Kabla ya kuchaguliwa kama Papa, Mtakatifu Pius X aliwahi kuwa paroko, na baadae askofu wa Mantua kuanzia mwaka 1884, halafu Patriarki (askofu mkuu) wa Venice kuanzia mwaka 1893. Hivyo maisha haya yanaonesha alikuwa na mang'amuzi mengi mengi ya kichungaji. Alimfuata Papa Leo XIII na kufanikiwa kuvishwa taji tarehe 9 Agosti 1903, wa kwanza katika karne ya 20 na baadae Papa Benedikto XV
.
Kadiri ya maandiko yanatueleza kuwa katika uchaguzi makardinali walimpiga kura kwanza mwenzao Rampolla, lakini aliwekewa kura ya turufu na Kaisari wa Austria-Hungaria , mara alipochaguliwa Pius X alifuta haki hiyo ya Kaisari na kuamua atengwe na Kanisa Katoliki yeyote atakayeingilia tena uchaguzi wa Papa.
Lengo la Mtakatifu Papa Pius X lilifafanuliwa na kaulimbiu yake: "Instaurare omnia in Christo" akiimanisha kukamilisha yote ndani ya Kristo.Hakika Mtakatifu Pius X alijitahidi kuleta hali mpya katika Kanisa, ingawa ilimbidi pia apambane na uzushi wa aina mbalimbali zilizotaka kulilinganisha mno na ulimwengu kwa kuenda na usasa.
Kati ya mambo muhimu zaidi ya upapa wake ni Katekisimu mpya, urekebisho wa liturujia, ruhusa ya kupokea ekaristi kwa watoto, na pia Mkusanyo wa Sheria za Kanisa , ambao ulifanyika kwa mara ya kwanza na kufuata mtindo wa sheria za nchi nyingi (code).
Alijitahidi pia kuzuia vitu vikuu vya kwanza , lakini ikashindikana. Inasemekana akafa kwa uchungu huo.
Mtakatifu Papa Pius X alitangazwa kuwa mtakatifu mwaka 1954 na Papa Pius XII .
More reading click here:
No comments:
Post a Comment