Fatima ni kijiji kilichopo Ureno ambapo mnapo mwaka 1916 palikuwepo watoto watatu ambao walikuwa wachunga kondoo walifunuliwa mambo mazito yatendekayo kupitia Rozari takatifu nao majina yao ni Lucia dos Santos (miaka 10), Francisco Marto (8) na Jacinta Marto (7).Watoto hao walitokewa na malaika kadiri ya maandiko ambapo aliwaambia kuwa yeye ni Malaika wa Amani. Aliwaambia waungane naye kuombea amani; maana hiki kilikuwa ni kipindi cha vita kuu vya kwanza vya dunia. Ilikuwa ni kama maandalizi ya kukutana na Bikira Maria.
Tarehe 13 Mei 1917 wakiwa machungani tena, waliona kama mtu akiwa anatoa nuru kali kuliko jua ambaye alikuwa ni mwanamke. Lucia alimwuliza anatoka wapi na anataka nini. Aliwaambia anatoka mbinguni na anataka wawe wanaenda pale inasemekana ilikuwa ni eneo liitwalo Cova da Iria kwa muda wa miezi sita lakini iwe ni kila tarehe ya 13 ya mwezi katika muda uleule. Kisha alisema kuwa baada ya hapo ndipo atawaambia kusudi lake. Akawaambia wawe wanasali rozari kila siku ili kuleta amani duniani na kumaliza vita.
Pia Tarehe 13 Juni 1917 walienda tena kwenye eneo lile inavyosemekana, na wakati huo kulikuwa na watu takribani 50 hivi pamoja nao ikadiliwavyo. Watoto wale walimwona tena huyoMama Bikira Maria (lakini si wale watu wengine) na akawaambia, “Nataka mje tarehe 13 mwezi ujao na kusali rozari kila siku. Kisha baadaye nitawaambia nitakacho.
Lucia alimwomba awapeleke mbinguni. Maria akasema kuwa angewachukua
Jacinta na Francisco baada ya muda mfupi, lakini Lucia angebaki. Ni kweli
Jacinta na Francisco walikufa wakiwa watoto lakini Lucia aliendelea kuwapo hadi
katika umri mkubwa.
Mama Bikira Maria alimwambia Lucia: Yesu anataka kukutumia wewe kunifanya mimi nijulikane na
kupendwa. Anataka kuanzisha ibada ya moyo wangu safi
duniani kote. Naahidi wokovu kwa yeyote atakayekubali; roho hizi
zitapendwa na Mungu. Kama maua yaliyowekwa name kupamba kiti chake cha enzi.”
Alafu tarehe 13 Julai watoto hao walifika tena Cova na kumwona Maria. Lucia
akamwuliza anachokitaka. Akawajibu tena: "Nataka mje hapa tarehe 13 mwezi
ujao ili kuendelea kusali rozari kila siku kwa heshima
ya Mama yetu wa Rozari; ili kuleta amani na mwisho wa vita duniani, ikiimanisha ni yeye tu ndiye anayeweza kuwasaidia."
Baadaye Mama Bikira Maria aliwaonyesha maono ya kuzimu
ambako roho nyingi zinateseka. Baada ya hapo kadiri ya maandiko, aliwaambia hao watoto kwamba: “Mmeona kuzimu zinakoteseka roho za wenye dhambi. Ili kuwaokoa, Mungu anataka kuanzisha duniani ibada kwa moyo wangu safi.
Kama mkifanya kile nitakachowaambia, roho nyingi zitaokolewa na kutakuwa
na amani ...”
Tarehe 13 Agosti ilipokaribia, habari hizi zilishafikia vyombo vya
habari ambavyo haviungi mkono mambo ya kidini. Hiyo ilifanya habari hizi
zisambae kwa watu wengi sehemu mbalimbali. Asubuhi ya tarehe 13, watoto wale
walitekwa na meya wa Vila Nova de Ourem, Arturo Santos. Walihojiwa juu ya siri
walizokuwa wanazijua lakini waligoma kabisa kusema. Watekaji walijaribu
kiuwahonga fedha na hata kuwatishia kifo, lakini hawakusema kabisa.
