Sala za Asubuhi
Ee Baba yetu Mungu Mkuu, Umenilinda usiku huu,
Ninakushukuru kwa moyo, Ee Baba, Mwana na Roho, Nilinde tena siku hii, Niache
dhambi nikutii, Naomba sana Baba wee, Baraka yako nipokee, Bikira safi ee
Maria, Nisipotee unisimamie, Mlinzi Mkuu Malaika wee, Kwa Mungu wetu niombee,
Nitake nitende mema tu, Na mwisho nije kwake juu, Amina.
Nia Njema
Kumheshimu Mungu wangu, Namtolea roho yangu, Nifanye kazi
nipumzike, Amri zake tu nishike, Wazo neno tendo lote, Namtolea Mungu pote,
Roho, mwili chote changu, pendo na uzima wangu, Mungu wangu nitampenda, Wala
dhambi sitatenda, Jina lako nasifia, Utakalo hutimia, Kwa utii navumilia, Teso
na matata pia, Nipe Bwana neema zako, Niongezee sifa yako, Amina.
Sala ya matoleo
Ee Yesu kwa mikono ya Bikira Maria, na kwa maungamo na
sadaka yako kuu, ninakutolea sala, matendo, masumbuko na furaha zangu zote za
leo. Ee Yesu, ufalme wako utufikie
Baba yetu
Baba Yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe; Ufalme wako ufike,
Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku,
Utusamehe makosa yetu, Kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea. Usitutie katika
kishawishi, Lakini utuopoe maovuni. Amina.
Salamu maria
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe;
umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa
kwetu. Amina.
Kanuni ya imani
Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi,/ mwumba mbingu na dunia./
Na kwa Yesu Kristu, Mwanaye wa pekee, Bwana wetu;/ aliyetungwa kwa Roho
Mtakatifu,/ akazaliwa na Bikira Maria,/ akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato,/
akasulubiwa, akafa, akazikwa,/ akashukia kuzimu;/ siku ya tatu akafufuka katika
wafu;/ akapaa mbinguni;/ amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi;/ toka huko
atakuja kuwahukumu wazima na wafu. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu,/ Kanisa
takatifu katoliki,/ ushirika wa Watakatifu,/ maondoleo ya dhambi,/ ufufuko wa
miili,/ uzima wa milele. Amina.
Amri Za Mungu
1. ndimi bwana mungu
wako, usiabudu miungu wengine. 2. usilitaje bure jina la mungu wako. 3. shika
kitakatifu siku ya mungu. 4. waheshimu baba na mama, upate miaka mingi na heri
duniani. 5. usiue 6. usizini 7. usiibe 8. usiseme uongo 9. usitamani mwanamke
asiye mke wako 10. usitamani mali ya mtu mwingine
Amri Za Kanisa
1. hudhuria misa takatifu dominika na sikukuu zilzoamriwa 2. funga
siku ya jumatano ya majivu; usile nyama siku ya ijumaa kuu 3. ungama dhambi
zako walau mara moja kila mwaka 4. pokea ekaristi takatifu hasa wakati wa
pasaka 5. sadia kanisa katoliki kwa zaka 6. shika sheria katoliki za ndoa
Sala Ya Imani
mungu wangu, nasadiki maneno yote linalosadiki , na
linalofundisha kanisa katoloki la roma:kwani ndiwe uliyefundisha
hayo,wala hudanganyiki, wala hudanganyi.amina
Sala Ya Matumaini
mungu wangu, natumaini kwako nitapewa kwa njia ya yesu
kristu,neema zako duniani na utukufu mbinguni, kwani ndiwe uliyeagana hayo
nasi, nawe mwamini.amina
Sala Ya Mapendo
mungu wangu, nakupenda zaidi ya cho chote, kwani ndiwe
mwema mwema, ndiwe mwenye kupendeza. nampenda na jirani yangu kama nafsi
yangu, kwa ajili yako.amina.
Sala Ya Kutubu
mungu wangu, nimetubu sana dhambi zangu, kwani ndiwe mwema ndiwe
mwenye kupendeza, wachukizwa na dhambi. basi sitaki kukosa tena, nitafanya
kitubio, naomba neema zako nipata kurudi amina.
Sala Kwa Malaika Mlinzi
malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote za roho na za
mwili amina
Sala ya Malaika wa Bwana.
Malaika wa Bwana
alimpasha habari Maria, naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Salamu
Maria,…. Ndimi Mtumishi wa Bwana, nitendewe ulivyonena. Salamu Maria, …… Neno
wa Bwana akatwaa Mwili, akakaa kwetu. Salamu Maria, ….. Utuombee, ee Mzazi
Mtakatifu wa Mungu, tujaliwe ahadi za Kristo. Tuombe: Tunakuomba ee Bwana, utie
neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika, kwamba,
Kristo Mwanao amejifanya mtu: kwa mateso na Msalaba wake, utufikishe kwenye
utukufu wa ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu, Amina.
Malkia wa Mbingu
Malkia wa mbingu, furahi, aleluya. Kwani uliyestahili kumchukua,
Aleluya. Amefufuka alivyosema, Aleluya. Utuombee kwa Mungu, Aleluya. Furahi
shangilia, ee Bikira Maria, Alaluya. Kwani hakika Bwana amefufuka Aleluya.
