Mtakatifu Anna ni Mtakatifu aliyemzaa Mama Bikira Maria pamoja na mmewe Mtakatifu Yohakimu.Jina Anna likitoka kwenye Kiebrania Hannah חַנָּה, yaani "fadhili".Mtakatifu Anna anaheshimiwa kama mama wa Bikira Maria na bibi wa Yesu kadiri ya mapokeo ya Ukristo na Uislamu, ingawa hatajwi katika Biblia wala katika Kurani, isipokuwa katika kitabu cha karne ya 2 kinachoitwa Injili ya Yakobo kadiri ya Maandiko.Mtakatifu Anna pamoja mmewe Mtakatifu Yohakimu wote wawili wanaheshimiwa kama watakatifu katika madhehebu mengi ya Ukristo, hasa tarehe 26 Julai.
No comments:
Post a Comment