Mtakatifu Yohane Maria Vianney alitangazwa kuwa mwenye heri na Papa Pius XI Tarehe 8 Januari 1905 na baadae alikuja kumtangaza kuwa mtakatifu mwaka 1925 na baadae mwaka 1929 aliwekwa kuwa msimamizi wa maparokia.Inasemekana aliishi kwa moyo wa kujitoa zaidi katika kuudumia waumini katika maswala ya maungamo huku akifunga mara kwa mara na kuwaombea waumini ili wawe katika muenendo wa kumpendezesha Mungu. Katika kuteleza shughuri za kichungaji alianza akiwa na miaka 29 akiwa anatekeleza baadhi na majukumu zaidi yalianza akiwa na miaka 32.
Sala za Mtakatifu Yohane Maria Vianney
Nakupenda, Bwana, na neema pekee ninayokuomba, ni kwamba nikupende milele...
Mungu wangu, ikiwa ulimi wangu hauwezi kukariri kila nukta kwamba nakupenda, nataka moyo wangu ukuambie tena na tena kila ninapopumua.
Yesu wangu, jinsi inavyopendeza kukupenda!
Unijalie niwe kama wanafunzi wako juu ya mlima Tabori, nikikuona wewe tu, Mwokozi wangu.
Tuwe kama marafiki wawili ambao hata mmojawao hawezi kukubali kumchukiza mwingine. Amina
For reading again click here again:
No comments:
Post a Comment