Mama Tereza alipofikia umri wa miaka 18 alijiunga na shirika la Masista wa Loreta huko Ireland na ilipofika mwaka 1929 alitumwa Uhindini ili afundishe kwenye shule ya masista katika mji wa Kolkata na mpaka kufikia kuwa mkuu wa shule.Katika kuishi kwake aliguswa sana na hali ya mafukara nje ya shule akajisikia wito wa kuwasaidia na kuishi pamoja nao.
Alipata kibali cha wakuu wa shirika lake na wa Kanisa mwaka 1948 alitoka jumuiya ya Loreto na kuanzisha maisha duni kati ya wakazi wa mitaa ya vibanda.
Alianzisha shule lakini baada ya muda alitambua umuhimu wa kuzingatia zaidi hali ya watu ambao walikuwa wagonjwa na hatimaye kufa katika mitaa hiyo.
Katika mwaka 1950 Mtakatifu Mama Tereza alianzisha shirika la Masista wamisionari wa Upendo ambalo mwanzoni lilikuwa jumuiya ndogo ya masista 12 tu.Kati ya kazi zao za kwanza ilikuwa nyumba kwa watu mahtuti; masista waliwakusanya wakiwa wamelala barabarani na kuwapeleka katika nyumba hiyo walipopata dawa, chakula na usaidizi mwingine.
Shirika lilikua haraka sana ambalo Mtakatifu Mama Tereza; hadi leo inasemekana kuna masista 4,500 kwa jumla katika matawi mengi kote ulimwenguni.Wanaendesha nyumba kwa watoto yatima, wagonjwa wa Ukimwi, wenye ukoma, walemavu, walevi, wenye kichaa na kila aina ya matatizo maishani. Kwa kazi hizi alitunukiwa Tuzo ya Nobel ya Amani mwaka 1979.Mama Teresa aliaga dunia tarehe 5 Septemba 1997 na kufanyiwa mazishi ya kitaifa.
Tarehe 19 Oktoba 2003 Papa Yohane Paulo II alitangaza Mama Tereza na kuwa mwenye heri. Baada ya kutokea muujiza wa pili kufanywa na Mungu kwa maombezi yake, na hatimaye Papa Fransisko amemtangaza kuwa mtakatifu tarehe 4 Septemba 2016. Sikukuu yake inaazimishwa kila mwaka tarehe 5 Septemba. Siku hiyohiyo ambayo ilitangazwa na mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa siku ya kimataifa ya Upendo kuanzia mwaka 2013.
Sala zake
Baba yetu, mwanao nipo hapa, tayari kwako unitumie ili kuendelea kupenda ulimwengu kwa kuupatia Yesu na, kwa njia yangu, kumtoa kwa kila mmoja na kwa ulimwengu.Ee Bwana, utufanye tustahili kutumikia watu wenzetu ambao ulimwenguni kote wanaishi na kufa kwa ufukara na njaa.
Kwa mikono yetu uwape leo mkate wao wa kila siku; na kwa upendo wetu wenye kuelewa uwape amani na furaha.
Ee Bwana wangu, nakupenda, Mungu wangu, najuta, Mungu wangu, nakuamini, Mungu wangu, nakutumainia.
Utusaidie kupendana unavyotupenda.
Bwana Yesu, wewe ambaye uliumba kwa upendo, ulizaliwa kwa upendo, ulitumikia kwa upendo, ulitenda kwa upendo, uliheshimiwa kwa upendo, uliteseka kwa upendo, ulikufa kwa upendo, ulifufuka kwa upendo, nakushukuru kwa upendo wako kwangu na kwa ulimwengu wote, na kila siku nakuomba: unifundishe mimi pia kupenda! Amina
for more:
ST. MOTHER TERESA OF CALCUTTA NOVENA PRAYERS
references:www.bbc.com/swahili/habari-37270128.
https://sw.wikipedia.org/wiki/Mama_Teresa
Pray for us
ReplyDelete