Monday, August 14, 2017

Maisha ya Mtakatifu Maksimiliano Maria Kolbe(Life of Saint Maximilian Maria Kolbe)

Tarehe 14 Augost ni Kumbukumbu ya Mtakatifu Maksimiliano Maria Kolbe
Image result for Image of Saint Maximilian Maria KolbeMtakatifu Maximilian Maria Kolbe alizaliwa tarehe 8 January 1894 na kufariki tarehe 14 Agost 1941mtakatifu huyu  alikuwa padre wa Kanisa Katoliki na mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo Wakoventuali  kutoka nchi ya Poland.

Katika historia ya Kanisa  inaonesha  kwa jinsi gani Mtakatifu Maximiliani Maria Kolbe allivyomheshimu Mama Bikira Maria kwa jina la Immakulata, ikiimnisha Mkingiwa Dhambi Ya Asili.
Baada ya kuanzisha chama cha Mashujaa wa Imakulata  huko Roma inchini Italia  na Mji wa Imakulata  huko Polandi, alikwenda Japani  kama mmisionari .
Wakati wa Vita Kuu ya pili ya Dubia Mtakatifu Maximiliana Maria Kolbe alifungwa na wafuasi wa nazi katika kambi ya wafungwa wa siasa  kule Auschwitz. Hatimaye alijitolea kushika nafasi ya mfungwa mwenzake aliyechaguliwa kuachwa bila ya chakula hadi kufa pamoja na wengine 9. Aliwaandaa hao wote kukabili kifo kwa tumaini la Kikristo na bila ya chuki, na alipobaki peke yake aliuawa kwa sindano ya sumu.

Mtakatifu Maximiliana Maria Koble alitangazwa kuwa mtakatifu mfiadini Mwaka 1982 na Papa Yohane Paulo II ambaye naye kwa sasa ni Mtakatifu alitangazwa. Sikukuu yake ni tarehe 14 Agosti kila mwaka

Maisha yake awali.
Mtakatifu Maximiliana Maria Koble.Inaonesha alijulikana kama Raymund Kolbe ambapo alizaliwa hiyo tarehe 8 Januari 1894  katika  Zdunska Wola ambapo ilikuwa Imaya ya Falme ya Poland(then part of the Russian Empire). Baba yake alikuwa Ujerumani na mama yake Mpoland. Wazazi wake walikuwa maskini na mwaka 1914 baba yake inasemekana alikamatwa na Warusi kwenye mapigano ya Uhuru inchini Poland.Mtakatifu Maxiliani Maria Kolbe ni mtakatifu aliyechagua kuishi kwa kufuata Mama Bikira Maria na kuishi utakatifu
    
Sala yake.
Wewe umenipenda milele, tangu u Mungu; hivyo umenipenda na utanipenda milele!...
Upendo wako kwangu ulikuwepo hata kabla sijakuwepo, na ni kwa sababu ya kunipenda, Mungu mwema, kwamba umeniita kutoka utovu wa vyote nianze kuwepo!

Reference:https://en.wikipedia.org/wiki/Maximilian_Kolbe
More reading:

Who is Saint Maximilian Kolbe? – Marytown

Maximilian Kolbe Biography | Biography Online

Prayers to St. Maximilian Kolbe - Militia of the Immaculata

 

 

 

No comments:

Post a Comment