Tuesday, August 29, 2017

Chakula cha Mkatoliki kila Siku

 Image result for sala za jioni za katoliki
Sala za Asubuhi
Ee Baba yetu Mungu Mkuu, Umenilinda usiku huu, Ninakushukuru kwa moyo, Ee Baba, Mwana na Roho, Nilinde tena siku hii, Niache dhambi nikutii, Naomba sana Baba wee, Baraka yako nipokee, Bikira safi ee Maria, Nisipotee unisimamie, Mlinzi Mkuu Malaika wee, Kwa Mungu wetu niombee, Nitake nitende mema tu, Na mwisho nije kwake juu, Amina.

Nia Njema
Kumheshimu Mungu wangu, Namtolea roho yangu, Nifanye kazi nipumzike, Amri zake tu nishike, Wazo neno tendo lote, Namtolea Mungu pote, Roho, mwili chote changu, pendo na uzima wangu, Mungu wangu nitampenda, Wala dhambi sitatenda, Jina lako nasifia, Utakalo hutimia, Kwa utii navumilia, Teso na matata pia, Nipe Bwana neema zako, Niongezee sifa yako, Amina.
Sala ya matoleo
Ee Yesu kwa mikono ya Bikira Maria, na kwa maungamo na sadaka yako kuu, ninakutolea sala, matendo, masumbuko na furaha zangu zote za leo. Ee Yesu, ufalme wako utufikie


Baba yetu
Baba Yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe; Ufalme wako ufike, Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku, Utusamehe makosa yetu, Kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, Lakini utuopoe maovuni. Amina.

Salamu maria
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.

Kanuni ya imani
Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi,/ mwumba mbingu na dunia./ Na kwa Yesu Kristu, Mwanaye wa pekee, Bwana wetu;/ aliyetungwa kwa Roho Mtakatifu,/ akazaliwa na Bikira Maria,/ akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato,/ akasulubiwa, akafa, akazikwa,/ akashukia kuzimu;/ siku ya tatu akafufuka katika wafu;/ akapaa mbinguni;/ amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi;/ toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu,/ Kanisa takatifu katoliki,/ ushirika wa Watakatifu,/ maondoleo ya dhambi,/ ufufuko wa miili,/ uzima wa milele. Amina.


Amri Za Mungu
1. ndimi bwana mungu wako, usiabudu miungu wengine. 2. usilitaje bure jina la mungu wako. 3. shika kitakatifu siku ya mungu. 4. waheshimu baba na mama, upate miaka mingi na heri duniani. 5. usiue 6. usizini 7. usiibe 8. usiseme uongo 9. usitamani mwanamke asiye mke wako 10. usitamani mali ya mtu mwingine

Amri Za Kanisa
1. hudhuria misa takatifu dominika na sikukuu zilzoamriwa 2. funga siku ya jumatano ya majivu; usile nyama siku ya ijumaa kuu 3. ungama dhambi zako walau mara moja kila mwaka 4. pokea ekaristi takatifu hasa wakati wa pasaka 5. sadia kanisa katoliki kwa zaka 6. shika sheria katoliki za ndoa

Sala Ya Imani
mungu wangu, nasadiki maneno yote linalosadiki , na linalofundisha kanisa katoloki  la roma:kwani ndiwe uliyefundisha hayo,wala hudanganyiki, wala hudanganyi.amina

Sala Ya Matumaini
mungu wangu, natumaini kwako nitapewa kwa njia ya yesu kristu,neema zako duniani na utukufu mbinguni, kwani ndiwe uliyeagana hayo nasi, nawe mwamini.amina

Sala Ya Mapendo
mungu wangu, nakupenda zaidi ya cho chote, kwani ndiwe mwema mwema, ndiwe mwenye kupendeza. nampenda na jirani yangu kama nafsi yangu, kwa ajili yako.amina.

Sala Ya Kutubu
mungu wangu, nimetubu sana dhambi zangu, kwani ndiwe mwema ndiwe mwenye kupendeza, wachukizwa na dhambi. basi sitaki kukosa tena, nitafanya kitubio, naomba neema zako nipata kurudi amina.

Sala Kwa Malaika Mlinzi
malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote za roho na za mwili amina

Sala ya Malaika wa Bwana.
Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria, naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Salamu Maria,…. Ndimi Mtumishi wa Bwana, nitendewe ulivyonena. Salamu Maria, …… Neno wa Bwana akatwaa Mwili, akakaa kwetu. Salamu Maria, ….. Utuombee, ee Mzazi Mtakatifu wa Mungu, tujaliwe ahadi za Kristo. Tuombe: Tunakuomba ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika, kwamba, Kristo Mwanao amejifanya mtu: kwa mateso na Msalaba wake, utufikishe kwenye utukufu wa ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu, Amina.