Tuombe. Ee Mungu, uliyependa kuifurahisha dunia kwa kufufuka kwake Bwana wetu
Yesu Kristu, Mwanao: fanyiza, twakuomba, kwa ajili ya Bikira Maria, tupate nasi
furaha za uzima wa milele. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina.
Sala za Jioni
Kwa jina la Baba na la Mwana na la
Roho Mtakatifu. Amina.
Sala ya Kushukuru.
Tunakushukuru, ee Mungu, kwa mapaji
uliyotujalia leo. Amina.
Baba yetu . . .
Salamu Maria . . .
Atukuzwe Baba . . .
Sala ya Imani.
Mungu
wangu, nasadiki maneno yote. Linayosadiki na linayofundisha Kanisa Katoliki la
Roma. Kwani ndiwe uliyetufumbulia hayo. Wala hudanganyiki, wala hudanganyi.
Amina.
Sala ya Matumaini.
Mungu
wangu, natumaini kwako, nitapewa kwa njia ya Yesu Kristo. Neema zako hapa duniani,
na utukufu mbinguni. Kwani ndiwe uliye agana hayo nasi, nawe mwamini. Amina.
Sala ya Mapendo.
Mungu
wangu, nakupenda zaidi ya chochote. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza.
Nampenda na jirani yangu, kama nafsi yangu, kwa ajili yako. Amina.
Kutubu dhambi.
Tuwaze
katika moyo wetu makosa ya leo tuliyomkosea Mungu kwa mawazo, kwa maneno, kwa
vitendo na kwa kutotimiza wajibu. (Husubiri
kidogo).
Nakuungamia
Mungu Mwenyezi, nanyi ndugu zangu, kwani nimekosa mno, kwa mawazo, kwa maneno,
kwa vitendo, na kwa kutotimiza wajibu.
Nimekosa
mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana. Ndiyo maana nakuomba Maria mwenye heri,
Bikira daima, Malaika na Watakatifu wote, nanyi ndugu zangu, niombeeni kwa
Bwana Mungu wetu.
Mungu
Mwenyezi atuhurumie, atusamehe dhambi zetu, atufikishe kwenye uzima wa milele.
Amina.
Sala ya kuombea watu.
Ee Mungu, nawaombea watu wa nchi
hii, wapate kusikia maneno yako na kukupenda wewe Bwana Mungu wetu.
Sala kwa Malaika Mlinzi.
Malaika mlinzi wangu, unilinde
katika hatari zote za roho na za mwili. Amina.
Malaika wa Bwana (kipindi
kisicho cha Pasaka)
Malaika wa Bwana alimpasha habari
Maria.
Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
Salamu, Maria,.....
Ndimi mtumishi wa Bwana.
Nitendewe ulivyonena.
Salamu, Maria....
Neno la Mungu akatwaa mwili.
Akakaa kwetu.
Salamu, Maria....
Utuombee, Mzazi mtakatifu wa Mungu.
Tujaliwe ahadi za Kristu.
Tuombe:
Tunakuomba,
Ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika
kwamba Mwanao amejifanya Mtu kwa mateso na msalaba wake tufikishwe kwenye
utukufu na ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. AMINA.
AU;
Malaika wa Mbingu (kipindi
cha Pasaka)
Malkia
wa mbingu, furahi, aleluya.
Kwani
uliyestahili kumchukua, Aleluya.
Amefufuka
alivyosema, Aleluya.
Utuombee
kwa Mungu, Aleluya.
Furahi
shangilia, ee Bikira Maria, Alaluya.
Kwani
hakika Bwana amefufuka Aleluya.
Tuombe.
Ee
Mungu, uliyependa kuifurahisha dunia kwa kufufuka kwake Bwana wetu Yesu Kristu,
Mwanao, fanyiza, twakuomba, kwa ajili ya Bikira Maria, tupate nasi furaha za
uzima wa milele. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina.
Atukuzwe (mara tatu)
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho
Mtakatifu. Kama mwanzo na sasa na siku zote na milele. Amina.
Kujikabidhi
Enyi Yesu, Maria na Yosefu
nawatolea moyo na roho na uzima wangu!
Enyi Yesu, Maria na Yosefu mnijilie
saa ya kufa kwangu!
Enyi Yesu, Maria na Yosefu mnijalie
nife mikononi mwenu!
(Rehema
ya siku 300).
Wimbo:
Kwa heri Yesu mpenzi mwema,
Naenda usiudhike mno.
Nakushukuru, nakupenda,
Kwa hizo nyimbo za mwisho.
Asubuhi nitarudi.
Yesu kwa heri.
Kwa heri Mama mtakatifu,
Sasa napita pumzika.
Asante kwa moyo na nguvu,
Leo umeniombea.
Asubuhi nitarudi.
Mama kwa heri.
Kwa heri Yosefu mnyenyekevu,
Kazi zatimilizika.
Kama mchana, leo usiku,
Nisimamie salama.
Asubuhi nitarudi.
Yosefu kwa heri.
Kwa jina la Baba na la Mwana na la
Roho Mtakatifu. Amina.
Kuomba Ulinzi wa Usiku
Mungu
wangu naenda kulala naomba malaika 14, waende nami, wawili juu, wawili chini,
wawili upande wa kuume, wawili upande wa kushoto, wawili wanifunike, wawili
waniamshe, wawili wanipeleke juu mbinguni. Mimi mtoto mdogo, roho yangu ni
ndogo, haina nafasi kwa mtu yoyote ila kwa Yesu pekee. Amina.