Wednesday, August 30, 2017

Maisha ya Mtakatifu Ignatius wa Loyola(Life of Saint Ignatius de Loyola)

Mtakatifu Ignatius wa Loyola alizaliwa kwenye mji huitwao Loyola,Guipuzco mwaka 1491 nchini Hispania na alifariki tarehe 31 Julai 1557 kwenye mji wa Roma nchini Italia .

Mtakatifu Ignatius wa Loyola alikuwa Padri wa Kanisa Katoliki na nimaarufu hasa kama mwanzilishi wa Shirika la Yesu na niwa mtindo wa Mazoezi ya kiroho na Papa Paulo V kuwa mwenye heri tarehe 27 Julai 1609 na baadae alitangazwa kuwa mtakatifu tarehe 12 Machi 1622 na Papa Paulo V.

Sala ya Mtakatifu Ignatius wa Loyola 
Pokea, Bwana, hiari yangu yote.
Pokea kumbukumbu, akili na utashi wote.
Vyovyote nilivyonavyo au kuvimiliki nimejaliwa na wewe: nakurudishia vyote na kuukabidhi utashi wako uvitawale.

Unijalie tu upendo wako na neema yako, nami nitakuwa tajiri kutosha, nisitamani kitu kingine chochote.

St. Ignatius Loyola - Saints & Angels - Catholic Online

Who was St. Ignatius Loyola? - Xavier University

 


No comments:

Post a Comment