Malkia wa Mbingu

Malkia wa mbingu, furahi, aleluya. Kwani uliyestahili kumchukua, Aleluya. Amefufuka alivyosema, Aleluya. Utuombee kwa Mungu, Aleluya. Furahi shangilia, ee Bikira Maria, Alaluya. Kwani hakika Bwana amefufuka Aleluya. Tuombe. Ee Mungu, uliyependa kuifurahisha dunia kwa kufufuka kwake Bwana wetu Yesu Kristu, Mwanao: fanyiza, twakuomba, kwa ajili ya Bikira Maria, tupate nasi furaha za uzima wa milele. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina.

Sala za Jioni
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Sala ya Kushukuru.

Tunakushukuru, ee Mungu, kwa mapaji uliyotujalia leo. Amina.
Baba yetu . . .
Salamu Maria . . .
Atukuzwe Baba . . .
Sala ya Imani.

Mungu wangu, nasadiki maneno yote. Linayosadiki na linayofundisha Kanisa Katoliki la Roma. Kwani ndiwe uliyetufumbulia hayo. Wala hudanganyiki, wala hudanganyi. Amina.
Sala ya Matumaini.

Mungu wangu, natumaini kwako, nitapewa kwa njia ya Yesu Kristo. Neema zako hapa duniani, na utukufu mbinguni. Kwani ndiwe uliye agana hayo nasi, nawe mwamini. Amina.
Sala ya Mapendo.

Mungu wangu, nakupenda zaidi ya chochote. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Nampenda na jirani yangu, kama nafsi yangu, kwa ajili yako. Amina.
Kutubu dhambi.

Tuwaze katika moyo wetu makosa ya leo tuliyomkosea Mungu kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo na kwa kutotimiza wajibu. (Husubiri kidogo).
Nakuungamia Mungu Mwenyezi, nanyi ndugu zangu, kwani nimekosa mno, kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo, na kwa kutotimiza wajibu.
Nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana. Ndiyo maana nakuomba Maria mwenye heri, Bikira daima, Malaika na Watakatifu wote, nanyi ndugu zangu, niombeeni kwa Bwana Mungu wetu.

Mungu Mwenyezi atuhurumie, atusamehe dhambi zetu, atufikishe kwenye uzima wa milele. Amina.
Sala ya kuombea watu.

Ee Mungu, nawaombea watu wa nchi hii, wapate kusikia maneno yako na kukupenda wewe Bwana Mungu wetu.
Sala kwa Malaika Mlinzi.

Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote za roho na za mwili. Amina.
Malaika wa Bwana (kipindi kisicho cha Pasaka)

Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria.
Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
Salamu, Maria,.....
Ndimi mtumishi wa Bwana.
Nitendewe ulivyonena.
Salamu, Maria....
Neno la Mungu akatwaa mwili.
Akakaa kwetu.
Salamu, Maria....
Utuombee, Mzazi mtakatifu wa Mungu.
Tujaliwe ahadi za Kristu.

Tuombe:
Tunakuomba, Ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika kwamba Mwanao amejifanya Mtu kwa mateso na msalaba wake tufikishwe kwenye utukufu na ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. AMINA.
AU;

Malaika wa Mbingu (kipindi cha Pasaka)

Malkia wa mbingu, furahi, aleluya.
Kwani uliyestahili kumchukua, Aleluya.
Amefufuka alivyosema, Aleluya.
Utuombee kwa Mungu, Aleluya.
Furahi shangilia, ee Bikira Maria, Alaluya.
Kwani hakika Bwana amefufuka Aleluya.
Tuombe.
Ee Mungu, uliyependa kuifurahisha dunia kwa kufufuka kwake Bwana wetu Yesu Kristu, Mwanao, fanyiza, twakuomba, kwa ajili ya Bikira Maria, tupate nasi furaha za uzima wa milele. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina.

Atukuzwe (mara tatu)

Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Kama mwanzo na sasa na siku zote na milele. Amina.
Kujikabidhi

Enyi Yesu, Maria na Yosefu nawatolea moyo na roho na uzima wangu!
Enyi Yesu, Maria na Yosefu mnijilie saa ya kufa kwangu!
Enyi Yesu, Maria na Yosefu mnijalie nife mikononi mwenu!
(Rehema ya siku 300).
Wimbo:

Kwa heri Yesu mpenzi mwema,
Naenda usiudhike mno.
Nakushukuru, nakupenda,
Kwa hizo nyimbo za mwisho.
Asubuhi nitarudi.
Yesu kwa heri.
Kwa heri Mama mtakatifu,
Sasa napita pumzika.
Asante kwa moyo na nguvu,
Leo umeniombea.
Asubuhi nitarudi.
Mama kwa heri.
Kwa heri Yosefu mnyenyekevu,
Kazi zatimilizika.
Kama mchana, leo usiku,
Nisimamie salama.
Asubuhi nitarudi.
Yosefu kwa heri.
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Kuomba Ulinzi wa Usiku


Mungu wangu naenda kulala naomba malaika 14, waende nami, wawili juu, wawili chini, wawili upande wa kuume, wawili upande wa kushoto, wawili wanifunike, wawili waniamshe, wawili wanipeleke juu mbinguni. Mimi mtoto mdogo, roho yangu ni ndogo, haina nafasi kwa mtu yoyote ila kwa Yesu pekee. Amina.

Image result for image of nature


No comments:

Post a Comment