Post a Comment