Thursday, August 24, 2017

MTAZAMO WANGU KUHUSU SIFA ZA PADRI

Padri ni mwanadamu ambaye amepewa  mamlaka na kibali cha KIMUNGU kutekeleza kazi mbalimbali za kiroho katika kumpendeza Mungu na hatimaye kufikia Mbinguni. Huyu mwanadamu mara nyingi anatekeleza kazi za kumwakilisha Yesu Kristu alizoziagiza toka mwanzo wa Ukristo kuanzishwa na hasa aliwapatia mamlaka yote pale alipowakabidhi mitume.

Tunapoangalia cheo hiki kilikabidhiwa kwa wanaume kutekeleza hili jukumu na tukiangalia Yesu akuwapatia wanawake hili jukumu na aimanishi wamama aliwatenga  bali alitoa mamlaka kwao watekeleze hili na hakina mama watekeleze jukumu lingine kwa kuwa viungo vyote sawa ila katika kutenda tofauti ndani ya mwili mmoja ndivyo hata hiki cheo kilivyo.

Mara nyingi kama waumini tunayo haki ya kuwaheshimu sana hata wakiwa na mapungufu ya kiubinadamu kwa kuwa niwapakwa mafuta na wanatekeleza badala ya Yesu mwenyewe.Padri anaweza kukusaidia mwanadamu kuhufikia utakatifu kwa njia ya kitubio,sala na majitolea ambayo yanamchango mkubwa wa kiroho.Pia ndo mtu pekee anayeweza kumshusha Yesu moja kwa moja wakati wa ibada takatifu hasa wakati wa mageuzo.Kingine anaweza kutoa baraka na kutoa rahana pia pamoja Mapadri hao hao ndio watoaji wakuu wa sakrament zote zilizopangwa na kanisa mama.

Hitimisho:Katika kuhitimisha mtazamo wangu napenda kusema hivi Mapadri lazima tuwaombee ili wabaki katika kuutukuza ufalme wa Mungu na kuendelea kuwa chachu ya utakatifu kwa wanadamu wote kwa kuwa wakipotea dunia nayo itapotea pia.Lakini wanadamu tusiwe chanzo cha kuwafanya Mapadri wetu kuanguka kwa kuwa wamebeba jukumu zito hapa duniani zaidi ya wanadamu wote.
Picha ya Francis Mushi


LITANIA YA KUWAOMBEA MAPADRE WOTE

Kwa ajili ya Baba Mtakatifu wetu ..(N); Bwana, umpe moyo wako wa uchungaji mwema
Kwa ajili ya makardinali na maaskofu wakuu; Uwape moyo wa kichungaji ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre wa majimbo; Uwajaze na Roho wako ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre watawa; Wakamilishe katika wito wao ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre walioko hatarini; Uwaokoe ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre wenye udhaifu; Uwatie nguvu ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre wenye hofu; Uwape amani ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre waliokata tamaa; Uwavuvie upya ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre wakaao upweke; Uwasindikize ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre wamisionari; Uwalinde ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre wanaohubiri; Uwaangazie ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre na watawa waliokufa; Uwafikishe kwenye utukufu wako ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre wote; Wajalie hekima na ufahamu wako ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre wote; Uwajalie elimu na shauri lako
Kwa ajili ya mapadre wako; wajalie wakuheshimu na wakuogope
Kwa ajili ya mapadre wote; Wajalie subira na upendo
Kwa ajili ya mapadre wote; wajalie utii na upole
Kwa ajili ya mapadre wote; uwajalie hamu kuu ya kuokoa roho za watu
Kwa ajili ya mapadre wote; wape fadhila za imani, matumaini na mapendo
Kwa ajili ya mapadre wote; Wajalie upendo mkuu kwa Ekaristi
Tunakuomba uwajalie mapadre wote; Waheshimu uhai na hadhi ya mtu ee Bwana
Tunakuomba uwajalie mapadre wote nguvu na bidii katika kazi zao ee Bwana
Tunakuomba uwajalie mapadre wote amani katika mahangaiko yao ee Bwana
Tunakuomba uwajalie mapadre wote upendo mkuu kwa Utatu Mtakatifu ee Bwana
Tunakuomba uwajalie mapadre wote upendo mkuu kwa Bikira Maria ee Bwana
Uwajalie mapadre wote wawe mwanga wa Kristo ee Bwana
Uwajalie mapadre wote, wawe chumvi kwa ulimwengu ee Bwana
Uwajalie mapadre wote, wajizoeze kujitoa sadaka na kujinyima ee Bwana
Uwajalie mapadre wote, wawe watakatifu kimwili, kiakili na kiroho ee Bwana
Uwajalie mapadre wote wawe watu wa sala ee Bwana
Uwajalie mapadre wote wawe kioo cha imani kwako ee Bwana
Uwajalie mapadre wote wajali sana wongofu wetu ee Bwana
Uwajalie mapadre wote wawe waaminifu kwa wito wao wa kikuhani ee Bwana
Uwajalie mapadre wote, ili mikono yao ibariki na kuponya ee Bwana
Uwajalie mapadre wote wawake moto wa mapendo yako ee Bwana
Uwajalie mapadre wote hatua zao zote ziwe kwa ajili ya utukufu wa Mungu ee Bwana
Uwajalie mapadre wote wajazwe na Roho Mtakatifu na uwajalie karama zake kwa wingi ee Bwana.
Tuombe.
Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, usikie sala tunazokutolea kwa ajili ya mapadre wetu. Uwajalie wafahamu waziwazi kazi uliyowaitia kuifanya, uwape neema zote wanazohitaji ili waitikie wito wako kwa ushujaa, kwa upendo, na majitoleo yenye udumifu katika mapenzi yako matakatifu. Amina.




No comments:

Post a Comment