Agosti 19, Lucia, Francisco na Jacinta walikuwa pamoja kwenye eneo
linaloitwa Valinhos, karibu na Fatima wakati wa mchana. Walimwona tena Maria
ambaye aliwaambia: "Nendeni tena Cova da Iria tarehe 13 na kuendelea
kusali rozari kila siku." Maria akasema kuwa angefanya muujiza ili watu
waamini, na kama watoto wale wasingekuwa wametekwa, basi huo muujiza ungekuwa
mkubwa zaidi.
Tarehe 13 Septemba kundi kubwa la watu
lilikusanyika Fatima. Mchana hao watoto walifika na waliweza kumwona Mama Bikira Maria
(lakini si watu wengine). Alimwambia Lucia:
"Endeleeni kusali rozari ili kukomesha vita. Mwezi wa Oktoba Bwana wetu atakuja
pamoja na Mama yetu wa huzuni na Mama yetu wa Karmeli (Our Lady of Dolours and
Our Lady of Carmel). Mtakatifu Yohana atatokea pamoja na mtoto Yesu ili
kuibariki dunia ....”
Tarehe 13 Oktoba 1917 watu wengi sana walikusanyika Cova. Wengi walienda
wakiwa hawajavaa viatu huku wakisali rozari kama namna ya kuonyesha unyenyekevu
kwa Maria. Mchana watoto wale walimwona Maria.
Kwa mara nyingine tena mtoto Lucia alimwuliza swali lilelile la siku zote:
Unataka nini? Akasema: Nataka kukuambia kwamba kanisa
lijengwe hapa kwa heshima yangu. Mimi ndimi Mama wa Rozari. Endeleeni
kila wakati kusali rozari kila siku. Vita vitakwisha, na askari watarudi hivi
karibuni nyumbani kwao.” Baadaye alianza kupaa kwenda juu kuelekea kwenye jua.
Kanisa lilikaa kimya kuhusu maono ya Fatima hadi ilipofika Mei 1922
ndipo Askofu Correia alitoa barua ya kichungaji juu ya jambo hili; akisema
kwamba angeunda tume ya kuchunguza suala hili. Mwaka 1930 alitoa barua nyingine
ambayo, pamoja na mambo mengine, ilisema:
“Kulingana na masuala ambayo yamewekwa wazi, pamoja na mengine
ambayo hatutayataja kwa lengo la kufupisha taarifa hii; huku tukimsihi Roho wa
Kiungu na kujiweka chini ya ulinzi wa Bikira Mtakatifu sana, na baada ya
kusikiliza maoni ya mapadri Washauri katika jimbo hili:
Mwanzo wa uwepo wa jina Bikira Maria wa FatimaBikira Maria wa Fatima yaani jina rasmi: Bibi Yetu wa Rosari takatifu wa Fatima Nossa Senhora do Rosário de Fátima.Jina mojawapo la Bikira Maria lililotokana na njozi maarufu mnapo mwaka 1917 walizozisimulia watoto watatu wa Fatima huko Ureno: yaani Lusia Santos pamoja na binamu zake Yasinta Marto na Fransisko Marto.
Inasemekana hizo njozi zilithibitishwa na Kanisa Katoliki kuwa za kuaminika mpaka ilianzishwa kumbukumbu yake katika liturujia kila tarehe ya ile ya kwanza, 13 Mei.Papa Pius XII tarehe 13 Mei 1946 alikubali rasmi Sanamu iliyotengenezwa kutokana na masimulizi hayo itiwe taji.Mnamo tarehe 11 Novemba 1954, alitangaza patakatifu pa Fatima kuwa basilika kwa hati Lucer Superna.
read more:
- Tunatangaza kuwa maono ya watoto wachunga kondoo kule Cova de Iria, parokia ya Fatima, katika jimbo hili, yaliyoanza tarehe 13 Mei hadi tarehe 13 Oktoba 1917 yanastahili kuaminiwa.
- Tunaruhusu rasmi imani ya Mama Yetu wa Fatima.
Inasemekana hizo njozi zilithibitishwa na Kanisa Katoliki kuwa za kuaminika mpaka ilianzishwa kumbukumbu yake katika liturujia kila tarehe ya ile ya kwanza, 13 Mei.Papa Pius XII tarehe 13 Mei 1946 alikubali rasmi Sanamu iliyotengenezwa kutokana na masimulizi hayo itiwe taji.Mnamo tarehe 11 Novemba 1954, alitangaza patakatifu pa Fatima kuwa basilika kwa hati Lucer Superna.
read more:
No comments:
Post a Comment