Tunapokumbuka siku ya kupalizwa kwa Mama Bikira Maria tarehe 15 Agost kila mwaka kuna mambo mengi inabidi kujifunza na kuwa na imani kubwa juu yake kwa kuwa kupitia ukaribu wake na Mungu Mwana,Mungu Baba na Mungu Roho Mtakatifu sisi binadamu tunapata uwepesi wa kusikilizwa maombi yetu kwa kuwa Mama anatukamilishia maombi yetu ambayo mara nyingi sala za kibinadamu zinamapungufu mengi na pengine tunakuwa atuna mastaili yetu.
Mara nyingi baadhi yawanadamu wanakosea kwa kusema Mama Bikira Maria anaabudiwa hii dhana si kweli.Mama Bikira Maria aabudiwi bali anaheshimiwa na ni haki kumheshimu kwa kuwa ndo kiungo muhimu katika historia ya ukombozi wa mwanadamu na tunamheshimu kwa maana Alikubali kupata mateso makali na kushiriki hatua zote za ukombozi.
Ukijaribu kutafakari huyu mama alikubali kubeba Mimba ya Mkombozi pia aliangaika katika nafasi mbalimbali kama mzazi wakati wa makuzi ya Mkombozi wetu.Baadhi ya misukasuko ni kama ule aliupopata wakati hakiwa na Mtakatifu Yoseph walipokuwa wanatafuta nyumba ya wageni huko mjini Elizabeth mpaka kulazimika kujifungulia kwenye holi la mifugo.Tena pale Bwana Yesu alipopotea kwa mda wa siku tatu na pale alipokuwa Bwana Yesu anapelekwa kuawa haya matukio ambayo kwakweli anastaili heshima kubwa.Ikumbukwe Yesu alipokuwa msalabani alikabidhiwa wanadamu wote ili aendelee kuwasimamia na kuwaombea pia kwa maneno yasemayo "Mama mtazame mwanao na Mwana mtazame mama yako".
Hakina jina la Mama Bikira Maria lazima lipate heshima ya pekee na ndo maana ilimpendeza Mwenyezi Mungu kumpaliza Mama Bikira Maria mwili na Roho.Sasa inakuwaje sisi wanadamu tusimpe heshima ya pekee? Fikiria siku ile ya harusi ya kana Bwana Yesu aliweza kubadilisha maji na kuwa divai kwa kupitia ombi la Mama Yetu Bikira Maria na inaonesha saa yake Yesu kufanya hivyo ilikuwa bado na ukirejea yale maneno aliyoyatamka Yesu"Mama unanini na mimi?" Lakini kwa kumhemu Mama yake alitii na kutekeleza.
Mwanadamu badilika achana kumzalau huyu mama kwa kujisemea kama alitumika tu hakika tunakuwa tunafanya kufuru hata mbele za Mungu kwa kuwa alipewa heshima ya pekee mpaka kumchaguwa awe Mama wa Mkombozi wetu ambaye kila goti linapigwa kupitia ujumbe ulioletwa na Malaika Gabriel pale alipotumwa kuambia atabeba mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.Huyu Mama akusita aliitikia na kusema maneno haya"Mimi ni mjakazi wa Bwana nitendewe alivyosema".Huu ni ujasiri mkubwa kuupokea huu ujumbe na lilikuwa jukumu kubwa na zito.
Jina Bikira Maria ni jina tukufu sana huko Mbinguni na hapa duniani kwa kuwa Malaika na Watakatifu wanaliheshimu na Ni Malkia wa viumbe wote.
Hakika tuendelee kumuomba huyu Mama na kumheshimu aendelee kutuombea kwa Kwa Mwanae Yesu nasi tutapata mastaili zaidi kupitia sala tumuombao huyu mama atatukamilishia.
NITAKUSHUKURU NA KUKUHESHIMU NA KUKUOMMBA MILELE YOTE MAMA KWA MAANA UMENIPATIA MASTAILI MENGI NA KUNIKAMILISHIA MAOMBI YANGU
Tusikilize nyimbo za kumsifu na Kumheshimu huyu Mama yetu
The Holy Rosary - Prayers - Catholic Online
Our Lady Of The Rosary Novena - EWTN.com
Prayers to Mary - Mary Pages
Litany of the Blessed Virgin Mary - Prayers - Catholic Online
↑↑→←
No comments:
Post a Comment