Mtakatifu Fransis wa Asis alizaliwa mwaka 1181 ambapo ni moja ya familia iliyokuwa na watoto Saba. Baba yake alikuwa anaitwa Pietro di Berdanode na mama yake alikuwa anaitwa Pica Bourlemont.Mtakatifu Fransis wa Asis alifariki mwaka 1226 tarehe 3 oktoba.
Inasemekana Mtakatifu Fransis wa Asis alizaliwa wakati baba yake akiwa katika safari zake za kibiashara. Maandiko yanatuambia wakati amezaliwa mama yake alitamani awe mmoja wa kiongozi wa kidini na huku baba yake akitamani awe mfanyabiashara.
Mtakatifu Fransis alikuwa mmoja ya watu wanyenyekevu toka Utotoni na mpole pia alikuwa mfano bora kama kiongozi.Mtakatifu Fransis wa Asisi aliamua kuachana na utajiri wa wazazi wake na kuamua kuanzisha Shirika la Kitawa la Ndugu Wadogo.Kitendo hiki kilimfanya Mtakatifu Fransis wa Asis kuwa katika Migogoro na baba yake zaidi anakumbukwa jinsis alivyoishi maisha ya umaskini kwa namna alivyochagua licha ya utajiri uliokuwepo kwa wazazi wake huku alikuwa akiishi kando ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro akiwa anawaombea wahitataji na wenye shida mbalimbali.
Sikukuu yake inaazimishwa tarehe 4,Octoba kila mwaka
For more reading: click that link referenced:
No comments:
Post a Comment