Mtakatifu Luka alizaliwa huko Antiokia, wakati huo chini ya utawala wa dola ya Warumi.
Tukisoma katika Wakolosai 4:14, tunagundua pia kuwa Luka alikuwa tabibu.
Mtakatifu Luka, alifuatana na mtume Paulo, kwenda sehemu mbalimbali kufanya uinjilishaji (Philemon 1:24). Katika 2 Tim 4: 11 tunaona katika tabu zote, bado mtakatifu Luka, hakumwacha Paulo peke yake.
Katika Biblia tunaona pia, jinsi Luka alivyoandika miujiza mbalimbali ya Kristo, ambayo haikuandikwa katika Injili zingine.
Katika Injili ya Luka tunakutana pia na maandiko kuhusu Mama Maria, ambayo mengine hatuyapati katika Injili zingine, Kama Salamu Maria.
Mtakatifu Luka alikufa huko Boeotia (Ugiriki ) ambako alitulia ili kuandika Injili.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Asclepiades
Mt. Athenodorus
Mt. Gwen
Mt. Justus wa Beauvais
Mt. Kevoca
Mt. Monon
Mt. Peter wa Alcantara
Mt. Tryphonia
Mt. Athenodorus
Mt. Gwen
Mt. Justus wa Beauvais
Mt. Kevoca
Mt. Monon
Mt. Peter wa Alcantara
Mt. Tryphonia
No comments:
Post a Comment